Nini Tofauti ya Leaded na Unleaded Petrol?

Naomba nichangie hapo kidogo mkuu,

Kuhusu UNLEADED & LEADED. Katika mafuta ya Petroli kuna kemikali ambazo huwa zinawekwa kwaajili ya kusaidia #perfomance ya mafuta kwenye engine za magari. Kemikali ambayo ilikua inatumika hapo awali ijulikana kwa jina la "Tetraethyl lead" kutoka katika familia ya kemikali za "#Organometallic" ilikua ikitumika katika mafuta ya #Petroli ambayo husaidia injini za magari zisinoki #Antiknocking "Knocking" .

🔸Sifa za kikemikali za kampaundi hiyo ambayo hugawanyika pale joto linapofika ⚠200 °C na kutengeneza kampaundi nyingine ya "Lead oxide" ambayo huzuia mlipuko (#combustion) wa mafuta ya petroli ndani ya injini ambayo huweza pelekea injini ikanoki.

🔸Kutokana na madhara yasabishwayo na #Lead "Madini ya risasi" , taasisi mbali mbali za kimataifa zimekua zikipiga marufuku matumizi ya kemikali hii kuanzia miaka ya #1970 katika nchi ya Marekani na baadae duniani kote.

🔸Sheria rasmi ya kupinga matumizi ya kemikali hii katika mafuta ya #Petroli ilipitishwa mwaka #1991 ambapo kampuni yoyote ile ya mafuta itakayotumia kemikali hii itatozwa faini isiyopungua $10, 000/- zaidi ya milioni 20 za kitanzania. 🌟

Hiyo ndio sababu katika sheli za mafuta ⛽⛽⛽ utakuta petroli imeandikwa #UNLEADED ikimaanisha haina #lead 🌟Kemikali mmbadala ambayo hutumika kwenye mafuta ya #Petroli ni pamoja na #MTBE "Methyl tert butylether". Kemikali hii haina madhara kwa mazingira na viumbehai ukilinganisha na hiyo ambayo imepigwa marufuku.
 
Leaded petrol means petrol containing lead, which should be avoided as they get emitted in to the air and causes harmful effects on plants, humans n animals too. While unleaded petrol means petrol without lead, which is used now-a-days
 
Leaded petrol means petrol containing lead, which should be avoided as they get emitted in to the air and causes harmful effects on plants, humans n animals too. While unleaded petrol means petrol without lead, which is used now-a-days
Asante, kwanini sasa waweke hio lead wakati wanajua ina madhara kwa mazingira?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante,Hio leaded ilitengenezwa kwa sababu zipi hasa, kulikuwa na ulazima gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante,Hio leaded ilitengenezwa kwa sababu zipi hasa,kulikuwa na ulazima gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Lead iliwekwa ili kuongeza ufanisi kwenye engine za petrol kwa kuongeza octane number , na kuongeza ufanisi kwenye engine, na quiet operation za engine kwa kuwa pia ilikuwa inapunguza knocking effect.

Kwa magari ya kisasa combustion process imeboreshwa sana ,ndi maana hata unleaded fuel Ina perform vizuri, tu Ila Yale ya zamani vavle mbili carburetor na point distributor , unleaded fuel ilikuwa ni mateso

Sent
 
Na 91 95 98 ?

Naona za hiyo station zinasoma 80s
 
Na 91 95 98 ?

Naona za hiyo station zinasoma 80s
Sina uhakika sana Ila nadhani ni octane number , lakini pia miaka ya karibuni kumekuwa na additives zingine kwenye petrol ambazo inadaiwa ni salama kwa mazingira,

Sent
 
Asante kwa hio kwa wenye magari ya kisasa una uamuzi wa kuweka yoyote tu kati ya leaded na unleaded sio?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…