Nini story au kisa nyuma ya username yako na avatar yako hapa JF

mwanzo nilikua natumia ID nyingine baadae nikaja kusahau password ndo nikaamua kuja na jina langu kamili....na hiyo avatar nimm mwenyewe huyo!
 
Sina undugu na Membe ila ni home boy wangu tu na namkubali kwa kazi zake na harakati zake simjui hanijui ila nilitamani awe Rais kwa sababu ya kazi zake huwa nazikubali sana jamaa ni jembe la KIMWERA ila now kamuachia MAJALIWA harakati za kwenda MAGOGONI akishindwa basi mimi nitakuwa nimeshakomaa tayari kwa kukabidhiwa nchi ili kuwavusha Watanzania kuwafikisha katika nchi ya ahadi.
 
mwanzo nilikua natumia ID nyingine baadae nikaja kusahau password ndo nikaamua kuja na jina langu kamili....na hiyo avatar nimm mwenyewe huyo!

Sante sana ndugu mwaipopo, umenikumbusha nilipokuwa Alevel pale Swilla High School, mbeya. Nilikuwa kwenye darasa ambalo zaidi ya asilimia 90 ya wafunzi wenzetu walikuwa na ubini unaoamziwa na MWA😱😱
 
Sawa KAPUKU.....
 
nilisoma kitabu cha Muhammed Said "THE HISTORY OF ABDULWAHID SYKES, The Untold Story of Muslim stragle in Tanganyika...... basi nikajikuta navutika na hiyo historia yake mwisho nikajikuta natumia hilo jina lake kwny mitandao ya kijamii kama ishara ya kumkubali, alikua muungwana na mzalendo.
 
Niite Sukari Yenu, ni sukari yenu hivo hivo. Nililazimisha nipendwe na kila mtu darasani, ilikua chuo tupo first year ndio tumepanga tukutane wote for the first time tujuane na mipango mikakati maana ilikua ngumu kumtambua mtu unayesoma naye Degree Program moja coz firsr year wote wa school ya business studies tulikua tunachanganyika na kushare course.

Kila mtu akawa anajitambulisha na anasema wishes, ambitions n.k kwa muda wote atakao kuwa chuo, wengine wanatia mbwembwe kibao. Kama kawaida mademu wengi wanafeel shy. Patamu hapo.

Ikafika zamu yangu, nikasimama, nikakohoa kidogo. Nikijifanya kama kuna kitu nawaza hivi, nikaongea kwa lafudhi ya Kipemba, yakhee mi naitwa Sukari Yenu. Watu eeh? Nikarudia...class ya watu 78 ikaburst into laughter.
Jamaa mmoja akanikazia, bro kuwa serious kuna kundi la madem wakamkazia yeye kwamba kwanini anasema mi sipo serious.

Niliiteka hadhira yote na nikawa kama comedian hivi. Wavulana wengi wakawa hawalipendi hilo jina lakini ndio ilikua njia rahisi ya kunikumbuka. Na nashukuru lilienea sana kwa mademu hasa kule hostel zao mpaka kuna siku nilikuta ubishi mkali. Kuna demu mmoja alikua anajua jina langu halisi akawa anawaambia wenzake wanamkatalia wanakomaa mi naitwa Sukari hivyo hivyo. Ilikua balaa...nilikua maarufu ghafla kuliko first year yeyote huku nikichagizwa na kuwasolvia solvia maswali mademu.

Lengo langu siku ile ya kujitambulisha lilikua kuwaambia mi ambition yangu ni kupendwa na kila mtu. Kwa hiyo mimi ni Sukari Yenu. Vicheko vilitawala mpaka sikutaja jina langu halisi.

Pale Ubungo kuna bar inaitwa Yenu....sjui ni registered name. I wish nisajili kitu yangu binafsi e.g company niite hivyo hivyo Yenu.
Tchao,
Sukari Yenu.
 

The best tale so far🙄🙄
 
User name Ochu inatoka kwa my late best friend tulicheza wote na kusoma wote hadi tulipofika 11 years, siku moja tukiwa tunacheza akashikwa na haja akawa anakimbilia kwao ndipo alipokanyaga mfuniko mbovu wa chemba na kutumbukia ndani huku tunamwona,kwani tuliishi kwenye flats,alitolewa ameshafariki.
Avatar ni kwa sababu namkubali sana J.Cole,personality na lifestyle yake.
 
Mimi ID yangu ilitokea baada ya kuwa inspired na mtu muhimu sana kwangu. Kwahiyo jina ndo lilipotokea..... Nahrene (Jina lake na la kwangu). Nilikuwa natumia hili jina kama nickname kwa muda mrefu sasa
 
Mimi ID yangu ilitokea baada ya kuwa inspired na mtu muhimu sana kwangu. Kwahiyo jina ndo lilipotokea..... Nahrene (Jina lake na la kwangu). Nilikuwa natumia hili jina kama nickname kwa muda mrefu sasa

Sante sana Nahrene, i can see the name irene in there, na huyo kwenye avatar ni wewe?!

Wewe pia uko kwenye list yangu
 
Napenda sana uigizaji wa Robert De Niro...
kuna movie inaitwa...Analyze this ..
aliulizwa na daktari 'what do you do for a living?'
akajibu 'i am the boss' 'i don't do anything'..
sijawahi isahau hiyo scene....

Asante mkuu, wewe pia ulokuwa kwenye list yangu, avatar na jina vinaendana
 
Napenda sana uigizaji wa Robert De Niro...
kuna movie inaitwa...Analyze this ..
aliulizwa na daktari 'what do you do for a living?'
akajibu 'i am the boss' 'i don't do anything'..
sijawahi isahau hiyo scene....
Hiyo sura ndo wewe mkuu?
 
Mimi ID yangu ilitokea baada ya kuwa inspired na mtu muhimu sana kwangu. Kwahiyo jina ndo lilipotokea..... Nahrene (Jina lake na la kwangu). Nilikuwa natumia hili jina kama nickname kwa muda mrefu sasa

Huwa nahisi utakuwa very very cute...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…