Nini sababu ya kuongezeka kwa kundi hili atheist?

Nini sababu ya kuongezeka kwa kundi hili atheist?

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,325
Reaction score
7,807
Miaka ya hivi karibuni kuanzia 2018 hapa jukwaani Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu ambao hawaamini uwepo wa Mungu (atheist) hii inaashiria Nini ?

Hii hali nimeona ni tofauti na jamiiforum Ile ya 2016 kurudi nyuma

Napenda kujua elimu zao au hali zao za uchumi hawa atheist
 
Binadamu anapitia mabadiliko kwa mfumo wa grafu.Anaanza chini kwenda juu halafu atarudi kulekule.Wa kileo wanasema anajitafuta kwa kila hali na kusingizia mabaya wenzake bila kutaka kutimiza wajibu wake ipasavyo.
 
Kwasababu tunaomuamini Mungu yupo, tumeshindwa kudhibitisha..!
Wenzako wanapewa keki ya upako, maji ya upako, mafuta ya upako ili hivo vitu vikamalize matatizo yao, ushindwe kutatua mambo yako utegemee maji ya kilimanjaro halafu unajiona unaakili
 
  • Wameelimika/elimu imewatoa matongotongo​
  • Changamoto ya ukosefu wa ajira, na kufanya sehemu ya dini kuwa ajira​
  • Ubahili au kutokuwa na hela/kipato kwa ajili ya kutoa michango, sadaka n.k​
 
Miaka ya hivi karibuni kuanzia 2018 hapa jukwaani Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu ambao hawaamini uwepo wa Mungu (atheist) hii inaashiria Nini ?

Hii hali nimeona ni tofauti na jamiiforum Ile ya 2016 kurudi nyuma

Napenda kujua elimu zao au hali zao za uchumi hawa atheist
Katika nchi nyingi sana za Magharibi ambako Ukristo ulipoanzia, hamasa ya kushika dini imeshuka Sana miongoni mwa watu, sehemu zingine Hadi makanisa yamegeuzwa kuwa kumbi za starehe. Sababu kubwa ikiwa ni maendeleo makubwa katika sayansi na teknolojia. Sababu wanazotoa ni Kwamba:-
1. Existence of God cannot be proved scientifically.
2. They have each and every thing in their lives, so they should go to Church to pray for what??
3. Science and technology can solve all their problems.
 
Miaka ya hivi karibuni kuanzia 2018 hapa jukwaani Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu ambao hawaamini uwepo wa Mungu (atheist) hii inaashiria Nini ?

Hii hali nimeona ni tofauti na jamiiforum Ile ya 2016 kurudi nyuma

Napenda kujua elimu zao au hali zao za uchumi hawa atheist
Ukijua Elimu zao au Hali zao za Kiuchumi ndiyo utagundua nini labda? Hatuwataki akina Kiboko ya Wachawi, Mwamposa, Mwacha, Kapola, Mwakibinga na Wapumbavu wengine kadhaa ambao kwa Hasira na Uchungu wanaowafanyia Watanzania nimeshau hadi na Majina yao.
 
Napenda kujua elimu zao au hali zao za uchumi hawa atheist
Ukijua elimu zao au hali zao za uchumi ndio utakua umepata jibu la swali lako?

GSM na Mo ni matajiri ila wana dini zao wanazoziamini,pia wapo matajiri wengine ambao hawana dini pia,

Wapo watu masikini wana dini zao na wapo masikini wengine hawaamini uwepo wa Mungu,

So,hakuna uhusiano wa swali lako na kutaka kujua hali za hao etheist,Dini ni imani na matendo.
 
Hawa watu mtani wameleta utapeli wa dini mchana kweupe sijui tunavowasanua hawaelewi
Sasa wataelewa na kutuelewa. Yaani GENTAMYCINE nishikilie Bango Jambo na Nisagie Kunguni halafu lisije Kufanikiwa?
 
Bila shaka wewe ni muumini wa nabii masanja, au kuhani mussa au mtume mwamposa, hua mnajiita mmeokaka si ndio mkuu?
Achana na hao kina mwamposa nawengine kwamba kila mtu ni mfuasi wa manabii wa uongo?

Nataka nijue elimu zenu nyie atheist mbona sisi tunao maaskofu wenye degree na PhD nyingi lakini bado wanafanya kazi ya Mungu
 
Mtani wangu Arovera malizana nae Kibingwa tafadhali kwani naona kuna anachokitafuta kwa Watu tusiopenda Upuuzi.
 
Miaka ya hivi karibuni kuanzia 2018 hapa jukwaani Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu ambao hawaamini uwepo wa Mungu (atheist) hii inaashiria Nini ?

Hii hali nimeona ni tofauti na jamiiforum Ile ya 2016 kurudi nyuma

Napenda kujua elimu zao au hali zao za uchumi hawa atheist
Uwezi ukapinga kitu ambacho hakipo! Sasa unapinga nini? Hakijawahi kuwepo maana yake na kwenye fikra/akili hakipo! Kwahiyo ukisema "hakuna Mungu" maana yake "Mungu yupo". Ni bangi tu zinawasumbua!
 
Mungu wa kwenye biblia na quran hayupo, amepewa sifa ambazo hastahili yaani amepambwa sana mpaka kuleta contradiction.

itahitaji mtu mpumbavu wa kiwango cha juu sana kuamini katika hizo tales.

mimi binafsi naamini katika nature, natural flow of things ambapo kila unachokifanya kina matokeo yake either good or bad
 
Mahubiri ya vitisho pia sio poa. Mtu anenda kwenye ibada akitegemea apate mafundisho ya kuupoza na kuuponya moyo wake lakini badala yake ni mwendo motoooooo mooootoooooo mooootoooooo siku ya kiama moootooooo mooootooooo.........so what!?

Hakuna majibu sahihi ya maswali hasa katika hatua ya ujana yanayohusiana na namna gani ya kujikwamua katika mustakabali wa maendeleo kwa ujumla wake, badala yake ni mwendo wa kuhamasisha utoaji sadaka na zaka zaidi pasipo kuongozwa namna gani ya kupata kipato.
 
Miaka ya hivi karibuni kuanzia 2018 hapa jukwaani Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu ambao hawaamini uwepo wa Mungu (atheist) hii inaashiria Nini ?

Hii hali nimeona ni tofauti na jamiiforum Ile ya 2016 kurudi nyuma

Napenda kujua elimu zao au hali zao za uchumi hawa atheist
Ni kweli kabisa atheism imeongezeka kwa kasi kubwa sana kulinganisha miaka 10 iliyopita. Sababu ni watu kupata access ya internet na kujifunza mambo mengi humo. Pia ni sababu ya watumishi wa Mungu kufanya dini kuonekana kama biashara za watu.
 
Back
Top Bottom