Nini Sababu Wasio Wakristo Kujaza Kwenye Ibada za Kilokole?


Katika Ukristo suluhu ya changamoto zako huzipati pasi na kuwa na IMANI katika KRISTO Yesu.

Wanawezaje kupokea UPONYAJI pasi na Imani?
 
Wapo wanaofanya na maigizo, wapo walioponywa kweli, wanafuata tumaini na faraja. usipovipata kanisani huvipati kwingine
 
Wanamfuata Yesu mwenye suluhisho la matatizo yao.
 
Kwa pesa za watu wenye uono mdogo anazozikusanya wala hashindwi kuwalipa mashuhuda wa uongo.
Kumbuka hiyo ndio kazi yake inayompatia ugali kwa hiyo hashindwi kufanya ubunifu wa kila siku ili kuwapumbaza watu wanaoamini haraka kama wewe.
Labda na wewe nikuulize swali katika hao mashuhuda uliowaona kuna ambao unawafahamu angalau jirani yako mmoja na unamjua kweli ni muislamu?maana kuropoka jina tu kila mtu anaweza labda ingekuwa baada ya kutaja jina kila mmoja anakuja kuonesha kitambulisho chake cha Nida watu wathibitishe jina hapo wangeogopa.
Sasa ngoja nikuelekeze jinsi ya kufanya research kujua kama mtu ni muongo au mkweli siku moja fanya hivi;
Nasikia pia huwa wanatibu vilema na wagonjwa mbalimbali sasa siku ili uwakamate uongo wao tafuta kiwete mmoja ambaye unamfahamu may be ni jirani yako or whatever kisha nenda naye halafu ukifika muda wa kuombewa nenda naye mbele ili asaidiwe kwa maombi ili apone kama wanavyopona wale wengine wanaowaoneshaga,kitakachotokea baadae uje kutusimulia.πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…