Nini suluhisho kwa vijana wetu walio mitaani wasiokuwa na Ajira?

Nini suluhisho kwa vijana wetu walio mitaani wasiokuwa na Ajira?

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Wazazi na vijana wamepoteza kabisa matumaini ya maisha, wanaishi kwa misongo ya mawazo kila siku.

Kila siku afadhali ya jana na serikali imetamka kuwa haiwezi ajiri vijana wote wanaotoka vyuoni bali wajiajiri.

Lakin haiwawezeshi njia za vijana hao kujiajiri, Bali ni matamko tu.

Kwa wenzetu nchi za Magharibi serikali inajali sana vijana wasiokuwa na Kipato yaani wale watu wa hali ya chini na wale wasiokuwa na Ajira kuna mpango maalum serikali hufanya juu yao kama vile malipo kidogo ya kujikimu kila mwezi kutoka katika serikali zao za mitaa.

Lakini Katika nchi nyingi za kiafrika na hata hapa kwetu ijapo tuna rasilimali za kutosha lakini Muundo mzima wa serikali yetu unatafunya tuishi kama tulivyo sasa,maana hata Demokrasia hakuna, na hivyo hakuna uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.
Ni kama tupo ndani ya boksi
 
Sekta ya kilimo na madini TANZANIA inaweza ikaajiri jumla ya vijana wote wa Afrika mashariki nzima na bado wasiitosheleze.
Shida Hakuna mswahili anaeweza mletea maendeleo mswahili mwenzake hii ni nature.
Hatuna watu wanaofikiri thus badala ya mito kumwaga maji mashambani eti inamwaga baharini,madini yapo mengi Sana ardhini wageni ndio wanufaika.
Market ya mazao ya kilimo na madini ni unlimited duniani.Shida tumekosa viongozi wanaofikiri.
Ingewekana wananchi tuagize au tuajiri viongozi toka nchi zingine wanaofikiri ingependeza zaidi.
 
Popote duniani hawajaajiwa wote! Kama wewe ni kijana na unasaka kazi unaweza usiajiriwe milele.

Pambana sana kwenye vibarua na utapeli mix
Hata hivo vibarua venyewe kupata ni shida. Serikali ipo kwa ajili ya wananchi wake je ifanyeje kupunguza tatizo lililopo
 
Wazazi na vijana wamepoteza kabisa matumaini ya maisha, wanaishi kwa misongo ya mawazo kila siku.

Kila siku afadhali ya jana na serikali imetamka kuwa haiwezi ajiri vijana wote wanaotoka vyuoni bali wajiajiri.

Lakin haiwawezeshi njia za vijana hao kujiajiri, Bali ni matamko tu.

Kwa wenzetu nchi za Magharibi serikali inajali sana vijana wasiokuwa na Kipato yaani wale watu wa hali ya chini na wale wasiokuwa na Ajira kuna mpango maalum serikali hufanya juu yao kama vile malipo kidogo ya kujikimu kila mwezi kutoka katika serikali zao za mitaa.

Lakini Katika nchi nyingi za kiafrika na hata hapa kwetu ijapo tuna rasilimali za kutosha lakini Muundo mzima wa serikali yetu unatafunya tuishi kama tulivyo sasa,maana hata Demokrasia hakuna, na hivyo hakuna uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.
Ni kama tupo ndani ya boksi
Umeuliza swali umeishia hewani ukilalamika tu!
 
Popote duniani hawajaajiwa wote! Kama wewe ni kijana na unasaka kazi unaweza usiajiriwe milele.

Pambana sana kwenye vibarua na utapeli mix
Huko awajawatupa vijana wao wametengeneza mfumo ambao ni rahisi kuajiri kwa mzawa so kuwa masikini ni choice yako.
Sapoti ni nyingi Sana kwa chochote ukitaka kufanya,mkulima analima Kazi ya soko sio jukumu lake,unazalisha chochote ishu ya market sio yako.
Sisi KILA kitu upambane mwenyewe utafute mtaji,soko,KILA kitu pekee yako huku kodi na tozo zipo kupunguza mtaji wako,kwetu virudisha nyuma ni vingi sana ikiwemo mifumo ya kukubana usiendelee wakiami huwezi mtawala mwenye shibe hii ni nadharia za kimasikini za kijamaa kwamba mtawaliwa apaswi kuwa na nguvu kuliko mtawala.
 
Rasilimali Rasilimali Rasilimali
Serikali ya Tanzania toka Uhuru imekua ikisema tuna Rasilimali Rasilimali Rasilimali mpaka leo awamu hii ya mama. We have to change mindset hata kidogo tuwe tunazungumzia kuzitumia hizo Rasilimali ilitupate matokeo pendwa.

I hate the phrase " Tanzania tunarasilimali"
 
Kweli Kabisa huo wingi wa madini tulio nao, bandari pamoja na ardhi ya rutuba tulio nao inatosha kabisa kuibadilisha hii nchi na sio kuwa omba omba kila wakati kwa nchi tajiri.
Tungepata viongozi wale wa juu watakaosimama haswa kwenye rasilimali tulizo nazo, umaskini ingekuwa ni hadithi nchi hii
 
Inueni sekta ya kilimo tengenezeni mazingira, miundo mbinu,masoko kwenye masuala ya kilimo watu vijana wengi watajikita huko
Bila kufanya hivyo taifa litazidi kuwa la bongo
Fleva tu

Ova
 
Kuanzia shule ya msingi wafundishwe ujenzi, ushonaji,na mengine na mengine km hayo.Yaani veta ianzie darasa la kwanza
True huu mfumo wa sasa wa elimu hauna msaada,vyuo vya maarifa ya kujinasua yaani vya ujasilimali ndo vinatakiwa viwe vingi sana Ili wengi wapite kule unamaliza la saba unaingia chuo unasoma fani ujuzi ukimaliza unaingia mtaani una ujuzi zaidi ya tatu mfano umefuzu udereva,ujenzi,useremala umeiva kote utakuwa vipi masikini sasa hapa.
Serikali ianzishe veta KILA kata na iwakopeshe elimu vijana watalipa kupitia TIN number kuliko kutupa pesa kwa kukopesha vyuo vikuu kisha wahitimu wanarudi kuwa machinga na bodaboda sababu imeshindwa waajiri na kichwani ni empty wamekariri archimedes principle na logarithms tu ambapo havina msaada.
Thus unakuta mtu kapoteza miaka 25 darasani anazidiwa maisha na la saba failure ambae akuendelea na shule sababu wazazi wake hawana uwezo akaamua kupambana mtaani akapata ujuzi wa kuzalisha.
Kuliko kumpa Mkopo mhitimu mmoja jumla ya milioni 7 kwa miaka 3 then awarudishi mikopo si bora hio milioni 7 ya mwanachuo mmoja ingetosha kuwapa darasa la saba 20 wakapata ujuzi baada ya mwaka mmoja tu zinaanza kurudi kupitia TIN number, kuliko kutupa kwa kuwakopesha wanachuo wakimaliza utawapatia wapi hawana ajira.
Kuwa na vyuo vikuu vingi katika nchi ni kuongeza idadi ya masikini nchini, kwa maana hata wakihitimu wanarudi vijiweni au kuwa mzigo vijijini.
 
Inueni sekta ya kilimo tengenezeni mazingira, miundo mbinu,masoko kwenye masuala ya kilimo watu vijana wengi watajikita huko
Bila kufanya hivyo taifa litazidi kuwa la bongo
Fleva tu

Ova
Hata mkoloni alijenga nchi hii kupitia kilimo.
Aliinua kilimo kwanza ndipo vikaja viwanda.
 
Raslimali tele zilizojaa ni nyingi Sana kuliko idadi ya wasaka ajira.
 
Inueni sekta ya kilimo tengenezeni mazingira, miundo mbinu,masoko kwenye masuala ya kilimo watu vijana wengi watajikita huko
Bila kufanya hivyo taifa litazidi kuwa la bongo
Fleva tu

Ova
Wazo zuri sana mkuu, wizara ya kilimo ipo pale kuneemesha mawaziri wake pamoja na makatibu wake na sio kumbeba mkulima na wale wote wanaotaka kujiingiza kwenye kilimo
 
Tena ilibidi wizara ya kilimo ihamishiwe vijijini huko ile iwe rahisi kwenye utandaji. Na sio wizara ya kilimo inakaa Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom