Nini maoni yako kuhusu video assistant Referees?

Mtazoea tu! Hata tennis na rugby walilalamika mwanzo!
 
Inapungusha amsha amsha na kamushange ya football
 
Hii nimeipenda kulikuwa na udanganyifu mwingi sana katika mabao ya kuotea. Wanaosema imepunguza msisimko ni vigeugeu maana timu yake ikifungwa goli la offside mpaka matusi ya nguoni yanamtoka lakini wakifunga la offside wanasema inaondoa msisimko.
kweli kabisa waache unafki ......hii ni hatua nzuri sana kwa haki fifa safi
 
Technology safi sana, watu muache kelele kumlaumu refa, ila kazi ni ngumu, msikae mkadhani wanakataa magoli burebure tu, wanakua wamefanya careful analysis hadi kufikia hiyo conclusion. Kama hujui sheria za mpira ukae tu kimya sio kujifanya umekua refa.
 
Mmesikia FA itaanza kuchezwa dakika 60 badala ya 90?
 
Ila yote tisa raha ya mpira bana kuwe na magoli ya utata..bila kujali umefunga au ndo umefungwa hapo ndo mpora unanoga.. Unakuta mpira haujavuka mstari watu wanashangilia goli tayari na refa akishasema mpira kati ngoma inogile..
 
Hizo video ni nzuri.
Nakumbuka mechi moja ya Yanga na Simba pale uwanja wa taifa.
Ilikuwa inaoneshwa mubashara na DSTV
Yanga iliongoza bao moja.
Dakika za majeruhi Mgosi akasawazisha, refa akakataa goli.
DSTV wakarudia haraka na kuonesha kuwa mpira ulivuka mstari na kuingia golini.
Refa akaoneshwa harakaraka, akalikubali goli.
Bila DSTV, Simba tulisha lala,
Najua baadhi yenu mnakumbuka siku ile.
Video ni muhimu kuna marefa wanazingua kwa makusudi au kwa kuto kuona vema.
 
mpira wa miguu ni mchezo wenye amsha amsha na unapendeza kuwa ivo so hio tekn inhrb mvuto wa football
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…