Wachangiaji,
Nawashukuru kwa mchango wenu, ni kweli kuna vyuo vingi vina ruhusu mwenye ADV DIPLOMA kusoma Master Degree, lakini kuna vyuo hawaruhusu vile vile kama vyuo vya Medicine IMTU, Muhimbili nk, Mfano holder wa Advance Diploma ya Clinical medicine (AMO) haruhusiwi kabisa kusomea master yeyote ya medicine bali atatakiwa asome Bachelar degree, wakati huo huo vyuo kama KCMC, na vyenginevyo hata ulaya vinawaruhusu AMO kuchukua Master kama za Public Health, epidemiology nk.
Hapa sasa ndipo panaponichanganya zaidi hivi ni utaratibu gani hasa unaotumika juu ya masuala kama haya ni utashi wa mtu , chuo au kuna sheria zinazoongoza utaratibu huu?? Naomba kusaidiwa na hili!