Nini sababu ya ukosefu/upungufu wa dola za Marekani nchini?

Nini sababu ya ukosefu/upungufu wa dola za Marekani nchini?

Burkinabe

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2023
Posts
2,800
Reaction score
4,930
Asalaam Aleykum wapenzi wana JF.

Ama baada ya salamu hizo, niingie kwenye mada moja kwa moja.

Kwa wiki nzima nimekuwa nahaha kupata walau dola za Marekani 200 ili nifanye kununua vifaa fulani kwa njia ya mtandao, bila mafanikio!.

Kila benki au bureau de change ninayoenda, naambiwa haina dola labda nirudi baadaye!

Je, shida ni nini?

Ni kweli dola hakuna au benki na bureau de change zetu zimeamua kuzificha?!

Au mahitaji ya dola yamekuwa makubwa sana kwa watu hasa wafanyabiashara kuliko upatikanaji wake?

Au kuna watu wameamua kuzificha kwa lengo la kuja kuziuza baadaye kwa bei ya juu?!

Au, kama nchi tumefilisika na hatuna tena fedha za kigeni ikiwemo USD?

Karibuni kwa majibu.
 
Bank yako ukitaka kununua mtandaoni wanakuzuia? Unanunuaje kitu mtandaoni kwa cash?
Hapa na mm nimeshangaa,
Wakati unaweza nunua kitu kwa mastercard tu easy bila kujua hata rate ipoje, yeye ananunua kitu mtandaon anaenda kubadili hela bank 😂😂😂😂😂😂
 
Asalaam Aleykum wapenzi wana jf.
Ama baada ya salamu hizo, niingie kwenye mada moja kwa moja.

Kwa wiki nzima nimekuwa nahaha kupata walau dola za Marekani 200 ili nifanye kununua vifaa fulani kwa njia ya mtandao, bila mafanikio!...
Mauzo ya nje yameporomoka mkuu, hatuna chakuuza nje tena, tunauza SIASA na bado.
 
Hapa na mm nimeshangaa,
Wakati unaweza nunua kitu kwa mastercard tu easy bila kujua hata rate ipoje, yeye ananunua kitu mtandaon anaenda kubadili hela bank 😂😂😂😂😂😂
sina Mastercard Mkuu
 
Sijaelewa kitu kimoja mleta mada yaani kufanya purchase online na cash unazohitaji vina uhusiano gani?
Account yangu haiwezi kufanya online purchase Mkuu.
Itabidi nifanye taratibu za kuibadilisha..
Lakini ujumbe wa muhimu hapa ilikuwa ni kusema hakuna au kuna upungufu mkubwa sana wa USD nchini
 
Kama kuna mtu anaweza kunisaidia bank ambayo naweza kupata hizo usd 200 kwa kesho anisaidie
 
Back
Top Bottom