Nini matumizi ya Maikrofoni nyingi kwenye kutoa hotuba za viongozi?

Nini matumizi ya Maikrofoni nyingi kwenye kutoa hotuba za viongozi?

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Kazi ya microfoni ni nini? Mbona viongozi wengine huwa na microfoni nyingi sana mbele yao wakati wakitoa hotuba na wengine huwa na moja au mbili (stereo) tu?

Je, wingi wa microfoni husaidia hotuba kuelewka?

1624520399383.png

1624520624802.png

1624520770093.png

1624520840846.png
 
Kwa hiyo hapo ambapo Trump anaonekana na Microphone mbili waandishi wa habari hawaripoti hilo tukio?
Huoni kuwa hapo ni UN general assembly? Waandishi hawawezi kupeleka mic zao. Ni sawa na bungeni kwetu ambapo kuna mfumo uliotayari ambao huo ndio utafeed vyombo vingine vya habari
 
Bongo movie stars huwa na.mic karibu 50 kwenye press zao.. samia mic.moja
 
Mic huwekwa mbili kwa sababu zifuatazo
1. Moja huwa connected kama standby mic incase moja ikikata kwa sababu za kiufundi nyingine inatake over
2. Katika baadhi ya setting mic moja hupeleka signal kwenye chumba (chamber) ya wakalimani ambao hupelekewa channel tofauti kwa ajili ya kutafsiri tofauti na mic inayoenda moja kwa moja kwenye PA system
3. Mic nyingi wakati mwingine hutumika kurusha matangazo ya moja kwa moja
4. Mic zenye logo kama hizo za Kiongozi Mkuu huwa ni za vombo va habari
 
Huoni kuwa hapo ni UN general assembly? Waandishi hawawezi kupeleka mic zao. Ni sawa na bungeni kwetu ambapo kuna mfumo uliotayari ambao huo ndio utafeed vyombo vingine vya habari
Sasa kwenye viongozi wengine wakubwa hakuwezi kukawa na mfumo ambao unafeed vyombo vingine vya habari?Kwenye dunia ya sasa hivi ya sayansi na techlojia mfumo si kitu ambacho ni portable na kidogo tu kama simu?
 
Back
Top Bottom