Nini tatizo? Binti mrembo anajua kuvaa, msomi ila ananuka mdomo

Nini tatizo? Binti mrembo anajua kuvaa, msomi ila ananuka mdomo

Mtu yeyote anaelala usiku bila kupiga mswaki lazima anuke mdomo.

Mtu unaswaki asubuhi, Siku nzima unakula kila utakacho, afu unalala hivyo hivyo, unategemea nini?

Procedure ni kupiga mswaki asubuhi na usiku umalizapo kula swaki ndo ulale.
Akifanya hivyo ikashindikana mshauri anunue mouth wash.

Ikishindikana jua ana jino bovu limetoboka, halifanyii usafi uchafu umejaa humo.
Ila mtihani unao ni ngumu sana sanaaa kumwambia mtu hicho kitu.

Kuna mwanaume alikuwa ananipenda sana tu,alikuwa na kila kitu mwanamke anachotamani, ila nilishindwa proposal yake, kila akiniuliza kwa nini simpendi namdanganya namchukulia kama kaka.
Kumwambia ilishindikana, ati nae sasa hivi kaoa, hivi wanalala vip kama kuongea tu naskia mmmmh , dah mapenzi upofu.
Halafu wa hivyo wana meno mazuri asikwambie mtu. Na kama ni mdada unakuta ni nzuri balaa.
Sidhani kuna watu wanashinda wiki hapigi mswaki au sanasana akutane na mswaki wa kijiti na hanuki mdomo hata robo.
 
[emoji3]demu aliua
Hii niliwahi kuwaambia.

Tukiwa O Level kuna mshkaji wetu akang'oa pini inaitwa Amina, hii pini ilikua inasoma Perfect Vision basi tulikua tunampa kampani mshkaji wetu kwenda kwa shemeji.

Over time tukajua shemeji ana shida na harufu ya mdomo mshkaji kumwambia hakuweza akatuomba ushauri.
Washkaji wa Class Z tukamshauri amnunulie dawa ya meno na mswaki ampe.

Jamaa akampelekea binti whitedent kubwa na miswaki miwili.

Jamaa akaja kutuambia tatizo halijakata.

Akamuuliza binti "Kama umemaliza zile zawadi nikuletee zingine" binti akajibu "Hapana nimezitunza zawadi zako mpenzi wangu"
 
mara nyingi harufu hukaa kwenye ulimi sio katika meno,
na watu wengi huwa wanasugua meno na kusahau ulimi, na hapo kwemye ulimi ndio huwa panatoa harufu so unaweza ukasugua ulumi tu na meno yawe machafu na harufu isitoke.

kipindi nikiwa shule ya msingi alikuja baba yetu mdogo yeye kila baada ya mlo anasugua meno hapo ni mara tatu kwa siku, lakini akikuongelea tu usoni aiseeee
unatamani ukimbie ukiwa na presha inapanda mda uouo(kiding)
Ila tulipomuambia kuhusu kusugua ulimi basi harufu haikuwahi kutoka tena, wale wanaokuwa wanashida ni wale ambao ulimi anausugua lakini harufu unakuta baada ya masaa kama manne au matano inaanza,
lakini pia unapokuwa unasugua meno sio lasha lasha kama wengi walivyozoea,
kabla haujaanza kusukutua unapaswa usugue hadi ile harufu ya dawa iwe imeisha kunywani mwako hapo ndio unaanza sasa kusukutua na maji,
tmesimama kwenye gari nilikuwa naongea na simu kuna bint alikuwa mbele yangu basi baada ya kumaliza kuongea nasimu kwa mara ya kwanza binti akaniomba namba,
baadaye anasema kavutiwa na harufu ya mdomo wangu,
khaaa nikashangaa sana kuingia google kuangalia angalia nikaja ona kumbe ukiwa na harufu fresh kinywa mara nyingi wanawake wengi hupenda kupata walau denda tu.
ha ha ha anyway tuachane na hayo ila muhimu azingatie kusugua ulimi, anywe maji ya kutosha pia, apende kutumia matunda haswa kama matikiti na nanasi au freshi juisi yake.
asikae mda mrefu pasipo kwenda haja pia la msingi ikizidi zaidi ya hapo akaangalie bakiteria hosipitali
 
Wakuu salaam

Sina lengo la kukashfu maumbile ya mtu, bali kutaka kujua sababu ziwe za kisayansi au nyinginezo. Kuna binti nipo naye karibu mazingira ya ofisini kwetu. Huyu binti ni nzuri na anajua sana kuvaa kuendena na wakati

Mara nyingi nikimkaribia na tukiwa tunaongea naskia harufu ya mdomo wake. Nilijua ni tatizo la siku moja ila kadri siku zinavyosonga mbele naona bado ile hali anayo

Sasa wakuu hivi hii usababishwa na Nini? Naamini mswaki anapiga vizuri tu ila sijui chanzo cha yule binti kunuka mdomo kiasi kile

Najisikia noma kumwambia na sijui nitumie njia gani kumfikishia ujumbe kwamba Ananuka mdomo atafute tiba
Siku moja jitolee tafuta mouth wash nzuri mpelekee mwambie asukutue baada ya kupiga mswaki inalinda meno kutoboka
 
Back
Top Bottom