hivi nani alikuja na hiyo idea ya advanced diploma,maana ukingalia vizuri mfano Bcom ya UD na ADA(IFM) or ADCA ya mzumbe(hope hazipo sasa) hazina tofauti yeyote,kwenye Accounting board wote hao ni level moja na wanaanza level moja,hata exemption katika ACCA wote ni sawa...nimeona States wengi wenye advanced diploma wanaingia graduate schools bila matatizo yeyote,tatizo liko pale UD maana nasikia advanced diploma haiwezi kukuingiza MBA,why? kama UCLA mtu wa advanced diploma anaingia MBA iweje UD wanamkataa? sielewi kabisa.
Tusitiane moyo wadau. Degree na Advanced Diploma haziko sawa katika anga za kimataifa. Tutabishana mpaka jioni, najua hilo as kuna watu wengi wenye Advanced Diploma hawatapenda kukubaliana nami. Kuna vyuo kibao duniani, ukienda kuomba kusoma Masters unaambiwa lazima ukasome Post Graduate Diploma. Meaning, Post Graduate Diploma ndio sawa na degree katika soko la kimataifa. Ila katika anga zetu za kibongo bongo, tunaona some colleges like IFM wanataka kuzipandisha chati swala ambalo kwangu mimi naona ni kuwapotosha wanafunzi.
Yes, kwenye professional exams za NBAA wanakubali Advanced Diploma in Accounting (only) manake focus yao ni kwenye few subjects (e.g. Business Law, QM, Financial Accounting, Introduction to Management Accounting n.k.) ambazo lazima uwe umezicover, and not issue ya certificate only na ndio maana wanachukua Course Outlines toka katika vyuo vya Biashara before hawajatoa exemptions. That's why ukienda na degree yako ya B.Com but major haikuwa accounting (may be ilikuwa Finance au Banking), usitegemee kupata exemption. Na ukichunguza historia, utagundua kuwa, vyuo vingi vilijitahidi kuweka required subjects za kukupa exemptions mapema ili kuwawezesha wanafunzi kuanzia level ya juu kiasi katika mitihani ya NBAA. Hata hivyo, kuna vyuo viliwahi kutishiwa kunyimwa exemption kutokana na performance ya wanafunzi wao kwenye mitihani ya bodi (kimoja kiko Dar City Centre). Pass rate ya wanafunzi toka katika hivyo vyuo kwenye mitihani ya CPA ilikuwa mbaya sana and NBAA wakatishia kufutilia mbali exemptions kwenye hivyo vyuo.
Ukienda kwenye soko la masomo ya biashara East Africa, I tell you, njoo na ADA yako halafu mtu mwingine aje na B.Com (Accounting) uone kama utakuwa at the same level kwenye ushindani. Nimekuwa involved kwenye interview panels nyingi East Africa, and nimekutana na wakenya wengi wakiponda Advanced Diplomas, na kuziheshimu degrees tena from some Universities not all in Tanzania / East Africa. Hii ni kutokana na idadi and perception ya degrees nchini Kenya na we should expect ziongezeke katika nchi kama Uganda. Naliongea hili from practical view and not story as nimeshaparticipate kwenye kuscreen watu and nimeona views za waganda, wakenya, wazimbabwe na pia waingereza.
Kwa ushauri wangu as nimekuwa kwenye hizo panels especially za wahasibu, ningependa kuwashauri ndugu zangu wenye Advanced Diplomas in Accounting, wahakikishe wanasoma CPA and ikiwezekana Post Graduate na Masters mapema before EAC haijatake-off kisawa sawa. Huu ni ushauri wa bure, and tusipende kujipa moyo, let's go by facts wadau otherwise tutakuja kukutana na maombi kibao ya kazi humu ndani.