Nini tofauti ya muundo wa Jiji la Mwanza na Jiji la Dar?

Hakuna Manispaa ya Nyamagana bali kuna Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza lenye mipaka ya iliyokuwa Manispaa ya Nyamagana ambayo ilifutwa.
Mji wa Mwanza haujawahi kuwa na Manispaa ya Nyamagana. Kulikuwa na Halmashauri ya manispaa ya Mwanza ambayo baadaye ilipandishwa hadhi na kuwa Halmashauri ya jiji la Mwanza baada ya mji wa Mwanza kuwa jiji. Mji huu baadaye ulikuja kugawanywa na kuwa na wilaya mbili - Nyamagana na Ilemela.Baadaye Halmashauri ya manispaa ya Ilemela ilianzishwa kuhudumia wilaya ya Ilemela ndani ya jiji la Mwanza. Halmashauri ya jiji la Mwanza ilibaki pale pale na kwa jina hilo hilo isipokuwa kiutawala ilibakiza eneo la wilaya ya Nyamagana baada ya wilaya ya Ilemela kuwa na halmashauri yake ya manispaa. Na muda si mrefu kama ambavyo rais ameahidi, wilaya ya tatu itaanzishwa ndani ya jiji la Mwanza eneo la Igoma ambayo nayo itakuwa na halmashauri ya manispaa.

Halmashauri ya manispaa ya Ilemela kiutawala haiko chini ya Halmashauri ya jiji la Mwanza bali zote ziko chini ya mkuu wa mkoa wa Mwanza ambaye ndiye kiunganishi wa halmashauri zote zilizomo kwenye mkoa wa Mwanza - yaani pamoja na halmashauri za wilaya na miji kama Sengerema, Kwimba, Magu na Misungwi.

Hicho ndicho kilichofanyika kwenye jiji la Dar es Salaam. Na hicho ndicho rais anataka kwa majiji mengine yatakayokuwa makubwa kiasi kwamba halmashauri moja haitatosheleza kusimamia maendeleo yake. Kilichofanyika ni kupunguza beurocracy isiyokuwa na tija ya kuwa na hamashauri moja inayojiita ya jiji kusimamia halmashauri zingine ndani ya jiji la Dar es Salaam. Kaivunja hiyo halmashauri inayosimamia halmashauri nyenzake!
 
Duh! Asante sana,nimeelewa leo aisee
 
Huwa tunasema mwenye macho haambiwi tazama, nahodha kasema ya moyoni jinsi alivyowavusha.
Ule haukuwa uchaguzi, ilikuwa ni tamthilia ya uchaguzi
Nahodha huwa hapendi kubaki na dukuduku yeye huweka mambo hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…