Machale yapo ya kutoka kwa Mungu na yapo ya kutoka kwa Shetani, inategemea na Aina ya Maisha yako unayoishi. Ukibahatika ukapata ya kutoka kwa Mungu basi ujue umefanikiwa na umepata bahati na zawadi kubwa. Wapo watu wengi wanayo machale ya kutoka kwa Mungu ila si rahisi kujitangaza na huwezi kuwajua, wengi wao ni watu wanaopenda kujishusha. Na si lazima uwe kiongozi mkubwa wa dini ili uweze kupata zawadi hiyo kwa wale wapenzi wa masuala ya dini. watu wenye machale unaweza kuwajua kwa maneno na matendo yao. Mfano inaweza kutokea akatoa ushauri mkaukataa, ila anaweza asiwalazimishe lakini jambo hilo akalifanya peke yake [ukitaka kujua kuwa ana machale au la muulize akiwa peke yake madhara ya kutofuata ushauri huo] ( LAKINI si wote wanaofanya hivyo wana machale, isipokuwa ni dalili mojawapo ya watu hao).