Nini nafasi ya Advanced Diploma East Africa?

Nini nafasi ya Advanced Diploma East Africa?

Hata mie najua ukisoma advanced diploma bongo, lazma usome post graduate diploma ndo usome masters.

Sio vyuo vyote kwamba ukiwa na adv diploma lazima uanze kusoma post. Mzumbe ni mfano mzuri tu
 
Wachangiaji,

Nawashukuru kwa mchango wenu, ni kweli kuna vyuo vingi vina ruhusu mwenye ADV DIPLOMA kusoma Master Degree, lakini kuna vyuo hawaruhusu vile vile kama vyuo vya Medicine IMTU, Muhimbili nk, Mfano holder wa Advance Diploma ya Clinical medicine (AMO) haruhusiwi kabisa kusomea master yeyote ya medicine bali atatakiwa asome Bachelar degree, wakati huo huo vyuo kama KCMC, na vyenginevyo hata ulaya vinawaruhusu AMO kuchukua Master kama za Public Health, epidemiology nk.

Hapa sasa ndipo panaponichanganya zaidi hivi ni utaratibu gani hasa unaotumika juu ya masuala kama haya ni utashi wa mtu , chuo au kuna sheria zinazoongoza utaratibu huu?? Naomba kusaidiwa na hili!
 
Kila nchi ina utaratibu wake...lakini Chuo kinaruhusiwa kuwa na utaratibu wake so far hauko tofauti na Mamlaka husika inayosimamia na kudhibiti Elimu ya Juu.

Nakumbuka kuna wakati huko nyuma rafiki yangu mwenye advance Diploma kwenye mambo ya afya, alikuwa anatafuta Masters degree nje ya nchi na hakufanikiwa, Advance Diploma yake ilikuwa haitambuliwi kabisa kwenye system zao na wote walikuwa wanamshauri asome first degree kwanza..walishindwa ku'harmonise' curriculum ya advance diploma na za kwao za undergraduate degree!

Postgraduate Diploma ilikuwa ni kwa wale ambao walipata C (pass) ktk undergradute degree na ili ukubaliwe Kufanya Masters unaanzia na PGDip, ukifaulu unamalizia Masters! Vyuo vingine katika nchi hizohizo hazitoi kabisa PGdipl, wao wanataka uwe na B or above kwenye first degree ndio wakukubali kwenye Program za Masters.

Vilevile Elimu imekuwa Biashara, na hii imepelekea vyuo vingi kutaka ku-enroll wanafunzi wengi kwa kushusha entrance minimum requirements.....
 
Wazo mbadala: hivi ni kweli mfano mwenye Bcom(accounting) anauelewa mkubwa kuliko mwenye Adv Diploma in Accounting? au tatizo ni matumizi ya neno degree....tukichukuwa takwim pale NBAA wanaofaulu sana ni wenye Bcom na ADA hawafanyi vizuri....? makazini je performance ya hawa watu ikoje....? let us think deeply!!!
 
Back
Top Bottom