Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watanzania tulio wengi ni "bendera fuata upepo" ukiwauliza wateja wengi wa samaki samaki ili swali watashindwa kukujibu. Wengi wanakwenda kwasababu panajaa.Ni swali zuri sana mkuu..na mimi naomba nikuulize kama wewe ni mteja wao pia kitu gani kina kuvutia uwende samakisamaki,na usiende sehemu zingine.
Wadau, mimi nashangaa sana. Mlimani city unakuta samaki samaki pamejaa kupitiliza hadi tunasimama hapa parking area, lakini spots za pembeni wahudumu hadi wanabembeleza watu kuingia lakini kutupu!! Ni nini siri ya huyu jamaa wa samaki samaki? Ni business tactic gani anaitumia kuvutia watu hivi aisee.
Kwenye nyama choma festival, banda la samak samak watu wanakanyagana miguu hakuna hata nafasi ya kupumia! Mabanda ya pembeni peupe!!??
Ni siri tuambiane na tujifunze!
si mseme yule mkaburu anaevaa kimasai na ambae tabia zake si za kikaburu kwani anapenda mambo ya kibongobongo,ni shemeji yenu kwani anagonga dada yenu?
Unajua sisis waTanzania tuna shida sana,tukisikia kitu kinasifiwa na mabishoo basi tunafikiri eti ndiyo kitu kizuri.Huenda kuna watu walimuona Diamond na Wema wanakula pale basi ikawa taabu.Unanikumbusha mbali sana enzi za chuo kuna saluni moja ipo maeneo ya Tambaza pale Upanga,ebwana si mama Anna Nkapa akawa anaenda kutengeneza nywele pale nakuambia ile saluni ikapata umaarufu ghafla tukawa tumeingia kwenye vita na mademu zetu nakuambia kla demu akawa anataka kusukwa Upanga
mkuu hakuna lolote bali jamaa ni mbunifu, huduma ya uhakika na kwa wakati, chakula kiwango na visichana vingi virembo alivyovivisha vivazi vya kuvutia na mpangilio bora wa ratiba za chakula, uvaaji na muziki. Kabla hajabomolewa pale mbezi beach alikuwa anauza local bia 3,500 lakini hata seat ukichelewa hupati halafu ucku anakuwashia vibatari na warembo wanapangwa kila kona kukaribisha wagen dah cjui itarudi lini tena mbezi hakika nimeimiss sana
Jamaa wana huduma nzuri na ameweza kuweka ubora huo popote ilipo samakisamaki.
Hawa wa migahawa mingine mlimani city wanahuduma mbovu halafu wafanyakazi viburi na lugha chafu.
Ni matatizo ya mameneja wabovu.
Samakisamaki naona anaandaa mazingira pale rock city malls mwanza. Anafanya vzr
Akikuja huku wallah atakuwa kanikamata hata mie...
Lakini hata Dagaadagaa Shekilangi inabamaba pia!