Nini siri ya samaki samaki?

Nini siri ya samaki samaki?

si mseme yule mkaburu anaevaa kimasai na ambae tabia zake si za kikaburu kwani anapenda mambo ya kibongobongo,ni shemeji yenu kwani anagonga dada yenu?
 
Ni swali zuri sana mkuu..na mimi naomba nikuulize kama wewe ni mteja wao pia kitu gani kina kuvutia uwende samakisamaki,na usiende sehemu zingine.
Watanzania tulio wengi ni "bendera fuata upepo" ukiwauliza wateja wengi wa samaki samaki ili swali watashindwa kukujibu. Wengi wanakwenda kwasababu panajaa.
 
Wadau, mimi nashangaa sana. Mlimani city unakuta samaki samaki pamejaa kupitiliza hadi tunasimama hapa parking area, lakini spots za pembeni wahudumu hadi wanabembeleza watu kuingia lakini kutupu!! Ni nini siri ya huyu jamaa wa samaki samaki? Ni business tactic gani anaitumia kuvutia watu hivi aisee.
Kwenye nyama choma festival, banda la samak samak watu wanakanyagana miguu hakuna hata nafasi ya kupumia! Mabanda ya pembeni peupe!!??

Ni siri tuambiane na tujifunze!

Nashukuru sana kwa swali zuri, ndio maana tunasema sio rahisi kuielezea BUSINESS MODEL kwamba huyu anafanya hivi na vile,,, la sivyo ingekuwa rahisi sana watu ku copy na ku paste na kufaulu pia ! ! !

Pia wasomi na watafiti wa biashara ndio wangekuwa vinara kwa biashara, ni sawa na kusema kwa mashule ya sekondary ST,MARY wanafanyaje kwa kuwa washindi wa kwanza miaka yote ? watu wameiga sana na hata kuwahamisha watumishi/waalimu karibia wote kila mwaka bado HAWAFANIKISHI,,,,,,,,,,,

Mara nyingi BUSINESS MODEL inafanana na founder wa biashara, pana vitu vidogovidogo sana na vingi vinapuuzwa kwa kuchanganya na vikubwa vinavyoonekana INAKAMILIKA,,,,

Na kuhama toka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ni kama ilivyo ujasiriamali inahitajika isipungue 10 yrs na hata zaidi kwa kuwa sambamba na mhusika

Waweza kutambua baadhi tu kwa ku-google GET's General Enterprising Tendecies
 
si mseme yule mkaburu anaevaa kimasai na ambae tabia zake si za kikaburu kwani anapenda mambo ya kibongobongo,ni shemeji yenu kwani anagonga dada yenu?

Heeee dada yetu yupiii???
 
Unajua sisis waTanzania tuna shida sana,tukisikia kitu kinasifiwa na mabishoo basi tunafikiri eti ndiyo kitu kizuri.Huenda kuna watu walimuona Diamond na Wema wanakula pale basi ikawa taabu.Unanikumbusha mbali sana enzi za chuo kuna saluni moja ipo maeneo ya Tambaza pale Upanga,ebwana si mama Anna Nkapa akawa anaenda kutengeneza nywele pale nakuambia ile saluni ikapata umaarufu ghafla tukawa tumeingia kwenye vita na mademu zetu nakuambia kla demu akawa anataka kusukwa Upanga

Watanzania hawana shida yoyote. Ni ukweli tu wa kisoko na saikolojia ya wanadamu dunia nzima. Na marketers wazuri wanalijua hilo. Hivi unadhani kwa nini ma-celebrity wanatumika kutangaza bidhaa mbalimbali duniani? Mama Mkapa alikuwa celebrity wa Bongo, kwa hiyo of course anakoenda lazima umma nao uende...basic psychology hiyo.
 
mkuu hakuna lolote bali jamaa ni mbunifu, huduma ya uhakika na kwa wakati, chakula kiwango na visichana vingi virembo alivyovivisha vivazi vya kuvutia na mpangilio bora wa ratiba za chakula, uvaaji na muziki. Kabla hajabomolewa pale mbezi beach alikuwa anauza local bia 3,500 lakini hata seat ukichelewa hupati halafu ucku anakuwashia vibatari na warembo wanapangwa kila kona kukaribisha wagen dah cjui itarudi lini tena mbezi hakika nimeimiss sana


Jibu Unalo!
 
Jamaa wana huduma nzuri na ameweza kuweka ubora huo popote ilipo samakisamaki.
Hawa wa migahawa mingine mlimani city wanahuduma mbovu halafu wafanyakazi viburi na lugha chafu.
Ni matatizo ya mameneja wabovu.
Samakisamaki naona anaandaa mazingira pale rock city malls mwanza. Anafanya vzr

Akikuja huku wallah atakuwa kanikamata hata mie...
 
Back
Top Bottom