Nini mustakabali wa shilingi yetu?

Nini mustakabali wa shilingi yetu?

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Posts
2,149
Reaction score
1,718
Katika kipindi cha kuanzia mwaka huu shilingi ya Tanzania imepitia misukosuko mikubwa. Shilingi yetu imepoteza karibu theluthi moja ya thamani yake dhidi ya fedha za kigeni kwa ulinganishi wa dollar ya marekani ambayo ndiyo haven currency kwa sasa.

Tuelewane kwamba naposema shilingi inashuka dhidi ya fedha za kigeni in particularly USD, nina maana ya kwamba bei ya kununua USD imekuwa ikipanda siku hadi siku. Mwaka jana wakati kama huu ili kununua dollar 1 ya Marekani ulihitaji kiasi cha wastani wa Tzs 1650 ila kwa sasa utahitaji kati ya Tzs 2200 kununua dollar hiyo moja ya Marekani. Na ukifanya kihesabu ongezeko hilo la bei linakupa asilimia 33.33% ambayo ndiyo theluthi moja niliyoiongelea. Ikiwa na maana shilingi yetu imepoteza asilimia 33.33 ya thamani yake ya mwanzo dhidi ya USD.

Katika makala yangu moja ya nyuma nililigusia hili na kuonesha ni sababu zipi ambazo zinasababisha shilingi yetu inazidi kupoteza thamani siku hadi siku dhidi ya fedha za kigeni USD in particular. Nilitaja sababu kadha wa kadha na kuzielezea ambazo ni:

1) Mfumuko wa bei
2) Deni kubwa la taifa ambalo sasa linavuka asilimia 30 ya pato letu la taifa na limekuwa kwa kasi kwa kipindi cha miaka 2 iliyopita.
3) Nakisi katika akaunti yetu ya biashara, ikiwa na maana Tanzania ina agiza sana bidhaa kutoka nje kuliko inavouza. Import>Export
4) Kudorora shughuli za utalii ambazo zilikuwa zinalipatia taifa fedha nyingi za kigeni. Na ikumbukwe unavokuwa na fedha nyingi za kigeni inakuwa rahisi kudhibiti thamani ya fedha yako.
5) Performance ya uchumi wa nchi na ukuaji wake.
6) Kuimarika kwa uchumi wa Marekani

Ningependa hizo sababu kwa maelezo mfanye reference kwenye chapisho langu la Forex trading maana nimezielezea hizo sababu kwa undani kidogo. Nilichotaka kufanya hapa ni kugusia kidogo hiyo point niliyo bold.

Hiyo ndiyo imekuwa madai ya serikali na sio kwa nchi yet utu kwamba kwa mwaka mmoja uliopita USD imeimarika sana dhidi ya currency nyingi za ulimwengu. Na sababu kubwa ni kuimarika kwa uchumi wa Marekani kwa ujumla wake.

Ikumbukwe kwamba katika masuala ya currency kama utafanya reference ya point namba 5 nchi inapokuwa na performance nzuri ya uchumi inamaana kwamba uchumi utakuwa unavutia capital inflow kutoka kila pembe ya dunia. Na kunapokuwa na capital inflow katika uchumi ina maana mahitaji ya currency ya nchi yatakuwa yapo juu na bei au thamani husika ya currency nayo inaenda juu dhidi ya currency nyingine za ulimwenguni.

Huku uchumi wa Marekani ukizidi kufanya vizuri kwa kuthibitishwa na data za hivi karibuni za ajira. Wadadisi wengi na wataalamu wa masuala ya ki uchumi wamedokeza kwamba mnamo mwezi December Banki kuu ya Marekani (Fed) wataangalia na kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza Interest rate.

Baada ya kuzisoma habari hizi nilikuwa kwenye hali ya sintofahamu kwa sababu najiuliza kwa sasa kwamba ikiwa shilingi yetu sasa inanunua dollar 1 kwa 2200 vipi kama wamarekani wataamua kupandisha rate? Na ikumbukwe hapo kwenye bold nimeeleza kwamba ndiyo sababu kubwa ambayo inatolewa kuwa chanzo cha currency nyingi kuporomoka.

Wengi watakuwa wanajiuliza uhusiano iliopo kati ya kupanda kwa interest rate huko Marekani na kuzidi kuimarika kwa dollar ya marekani dhidi ya currency nyingine. Ipo hivi:

Pale banki kuu (Fed) wanapoamua kupandisha interest rate ina maana kwamba hii itaenda pia kuathiri taasisi nyingine za fadha hususani mabenki. Kwa hiyo napo huko interest rate ya kuanzia kwenye loans, mortgage na savings nazo zitaenda juu. Katika hali hiyo interest rate inavokuwa juu katika nchi fulani ina maanisha kwamba nchi itakuwa inavutia capital inflow kutoka pembe mbalimbali za dunia kwa sababu investors watapata return kubwa za pesa zao kama wakiwekeza mahali penye interest rate kubwa.

Sasa inapotokea capital inflow kuingia kwenye nchi ndipo hapo mahitaji ya fedha ya nchi husika yanapoongezeka na thamani yake kuongezeka pia.

Hivi ndivo itavotokea pale ambapo Fed wataamua kuongeza interest rate tutashuhudia dola ya marekani ikizidi kupanda thamani maradufu dhidi ya currency nyingine za dunia hususani shilingi yetu ya Tanzania.

Na ikumbukwe pia kwa nchi ya Tanzania ambayo madeni yake mengi yapo kwa USD inakuambia kwamba pale rate itakapokuwa juu na dola kupanda inamaana automatically deni litazidi kwenda juu sana kwa sababu ikumbukwe wenzetu huko duniani wanavokopesha interest rate inakuwa haipo fixed bali ipo flexible kutegemeana na hali ya kiuchumi ya kipindi husika. Na kwasababu rate zitakuwa zimepanda basi hata deni la taifa nalo litapaa.

Kwa maelezo hayo mafupi bado nazidi kuona kiza kinene kwenye dafu letu hili (TZS) na kwa story nnazo sikia kwamba serikali sasa haina pesa ni wazi kwamba kwa mwaka ujao dafu letu litazidi kuwa kwenye msukosuko mkubwa na sitashangaa kama dollar moja ikitrade kwa 2500 au zaidi. Kwa sababu viashiria vyote ambavyo ndio visababishi vya kushuka kwa shilingi yetu kama nilivoorodhesha hapo juu bado vipo against us.

Naona bado utalii utaendelea kudorora, deni la taifa linazidi kukua kwa kasi, mfumuko wa bei kama bado naunusa, ukuaji wetu wa uchumi bado hauridhishi japo tunasifiwa sana lakini sio ukuaji ambao naona utaongeza thamani ya dafu letu na hiyo point ya uchumi wa Marekani na shaka za kupanda kwa interest rate.

Najaribu ku foresee labda haya mafuta na gas yaliyogunduliwa labda in the future yaka attract capital inflow ambayo inaweza kuitoa sarafu yetu kimasomaso. Na pia kama tutatumia oil na gas vizuri inamaana tutaweza ku correct nakisi katika akaunti yetu ya biashara maana tutakuwa tunauza nje oil na gas na hapo hapo hatutakuwa tena tuna import oil na gas kama tunavofanya sasa. Na ni oil na gas ambayo pia inaweza kupunguza inflation katika nchi nikiwa na maana kama bei ya hivi vitu ingekuwa chini tungebakiwa na kazi moja tu ya kucontrol ile part ya inflation inayotokana na chakula.

Ila kwa gas na oil kufanya hiyo miujiza hatuna budi kuwa na policymakers wenye nia kweli ya kutenda kwa ajili ya Tanzania.

However, point yangu ya msingi ni kwamba dafu letu tukufu lipo kwenye mtihani mkubwa sana.
Inawezekana kwamba nime exaggerate sana kwenye analysis yangu hii, ningeomba pia wataalamu wengine wa uchumi wanisaidie katika hili ndo mana naamua kuileta hapa jukwaa la uchumi na biashara.

Regards Davion Delmonte Jr.

Nakala imfikie Bavaria Econometrician
 
Nimerudi.

Mustakabali wa shilingi yetu utategemea na sera za serikali mpya.

Na hatuwezi kusema tusubiri uchumi wa marekani uanguke ili shilingi yetu ipate nguvu.

Magufuli inabidi apige marufuku matumizi ya dola ndani ya nchi, ahakikishe anapiga marufuku uagizaji wa bidhaa zisizo na tija kwenye uchumi wetu.

Ajenge viwanda ili vizalishe mbadala wa vinavyoletwa humu Tanzania.

Pia aweke mazingira bora ili wananchi waweze ku-export bidhaa kwenda nje, tukianza na bidhaa za kilimo.
Davion Delmonte Jr.
 
Last edited by a moderator:
ngoja nkakusanye nguvu za kuisoma yote na ku-reason properly.
 
Nimerudi.

Mustakabali wa shilingi yetu utategemea na sera za serikali mpya.

Na hatuwezi kusema tusubiri uchumi wa marekani uanguke ili shilingi yetu ipate nguvu.

Magufuli inabidi apige marufuku matumizi ya dola ndani ya nchi, ahakikishe anapiga marufuku uagizaji wa bidhaa zisizo na tija kwenye uchumi wetu.

Ajenge viwanda ili vizalishe mbadala wa vinavyoletwa humu Tanzania.

Pia aweke mazingira bora ili wananchi waweze ku-export bidhaa kwenda nje, tukianza na bidhaa za kilimo.
Davion Delmonte Jr.
Of course kama akiyafanya hayo shilingi inaweza kupaa kwa namna moja au nyingine ila sidhani kama anaweza kuyafanya haya maamuzi kwa kipindi kifupi kijacho. Labda tuone baada ya miezi kama sita ndo tutaweza kuona kama kweli ana nia ya kuikomboa shilingi yetu.
 
Of course kama akiyafanya hayo shilingi inaweza kupaa kwa namna moja au nyingine ila sidhani kama anaweza kuyafanya haya maamuzi kwa kipindi kifupi kijacho. Labda tuone baada ya miezi kama sita ndo tutaweza kuona kama kweli ana nia ya kuikomboa shilingi yetu.

Maamuzi ya haraka anayoweza kufanya na yakaleta matunda ndani ya muda mfupi ni kupiga marufuku uagizaji wa bidhaa zisizo na ubora, bidhaa ambazo zinaweza kuzalishwa nchini na bidhaa ambazo hata zisipokuwepo nchini hazitaleta athari yeyote.
 
[Kuzuwia bidhaa za kipuuzi kuingia Tanzania Mh. JPM anaweza kuzuwia kwa kutamka tu. Ila ninajiuliza je ni wajibu wa rais ( serikali) kuzalisha bidhaa za kuuza nje?, je ni jukumu la serikali kuanzisha viwanda( nilidhani ni kujenga mazingira rafiki). Kwa nini tunataka kubaki walalamikaji? Rais azuwie ujinga wa kununua matunda( apples) Afrika Kusini tunaacha za kwetu zinaoza Lushoto na Makete?
 
Back
Top Bottom