Nini Nitampa Mbwa?

Ndahani

Platinum Member
Joined
Jun 3, 2008
Posts
18,160
Reaction score
9,151
Mimi mbwa nimefuga, ili nyumba ailinde,
Kwa jirani nimeiga, anaye kama kipande,
Wabaya akiwaniga, na kuwafanya wakonde,
Nini nitampa mbwa, ailinde nyumba yangu.

Cha ajabu huyu wangu, kutwa kucha amelala,
Jua au liwe wingu, njaa hata na chakula,
Kung’ang’ania uvungu, na kuleta masihala,
Nini nitampa mbwa, ailinde nyumba yangu?

Wamkimbia mwenzangu, na kujaa vamia kwangu,
Wamejua shida yangu, mbwa ashinda uvungu,
Wataka nitia pingu, wachukue mali zangu,
Nini nitampa mbwa, ailinde nyumba yangu?

Mbwa nimempa yote, lakini kaniangusha,
Sasa sijui lolote, kweli kanipagawisha,
Natamani ajikate,, thamani yake kashusha,
Nini nitampa mbwa, ailinde nyumba yangu?

Kapoteza yangu ndoto, ameniacha gizani,
Angelikuwa mtoto, ningemuuza dukani,
Kaniongeza msoto, na kuninyima amani,
Nini nitampa mbwa, ailinde nyumba yangu?

Wajuzi wale mahiri, mnijulishe jamani,
Mwaweza ijua siri, kunitoa matatani,
Ili niitafakari, na kujipa tumaini,
Nini nitampa mbwa, ailinde nyumba yangu?
 
mbwa ataka upendo, siyo nyama na ugali,
umpatie uhondo, tena usikae mbali,
mwonyeshe vyote vionjo, tena kwa kila hali,
uvungu takuwa uvundo, na yeye atakujali!
...au labda...
mbwa wako ana mimba,pengine ana minyoo,
mpeleke kwa mkunga, au mpatie dawa!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…