Nini sababu za wasanii wa kike kushindwa kuhimili na kufanya vizuri kwenye Bongo Flava?

Nini sababu za wasanii wa kike kushindwa kuhimili na kufanya vizuri kwenye Bongo Flava?

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
4,854
Reaction score
1,129
Mara nyingi huwa najiuliza sababu ya wasanii wa kike kushindwa kufanya vizuri katika muziki wa hapa nyumbani almaarufu kama Bongo Flava. Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakiibuka na kupotea, ni nadra kuona msanii wa kike alifanya vizuri kwa miaka achilia mbali Lady Jay Dee. Wasanii wengi wa kike huishia kutoa nyimbo mbili au 3 zinazobamba na baada ya hapo kimya hutawala.

Alipoibuka Keisha nilifikiri ataenda kututoa kimasomaso ila hali haikuwa hivyo, vivyo hivyo kwa Baby Madaha, Baby J, Linah, Stata T na hata Farida!!

Sababu ya wao kutogangamala kwenye game ni nini!? Je ni uvivu ama kukosa kujiamini?

Mimi bado naamini wasanii wa kike wana fursa ya kufanya vizuri zaidi katika huu muziki!!
Natamani sana kuwaona akina Leona Lewis, Avril lavigne, Monica na Kelly Hilson wa hapa kwetu.
 
Ni kukosa umakini tu na kile wanachokifanya,pia kujitambua ni nini wanatakiw kufanya katika maisha yao,wengi wanakurupuka

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom