Nini sababu ya wasafiri wa vijijini kukaa kila mtu na kituo chake?!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Moja ya ushahidi wa baadhi ya wanakijiji kutotumia akili ni suala la wao kuchagua apandie wapi gari. Sio kukusanyika kwenye kituo kimoja cha karibu.

Unakuta kituo kinafahamika lakini yeye anakaa mita 200 ya kituo anataka gari limfuate. Hata mwingine atakaa mbele kidogo ya mwenzie. Nimeshuhudia sana hili kanda ya ziwa.

Au abiria kurundikana karibu ya mlango kama vile akitaka kushuka gari haitasubiri ashuke.

Je, watu hawa hawana common sense mpaka washindwe kuona sababu ya uwepo kituo cha gari?
 
Wenye magari huwafuata au hawawafuati? Hapo ni nani asiyetumia akili?
 
We
Wewe ni utingo?
 
Walimu wanchi hii wanakazi ila makonda wanaangaliwe maana wengi wamedata
 
Si ungesema tu wasukuma ni washamba mzee mbona kama unazunguka sana [emoji22]
 
Unaonekana wewe sio mkazi wa kanda ya ziwa.

Common sense ya huko kwenu sio lazima iwe common sense ya kila sehemu.

Jifunze kushauri bila kukejeli, itakusaidia kujenga mahusiano mazuri na jamii nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…