Nini siri ya samaki samaki?

utinotino

Senior Member
Joined
Jan 23, 2014
Posts
119
Reaction score
45
Wadau, mimi nashangaa sana. Mlimani city unakuta samaki samaki pamejaa kupitiliza hadi tunasimama hapa parking area, lakini spots za pembeni wahudumu hadi wanabembeleza watu kuingia lakini kutupu!! Ni nini siri ya huyu jamaa wa samaki samaki? Ni business tactic gani anaitumia kuvutia watu hivi aisee.
Kwenye nyama choma festival, banda la samak samak watu wanakanyagana miguu hakuna hata nafasi ya kupumia! Mabanda ya pembeni peupe!!??

Ni siri tuambiane na tujifunze!
 
ni swali zuri sana mkuu..na mimi naomba nikuulize kama wewe ni mteja wao pia kitu gani kina kuvutia uwende samakisamaki,na usiende sehemu zingine.

mkuu hakuna lolote bali jamaa ni mbunifu, huduma ya uhakika na kwa wakati, chakula kiwango na visichana vingi virembo alivyovivisha vivazi vya kuvutia na mpangilio bora wa ratiba za chakula, uvaaji na muziki. Kabla hajabomolewa pale mbezi beach alikuwa anauza local bia 3,500 lakini hata seat ukichelewa hupati halafu ucku anakuwashia vibatari na warembo wanapangwa kila kona kukaribisha wagen dah cjui itarudi lini tena mbezi hakika nimeimiss sana
 

Unajua sisis waTanzania tuna shida sana,tukisikia kitu kinasifiwa na mabishoo basi tunafikiri eti ndiyo kitu kizuri.Huenda kuna watu walimuona Diamond na Wema wanakula pale basi ikawa taabu.Unanikumbusha mbali sana enzi za chuo kuna saluni moja ipo maeneo ya Tambaza pale Upanga,ebwana si mama Anna Nkapa akawa anaenda kutengeneza nywele pale nakuambia ile saluni ikapata umaarufu ghafla tukawa tumeingia kwenye vita na mademu zetu nakuambia kla demu akawa anataka kusukwa Upanga
 

hahahaa, kwa hiyo na sisi wazee tunaangalia dayamondi anakula wapi? washabiki wa huyo dayamondi wenye umri wa kumuiga hawana hata hiyo pesa ya kula samakisamaki! siri ya urembo ni HUDUMA NZURI.
 
hahahaa, kwa hiyo na sisi wazee tunaangalia dayamondi anakula wapi? washabiki wa huyo dayamondi wenye umri wa kumuiga hawana hata hiyo pesa ya kula samakisamaki! siri ya urembo ni HUDUMA NZURI.
Sina uhakika sana lakini nakuamabia asilimia 85% ya watu wanaokula Samakisamaki ni mabrothermen na ma sisterdu, asilimia 10% wanaenda pale kula na kupanga mipango either ya maendeleo, ya wizi ama ya kutafuta wake za watu ni asilimia 3% ya waendaji wa Samakisamaki wanaoenda kwa ajili ya kula na kunywa tu na asilimia 2% wanaenda pale by coincidence yaani wanashangaa wapo pale wanakula na kunywa lakini ukiwauliza kwa nini wapo pale hawajui hata kidogo.Sasa sijui wewe upo upande upi katika huo mchanganuo wangu
 
Huwa naisikiaga tu ila sijawahi kuingia.

Kipindi nilivyokuwa kijana nlikuwa naingia chicken hunt sijui bado ipo??

Otherwise, kwa mama kamcheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Asee sikumbuki mara ya mwisho nmeenda mliman city ni lini daah inabdi na mm niende siku moja sio kula lkn kuangalia hvo vibinti lazima niondoke na namba ya simu.
 

Mkuu nafikiri uko sahihi kabisa. Niliamua kufanya ka study nikaenda ile restaurant pembeni na kuagizia salad. Ilichukua dakika 52 kuja. Nilishangaa sana na kahudumu kana kauli mbaya. Nikamwita manager ambaye alikua mstaarabu na kumuelewesha.
Kwaio uko sahihi ulivosema hapo, cha kushangaza kingine hizi restaurant za pembeni zinashindwa kabisa ku copy jirani yao na ku improve kidogo?
Au ni uvivu wa fikra? Ingekua mimi ni mmiliki wa restaurant za pembeni ningeapply similar formula.
 
Aisee,ngoja mimi niseme kwanini nilienda na napenda kwenda Samaki Samaki M.City:
1. Huduma nzuri (prompt service kinywaji na chakula
2. Muziki mtamu (Wa Enzi hzo[Groove Back] ulio-tuniwa vizupgpi: RnB, House,Pop,Hip Pop etc)
3. Parking ya kutosha na safi (sehemu zingine gari unaipaki kuchafu ama kwenye tope tope)
3. Usalama (kwa mnywaji na kwa gari - kwingine umepaki hatua mia nne kule mara mjinga mjinga wakati anatoa gari yake anakubonyeza halafu huna taarifa,wakati wa kuondoka ama kesho yake ndipo unagundua)
4. Interactions (ni sehemu ambayo unaeza ku-hang out na kukutana na wageni-'expatriates' toka nchi mbalimbali na kujenga network za maana)
5. Ni center kwangu na washkaji zangu, so its easy to drive towards or from it)

Etc, etc, etc
 
Samakisamaki ya Morogoro nayo balaa kwa kujaza wateja,kuna siku nilikula ujana kushtuka saa moja asubuhi.
 

sehemu zingine mi nazisikiaga tu
 
me hata ukiniuliza hio samaki cjui imekaa upande gan
 
Jamaa wana huduma nzuri na ameweza kuweka ubora huo popote ilipo samakisamaki.
Hawa wa migahawa mingine mlimani city wanahuduma mbovu halafu wafanyakazi viburi na lugha chafu.
Ni matatizo ya mameneja wabovu.
Samakisamaki naona anaandaa mazingira pale rock city malls mwanza. Anafanya vzr
 

huo utafiti wako hauna mashiko! mimi pale huwa naenda kwa ajili ya sumu fulani kuna mtu mmoja anajua sana kuichanganya pale, chakula safi fast, ni wabunifu sana wa viburudani vya hapa na pale. vipi mkuu, una biashara ya mfanano na huo sehem unaona haiendi nn?....wape tu hongera zao, wako vizuri, ni wabunifu!
 
pamoja huduma nzuri,wabongo wanaona sifa kwenda samaki samaki yaani wanajitutumua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…