Nini Simba ifanye kuvuka group stage ya CAF CL

Tulia tuwatafutie nafasi ya Viti Maalum
 
Tulia tuwatafutie nafasi ya Viti Maalum
Yanga ni kama wale wakinadada wa Covid-19 wa Bawacha.
Alafu Simba ndo mzee Ndungai, anapambana wanamama(Yanga)waingie Bungeni(klabu bingwa)
Simba- Ndungai.
Yanga- Bawacha.
Bunge- Mashindano ya klabu bingwa.
 
Mkuu, target ya alama 13 ni nzuri sana lakini nadhani hata alama 10 zinaivusha kwenda hatua inayofuata.
Kwa ''nature'' ya haya mashindano, ni lazima wengine wakufanyie kazi.
Simba ikishinda mechi zote 3 za nyumbani na sare 1 yoyote ya ugenini (Alama 10), automatically atakua ananufaika na matokeo ya wapinzani wake (wanamfanyia kazi mwenye point 10).

Mambo ya kuzingatia kwa timu ya Simba kwa maoni yangu ni kama ifuatavyo:

1. Ili kuongeza morali ni lazima tupate pointi yoyote kwenye mchezo wa kwanza. (Never underestimate the power of starting big).

2. Tupunguze makosa yanayopelekea adhabu za mipira iliyokufa (kona na faulo), lakini pia tufanyie kazi ku-clear dead-balls zinazoelekezwa kwetu. (Mabeki wote wajitahidi kucheza kama Onyango katika hili).

3. Tuongeze ufanisi na aggressiveness kwenye kutumia nafasi za kufunga. Katika hatua hii wapinzani hawatakua wanakuruhusu utengeneze nafasi nyingi. Chache tunazopata tusizitapanye. Hapa Bwalya apigiwe sana kelele kwenye hili.

Vinginevyo nadhani tuna timu nzuri na tunaweza kufanya jambo na kuvuka hatua hii.
 
Mkuu maoni yako ni mazuri, shida ni mechanism ya namna tutavukaje! Kikosi cha Simba bila Onyango pale kati tayari kimeshaonekana kuleta wasiwasi hasa ukizingatia beki mwingine muhimu Erasto Nyoni nae haijulikani afya yake kama ataweza kucheza!
Kwa kocha anapaswa kushugulikia sana kwenye kujenga defence na tuwe na mfumo mzuri wa kujilinda.
Hata mechi ya juzi na Azam kilichotuponza ni defence na pia middle bado hazijaivana vizuri, nashauri kama vipi Mkude arudishwe pale kati!
Wachezaji wote wajengewe saikolojia nzuri ya ukabaji, watambue kuwa kila tunapopoteza mpira maana yake tunaanza kukaba sisi, na tukabe kwa kasi ili kuvuruga mbinu za wapinzani wetu. Timu ikiwa bora kwenye ukabaji huwa ni vigumu kupoteza mchezo hata ikiwa ugenini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…