Wachangiaji wooote mmekosea!
Nimefuatilia namna wote mlivyo changia hii mada na kugundua kuwa wote mmekosea.
Maziko na Mazishi yote yanamaanisha kitu kimoja
Kwa Mujibu wa Kamusi ya TUKI
Maziko nm [ya-] funeral, burial, interment, exequies:
Mazishi nm [ya-] funeral, burial.
Sasa kwa sababu kuna maswali mengine yameongezwa hapa ngoja niwajibu!
Msiba nm mi- [u-/i-] bereavement, sorrow, misfortune; disaster.
(ms) Hakuna matanga usiokuwa na mwezi - misfortune never comes singly;
Msiba mkuu - catastrophe.
Matanga nm [ya-] mourning period: Weka matanga - remain in mourning; Vunja/ondoa matanga - end mourning;
Kilio nm vi- [ki-/vi-] 1 wailing. 2 cry, shout. 3 mourning. 4 problem. Kilio cha maji water problem.
.