Nini Sababu Wasio Wakristo Kujaza Kwenye Ibada za Kilokole?

Nini Sababu Wasio Wakristo Kujaza Kwenye Ibada za Kilokole?

2) Wengine huenda kama wanavyo kwenda kwa mganga wa kienyeji kutafuta suluhisho la matatizo yao (baadala ya kuiitikia TAWIRE kwa mganga wao kiitikio BWANA YESU ATUKUZWE) wakitoka hapo Imani ya kidini hakuna Wala hawajui Masiha alibatizwa wapi na nani au hata kujisomea Biblia.

Katika Ukristo suluhu ya changamoto zako huzipati pasi na kuwa na IMANI katika KRISTO Yesu.

Wanawezaje kupokea UPONYAJI pasi na Imani?
 
Wapo wanaofanya na maigizo, wapo walioponywa kweli, wanafuata tumaini na faraja. usipovipata kanisani huvipati kwingine
 
Nimekuwa nikitazama sana vipindi vya kimahubili luningani hasa vya wale wachungaji wakubwa mno kama Vile Much Mwamposa wa Arise&Shine TV, Kuhani Mussa Richard wa JehovaJireTV nakadhalika.

Katika nyakati za kutoa ushuhuda wa Yale waliyotendewa na Mungu, iwe uponyaji au kufunguliwa kutoka katika monyororo ya shetani, pamekuwa na watoa ushuhuda wengine wenye majina yasio fanana na ya kikristo kwa Mfano, Ashura, Jummane, Fadhili, Abdul, Huseni na mengineo yenye kunasibu dini nyingine.

Nini Sababu ya ongezeko la wasio wakristo katika madhabahu za bwane Yesu.?

Je inawezekana kuwa nyakati zinakaribia na kwamba Kristu analikusanya KANISA lake?

Au ni kwasababu ukweli inaanza kutamalaki machoni pa walio si wakristo?

Karibuni.
Wanamfuata Yesu mwenye suluhisho la matatizo yao.
 
Inawezekana.

Lakini kwenye kulipwa hapo ninapinga kidogo.

Mtu kama Mwamposa ameanza huduma tngu kitambo sana. Tusema tuanze kuhesabu watu walio kuwa wanatoa USHUHUDA tangu anaanza huduma.

Kwa mwaka Kuna juma pili 52. Kila Juma pili watu 10 hutoa USHUHUDA kanisani

Hivyo 52 X 10 = 520 watoa USHUHUDA kwa kulipwa (kwa mwaka)

Mwamposa huduma yake ilianza kushamiri mwaka 2010. Hivyo ni miaka 14 mpaka Leo hii.

Watu 520 X 14 = 7,280 watoa USHUHUDA kwa kulipwa.


Jumla ni watoa USHUHUDA 7,280 wa kulipwa.

SWALI:-
Umeshawahi kutana na mtoa USHUHUDA wa kulipwa hata mmoja (1) kati ya hao 7,280 ambaye akakuthibitishia kuwa alilipwa na Mwamposa?
Kwa pesa za watu wenye uono mdogo anazozikusanya wala hashindwi kuwalipa mashuhuda wa uongo.
Kumbuka hiyo ndio kazi yake inayompatia ugali kwa hiyo hashindwi kufanya ubunifu wa kila siku ili kuwapumbaza watu wanaoamini haraka kama wewe.
Labda na wewe nikuulize swali katika hao mashuhuda uliowaona kuna ambao unawafahamu angalau jirani yako mmoja na unamjua kweli ni muislamu?maana kuropoka jina tu kila mtu anaweza labda ingekuwa baada ya kutaja jina kila mmoja anakuja kuonesha kitambulisho chake cha Nida watu wathibitishe jina hapo wangeogopa.
Sasa ngoja nikuelekeze jinsi ya kufanya research kujua kama mtu ni muongo au mkweli siku moja fanya hivi;
Nasikia pia huwa wanatibu vilema na wagonjwa mbalimbali sasa siku ili uwakamate uongo wao tafuta kiwete mmoja ambaye unamfahamu may be ni jirani yako or whatever kisha nenda naye halafu ukifika muda wa kuombewa nenda naye mbele ili asaidiwe kwa maombi ili apone kama wanavyopona wale wengine wanaowaoneshaga,kitakachotokea baadae uje kutusimulia.😄😄😄😄😄
 
Back
Top Bottom