Nini sababu ya kujirudia rudia kwa U.T.I.?

Nini sababu ya kujirudia rudia kwa U.T.I.?

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
3,607
Reaction score
9,430
Habari wana JF, hususani wana jukwaa hili,, nimekua nikipata mafundisho na ushauri mbali mbali kuhusu afya kwa ujumla! Pongezi kwenu!

Ndugu wanajukwaa, kuna tatizo limenileta hapa naombeni msaada wenu wa kitaalamu !

Ni hivi, nina rafiki yangu (ke) ambae anasumbuliwa sana na U.T.I kila akiumwa akienda hosp anapewa dawa au kuchomwa sindano baada ya muda flan (miezi miwili au mitatu) tatizo linajirudia tena, akienda kupima anakutwa nao !!!

Msaada!
1. Naomba kueleweshwa kuhusu huu ugonjwa
2. Je huu ugonjwa ni moja ya STD'S ?
3. Huu ugonjwa unasababishwa na nini haswa ?
4. Huu ugonjwa unaweza kuepukwa kwa njia zipi? (kwa mtu ambae hajaupata)
5. Nini madhara makubwa ya huu ugonjwa ?

Mwisho kabisa naomba kuelekezwa ni hospitali gani ama nimshauri nini huyu rafiki yangu ili aweze kupona tatizo linalomsumbua!!?? tatzo hili yupo nalo kama mwaka na miez kadhaa imepita !

Hajawahi kwenda kwa mganga wa kienyeji wala kutumia miti shamba !!
 
!!

1. Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wabaya kwenye mrija wa urine.
2. Unaweza kuwa STD lakini chances ni ndogo sana. Mara nyingi sio wa kuambukizwa.
3. Unasababishwa na ongezeko la bakteria kwenye kibofu na mrija wa kupitisha urine.
4. Unashambulia sana wanawake kwa sababu ya maumbile. Kwa wanawake hakikisha unasafisha na maji na sabuni kila unapo urinate, vaa nguo za ndani safi, epuka public toilets, hakikisha ni mkavu muda wote, usivae nguo za ndani za mitumba au nguo za kubana sana hasa mbele, jisafishe mbele kwenda nyuma, na usipulizie manukato sehemu za siri.
5. Unaweza kusababisha utasa, kuoza, vvu na hata upofu.

Natumaini nimekusaidia.
 
nashukuru sana Mkuu kwa majibu mazuri , hakika nimesaidika sana!!! je nimshauri aende hosp gani ? yan mpaka ameanza kukata tamaa
 
Ni ugonjwa wa njia ya mkojo sababu inaweza kuwa bakteria au mimba mfano wa wadudu hawa bakteria ni escherichia coli
 
Kipindi cha mimba kunakuwa na uzarishaji wa kutosha wa hormone ya progesterone ambayo hupunguza usafirishaji wa mkojo
 
dalili zake:maumivu wakati wa kukoja,kuchomachoma mkojo,maumivu ya tumbo chini ya kitovu au kwenye pembe ambapo figo
 
zinapatikana matibabu:dawa zinazosafisha njia ya mkojo mfano nitrofuratoin 100mg tds kipindi unafanya uchunguzi juu ya
 
aina gani ya bakteria amesababisha na dawa ambayo itafaa kuwa (culture sensitivity) kama uti itarudia mara kwa mara
 
TUMIA CAP AMOXYLINE 5OOmg tds 5/7vile vile mpe tab pcm 1g tds 3/7 kama ana homa na msisitize kunywa maji mara kwa mara
 
(HYDROTHERAPY) hii husaidia kusafisha njia ya mkojo kwa kukojoa na kupunguza kuchomachoma(burning sensation)
 
Ushauri mzuri sana,
Nyongeza MSHAURI AWE ANAKUNYWA MAJI KWA WINGI yanasaidia kusafisha bacteria waliojishikisha kwenye njia ya mkojo.
Najua wanawake wengi ni wavivu sana kunywa maji.
 
Habari wana JF, hususani wana jukwaa hili,, nimekua nikipata mafundisho na ushauri mbali mbali kuhusu afya kwa ujumla! Pongezi kwenu!

Ndugu wanajukwaa, kuna tatizo limenileta hapa naombeni msaada wenu wa kitaalamu !

Ni hivi, nina rafiki yangu (ke) ambae anasumbuliwa sana na U.T.I kila akiumwa akienda hosp anapewa dawa au kuchomwa sindano baada ya muda flan (miezi miwili au mitatu) tatizo linajirudia tena, akienda kupima anakutwa nao !!!

Msaada!
1. Naomba kueleweshwa kuhusu huu ugonjwa
2. Je huu ugonjwa ni moja ya STD'S ?
3. Huu ugonjwa unasababishwa na nini haswa ?
4. Huu ugonjwa unaweza kuepukwa kwa njia zipi? (kwa mtu ambae hajaupata)
5. Nini madhara makubwa ya huu ugonjwa ?

Mwisho kabisa naomba kuelekezwa ni hospitali gani ama nimshauri nini huyu rafiki yangu ili aweze kupona tatizo linalomsumbua!!?? tatzo hili yupo nalo kama mwaka na miez kadhaa imepita !

Hajawahi kwenda kwa mganga wa kienyeji wala kutumia miti shamba !!

urinary track infection.......inahusisha viungo vyako vinavyohusika na utoaji wa maji machafu mwilini.figo ,milija kibofu ,na njia ya mkojo
kwa experience yangu huu ugonjwa ni rahisi Zaidi kuambukizwa kwa kina dada
na sehemu kuu ya kuambukiziwa ni public toilet au family toilet
1.labda niulize swali kwa kina dada uingiapo chooni vitu vingapi unashika ? sidhani kama huwa mna kumbukumbu kuwa umeshika kitasa nje....kisafi? tena kitasa ndani ....kisafi
unashika nguo zako ....safi? unakaa kama choo cha kukaa.....kisafi? au unachuchumaa ....unakojoa mkojo kwa pressure sana ....mwingine come back to you after rebound....msafi?......unashika pressure tape kwa ajili ya kutawaza .....safi? unatawaza ...... sasa tu assume wewe ni wa kwanza kuuingia katika choo hiki ....na una U.T.I anaye fuata atakuwa salama? nope nope nope
2. cha pili kwa mwanamke kama unaingia chooni unakuta ndoo ya maji imewekwa hapo hayo maji sio salama kwako at all usitumie kabisa .....ni vyema ukatumia tissue ambazo una uhakika nazo si kila tissue na ni vema ukawa nazo
3.kujishika shika kwa bibi make sure you are clean usijishike tu kwa sababu ni mwili wako
4.chupi zako anika juani ile biashara ya kuanika chupi uvunguni imepitwa na wakati .anika chupi zikauke.unatakiwa kuwa na pea za kutosha ilikuepusha kurudia rudia mara kwa mara
5.maji ni tatizo kubwa sana .watu wengi wanao ishi maeneo yaliyo na visima kwa mfano dar es salaam wana athirika sana na tatizo la uti Zaidi ya wengine so maji ya kutawaza /kuoga yaangaliwe sana
 
Kujirudia kwa UTI ni kutokana na either dawa kutokutibu au dawa husika kiwa sugu kwako.

Ili kutibu kwa uhakika UTI daktari aoteshe mkojo, ili aweze kubaini kwa hakika dawa ya wadudu husika au ulionao.
 
nashukuru sana Mkuu kwa majibu mazuri , hakika nimesaidika sana!!! je nimshauri aende hosp gani ? yan mpaka ameanza kukata tamaa

Nenda hospital kama kairuki,au tmj au rejency wakafanye culture and sensitivity of urine,then watakupa dawa sahihi
 
Back
Top Bottom