Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mwanzo nilikua natumia ID nyingine baadae nikaja kusahau password ndo nikaamua kuja na jina langu kamili....na hiyo avatar nimm mwenyewe huyo!
Njoo gheto ubebe na zingineAll star (converse) ndo viatu ninavyovaa mara nyingi. Navipenda sababu viko simpo sana
Sawa KAPUKU.....Ukiitazama hiyo avatar yangu ni imagination yenye kuleta uhalisia wa eneo flani.
Na kuhusu kutumia jina la EMMYGUY, namthamini, nampenda, na kumheshimu sana mama yangu aitwae EMMY maana tangu kanizaa mpaka nimekuwa mkubwa sasa bado ana mchango mkubwa sana katika kufanikisha furaha yangu.
cc: Linamo, sizzya007.
Niite Sukari Yenu, ni sukari yenu hivo hivo. Nililazimisha nipendwe na kila mtu darasani, ilikua chuo tupo first year ndio tumepanga tukutane wote for the first time tujuane na mipango mikakati maana ilikua ngumu kumtambua mtu unayesoma naye Degree Program moja coz firsr year wote wa school ya business studies tulikua tunachanganyika na kushare course.
Kila mtu akawa anajitambulisha na anasema wishes, ambitions n.k kwa muda wote atakao kuwa chuo, wengine wanatia mbwembwe kibao. Kama kawaida mademu wengi wanafeel shy. Patamu hapo.
Ikafika zamu yangu, nikasimama, nikakohoa kidogo. Nikijifanya kama kuna kitu nawaza hivi, nikaongea kwa lafudhi ya Kipemba, yakhee mi naitwa Sukari Yenu. Watu eeh? Nikarudia...class ya watu 78 ikaburst into laughter.
Jamaa mmoja akanikazia, bro kuwa serious kuna kundi la madem wakamkazia yeye kwamba kwanini anasema mi sipo serious.
Niliiteka hadhira yote na nikawa kama comedian hivi. Wavulana wengi wakawa hawalipendi hilo jina lakini ndio ilikua njia rahisi ya kunikumbuka. Na nashukuru lilienea sana kwa mademu hasa kule hostel zao mpaka kuna siku nilikuta ubishi mkali. Kuna demu mmoja alikua anajua jina langu halisi akawa anawaambia wenzake wanamkatalia wanakomaa mi naitwa Sukari hivyo hivyo. Ilikua balaa...nilikua maarufu ghafla kuliko first year yeyote huku nikichagizwa na kuwasolvia solvia maswali mademu.
Lengo langu siku ile ya kujitambulisha lilikua kuwaambia mi ambition yangu ni kupendwa na kila mtu. Kwa hiyo mimi ni Sukari Yenu. Vicheko vilitawala mpaka sikutaja jina langu halisi.
Pale Ubungo kuna bar inaitwa Yenu....sjui ni registered name. I wish nisajili kitu yangu binafsi e.g company niite hivyo hivyo Yenu.
Tchao,
Sukari Yenu.
Mimi ID yangu ilitokea baada ya kuwa inspired na mtu muhimu sana kwangu. Kwahiyo jina ndo lilipotokea..... Nahrene (Jina lake na la kwangu). Nilikuwa natumia hili jina kama nickname kwa muda mrefu sasa
Sante sana Nahrene, i can see the name irene in there, na huyo kwenye avatar ni wewe?!
Wewe pia uko kwenye list yangu
Napenda sana uigizaji wa Robert De Niro...
kuna movie inaitwa...Analyze this ..
aliulizwa na daktari 'what do you do for a living?'
akajibu 'i am the boss' 'i don't do anything'..
sijawahi isahau hiyo scene....
Everlenkiiiiii sijakutenga Mae, umepotea sanaKyutiii biiii......lol.....siyo kwa kunitenga huko.
Hiyo sura ndo wewe mkuu?Napenda sana uigizaji wa Robert De Niro...
kuna movie inaitwa...Analyze this ..
aliulizwa na daktari 'what do you do for a living?'
akajibu 'i am the boss' 'i don't do anything'..
sijawahi isahau hiyo scene....
Mimi ID yangu ilitokea baada ya kuwa inspired na mtu muhimu sana kwangu. Kwahiyo jina ndo lilipotokea..... Nahrene (Jina lake na la kwangu). Nilikuwa natumia hili jina kama nickname kwa muda mrefu sasa