ICBM ina arc yake ikifyatuliwa haipindipindi angani, inaenda nje ya anga la dunia kisha inaingia anga la dunia (re-entry). Uko nje ya anga la dunia sababu hakuna friction inaenda kwa kasi kubwa na inakuja nayo duniani.
ICBM ni nzito inaweza beba multiple reentry vehicles (MIRVs) vichwa vya warheads kadhaa vikatua sehemu tofauti. Haina shabaha kubwa sababu mlipuko ni mkubwa sanasana inabeba nuclear warhead hata circular error probable (CEP) ikiwa 1km sawa.
ICBM inaweza fyatuliwa ardhini kwenye missile silos kama Minuteman series ya Marekani
View attachment 3148453
Kuna za kufyatuliwa kwenye magari makubwa TEL kama RS-28 Sarmat ya Urusi
View attachment 3148457
Kuna ya kufyatuliwa na nuclear submarine ni submarine-launched ballistic missile (SLBM) kama Trident ya Marekani
View attachment 3148452
Cruise missile inaendeshwa na jet engine mara nyingi, jet engine inaweza piga kona. Cruise missile inaendeshwa na inertial guidance ikaongezwa na terrrain following na pia lazima mifumo ya satellite kama GPS, Glonass au BeiDou ihusike.
Cruise missile haitoki nje ya dunia na haina speed kubwa sana ila haitabiriki inakoenda maana inaweza kata kona. Ina accuracy nyingine hadi within 30m CEP nyingine 5m CEP. Anti ship cruise missiles ndio zina CEP ndogo zaidi.
Cruise missiles sio ngumu sana kuunda nchi zikijitutumua zinaunda tu. Cruise zinabebwa hata na ndege.