Nini sababu ya kujirudia rudia kwa U.T.I.?

Nini sababu ya kujirudia rudia kwa U.T.I.?

Habari wana JF, hususani wana jukwaa hili,, nimekua nikipata mafundisho na ushauri mbali mbali kuhusu afya kwa ujumla! Pongezi kwenu!

Ndugu wanajukwaa, kuna tatizo limenileta hapa naombeni msaada wenu wa kitaalamu !

Ni hivi, nina rafiki yangu (ke) ambae anasumbuliwa sana na U.T.I kila akiumwa akienda hosp anapewa dawa au kuchomwa sindano baada ya muda flan (miezi miwili au mitatu) tatizo linajirudia tena, akienda kupima anakutwa nao !!!

Msaada!
1. Naomba kueleweshwa kuhusu huu ugonjwa
2. Je huu ugonjwa ni moja ya STD'S ?
3. Huu ugonjwa unasababishwa na nini haswa ?
4. Huu ugonjwa unaweza kuepukwa kwa njia zipi? (kwa mtu ambae hajaupata)
5. Nini madhara makubwa ya huu ugonjwa ?

Mwisho kabisa naomba kuelekezwa ni hospitali gani ama nimshauri nini huyu rafiki yangu ili aweze kupona tatizo linalomsumbua!!?? tatzo hili yupo nalo kama mwaka na miez kadhaa imepita !

Hajawahi kwenda kwa mganga wa kienyeji wala kutumia miti shamba !!
Mara nyingi hiyo sio UTI inayosababishwa na bacteria. Hizo ni fangasi, meza vidongo vya fluconazole siku 14, na kuepuka kuosha uchi kwa sabuni, epuka kutumia vidonge au cream zenye steroids, epuka "kufanya" kotekote matakoni na mbele kuepuka kuhamisha vijidudu vinavyosababisha UTI kutoka kwenye kinyesi kwenda ukeni.
 
Kuna dawa inaitwa FLUCAMOX. Hii ni kiboko ina flucloxacillin na Amoxyciline, akitumia hiyo na asipopona basi huyo ana matatizo mengine zaidi ya UTI
 
ni either bado anakua kwenye mazingira yaleyale(hasa vyoo na bafu) ambayo yana habour bacteria wasababishao tatzo,namna ya kujisafisha isiyofaa baada ya kujisaidia(ajisafishe toka mbele kwenda nyuma kwa maji mengi na safi),aepuke bubble bath,nguo za kubana hasa kyupi,sometimes inaweza kuwa bacteria wamekua sugu kwa dawa anazotumia so nakushauri uende kwenye centre kubwa kwa ajili ya culture na sensitivity
 
nashukuru sana Mkuu kwa majibu mazuri , hakika nimesaidika sana!!! je nimshauri aende hosp gani ? yan mpaka ameanza kukata tamaa

sina uhakika wa hospitali za Tanzania, hata hivyo akitibiwa awe mwangalifu sana na azingatie mambo namba nne-4
 
Bwana Kitalembwa;
Pole sana kwa yanayokukuta
Naona umepata michango mingi mizuri ila na mimi naona nijazilishie; Mwambie aongezee yafuatayo

  • Kunywa maji mengi mara kwa mara..kwani kukojoa mara kwa mara kuna zuia bacteria wabaya wasikae kwenye urinary track
  • Baada ya kujisaidia, nawa (tawadha kutoka mbele kwenda nyuma) kwa bacteria wengi wabaya wapo kwenye mfumo wa haja kubwa.
  • Kojoa kabla na baada ya tendo la ndoa (baada ya tendo ni muhimu zaidi)
  • Osha sehemu zako za siri kabla na baada ya tendo
  • Wale wanawake wanaofanywa kinyume na maumbile hasa kama anafanya pande zote bila mwanamme kuosha rungu kwa sabauni; hawezi kuepuka UTI
  • Usitumie diaphragm or spermicide kama njia ya kuzuia mimba kwani sehemu ambayo diaphragm inawekwa, inazuia mtu akikojoa mkojo usiishwe wote kwenye Kibofu
  • Choo cha kukaa cha public sio kuzuri...au kukojoa mkojo umrukie kwa joo cha public sio vizuri japo Tuna shauri akiingoa Chooni aflash kwanza kabla ya kukojoa
Naamini ukiunganisha huu ushauri wote utaweza kuepukana na hayo
Asante
 
urinary track infection.......inahusisha viungo vyako vinavyohusika na utoaji wa maji machafu mwilini.figo ,milija kibofu ,na njia ya mkojo
kwa experience yangu huu ugonjwa ni rahisi Zaidi kuambukizwa kwa kina dada
na sehemu kuu ya kuambukiziwa ni public toilet au family toilet
1.labda niulize swali kwa kina dada uingiapo chooni vitu vingapi unashika ? sidhani kama huwa mna kumbukumbu kuwa umeshika kitasa nje....kisafi? tena kitasa ndani ....kisafi
unashika nguo zako ....safi? unakaa kama choo cha kukaa.....kisafi? au unachuchumaa ....unakojoa mkojo kwa pressure sana ....mwingine come back to you after rebound....msafi?......unashika pressure tape kwa ajili ya kutawaza .....safi? unatawaza ...... sasa tu assume wewe ni wa kwanza kuuingia katika choo hiki ....na una U.T.I anaye fuata atakuwa salama? nope nope nope
2. cha pili kwa mwanamke kama unaingia chooni unakuta ndoo ya maji imewekwa hapo hayo maji sio salama kwako at all usitumie kabisa .....ni vyema ukatumia tissue ambazo una uhakika nazo si kila tissue na ni vema ukawa nazo
3.kujishika shika kwa bibi make sure you are clean usijishike tu kwa sababu ni mwili wako
4.chupi zako anika juani ile biashara ya kuanika chupi uvunguni imepitwa na wakati .anika chupi zikauke.unatakiwa kuwa na pea za kutosha ilikuepusha kurudia rudia mara kwa mara
5.maji ni tatizo kubwa sana .watu wengi wanao ishi maeneo yaliyo na visima kwa mfano dar es salaam wana athirika sana na tatizo la uti Zaidi ya wengine so maji ya kutawaza /kuoga yaangaliwe sana

amen Mkuu! asante Maelezo mazuri ya kina !!!!
 
napenda kutoa shukrani kwa wanajukwaa wote mliomipa ushauri na maelezo ya kina kuhusu huu ugonjwa!!! ni jambo la faraja sana kwa kweli, nitamshauri rafiki yangu kama mlivyonielekeza pia naahidi kuleta mrejesho
 
Ushauri mzuri sana,
Nyongeza MSHAURI AWE ANAKUNYWA MAJI KWA WINGI yanasaidia kusafisha bacteria waliojishikisha kwenye njia ya mkojo.
Najua wanawake wengi ni wavivu sana kunywa maji.

Pombe je haisaidii?
 
Bwana Kitalembwa;
Pole sana kwa yanayokukuta
Naona umepata michango mingi mizuri ila na mimi naona nijazilishie; Mwambie aongezee yafuatayo

  • Kunywa maji mengi mara kwa mara..kwani kukojoa mara kwa mara kuna zuia bacteria wabaya wasikae kwenye urinary track
  • Baada ya kujisaidia, nawa (tawadha kutoka mbele kwenda nyuma) kwa bacteria wengi wabaya wapo kwenye mfumo wa haja kubwa.
  • Kojoa kabla na baada ya tendo la ndoa (baada ya tendo ni muhimu zaidi)
  • Osha sehemu zako za siri kabla na baada ya tendo
  • Wale wanawake wanaofanywa kinyume na maumbile hasa kama anafanya pande zote bila mwanamme kuosha rungu kwa sabauni; hawezi kuepuka UTI
  • Usitumie diaphragm or spermicide kama njia ya kuzuia mimba kwani sehemu ambayo diaphragm inawekwa, inazuia mtu akikojoa mkojo usiishwe wote kwenye Kibofu
  • Choo cha kukaa cha public sio kuzuri...au kukojoa mkojo umrukie kwa joo cha public sio vizuri japo Tuna shauri akiingoa Chooni aflash kwanza kabla ya kukojoa
Naamini ukiunganisha huu ushauri wote utaweza kuepukana na hayo
Asante

nashukuru Mkuu kwa Maelezo na ushauri mzuri
 
Wewe acha kumsingizia rafiki yako! Utakuwa mchafu wewe...
 
Back
Top Bottom