Nini tofauti

fizo talent

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
2,255
Reaction score
3,889
Habari wana jamvi,nahitaji kufahamu tofauti ya Mtume na Nabii na namna walivyotenda kazi ktk ulimwengu
 
Habari wana jamvi,nahitaji kufahamu tofauti ya Mtume na Nabii na namna walivyotenda kazi ktk ulimwengu
Nabii ni mjumbe aliyetumwa na Allaah Aliyetukuka bila kuteremshiwa sheria au kanuni mpya ilhali Rasuul ni yule aliyeteremshiwa sheria mpya. Hivyo, Nabii hutumia sheria ya Mtume aliyemtangulia.
Kwa ufupi ni kuwa kila Mtume ni Nabii lakini si kila Nabii ni Mtume. Mtume ana daraja kubwa kuliko Nabii.
Na Allaah Anajua zaidi

Mitume ni wale ambao Mwenyezi Mungu aliwatuma kwa umma mbalimbali ili kuwaelekeza njia yake na kuwaepusha na njia za upotofu za Ibilisi na Shetani .
Kumbe Manabii ni wale walioletewa ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili wawafahamishe watu wao kuhusu ujumbe wake.
 
Umeeleweka
 
Unaweza kunipa mfano hai wa mtume na nabii kwa majina
 
Unaweza kunipa mfano hai wa mtume na nabii kwa majina
Mitume wakubwa wa Qurani ambao walipewa mitihani mingi wakawa na subira kustahimili matatizo ya umma zao. Hawa ni:
1. Nuhu
2. Ibrahimu
3. Musa
4. Isa
5. Muhammad.

Baadhi ya majina ya manabii waliotajwa katika Qurani ni pamoja na:
1. Adam ( Adamu ) ( ﺁﺩﻡ )
2. Idris au Idrisa ( Henoko ) (ﺇﺩﺭﻳﺲ )
3. Nuh ( Nuhu ) ( ﻧﻮﺡ)
4. Hud ( ﻫﻮﺩ)
5. Saleh au Salih (ﺻﺎﻟﺢ )
6. Ibrahim au Ibrahimu (Abrahamu ) (ﺇﺑﺮﺍﻫﻴﻢ )
7. Luut (Lut ) ( ﻟﻮﻁ)
8. Ismail au Ismaili (Ishmaeli ) (ﺇﺳﻤﺎﻋﻴﻞ )
9. Ishaq au Isihaka ( Isaka ) (ﺇﺳﺤﺎﻕ )
10. Ya'qub au Yakubu ( Yakobo Israeli ) (ﻳﻌﻘﻮﺏ )

Baadhi ya majina ya manabii waliotajwa katika Biblia ni:
1. Nabii –Ibrahimu (Mwa 20:7).
2. Nabii –Haruni (Aroni) (Kut 7:1).
3. Nabii –Musa (Kumb 18:15; 34:10).
4. Nabii –Samweli (1Sam 3:20).
5. Nabii –Gadi (1Sam 22:5).
6. Nabii –Nathani (2Sam 7:2).
7. Nabii –Ahiya (1Fal 11:29).
8. Nabii –Yehu (1Fal 16:7).
9. Nabii –Eliya (1Fal 18:22). Nabii si mwandishi.
10. Nabii –Elisha (1Fal 19:16; 2Fal 5:8; 2Fal 6:12).

Haya ni majina ya mitume waliotajwa kwenye Biblia ni:
1. Simoni Petro
2. Andrea
3. Yakobo Mkubwa
4. Yohane
5. Filipo
6. Bartholomayo
7. Tomaso
8. Mathayo
9. Yakobo Mdogo
10. Simoni Mkananayo
11. Yuda Tadei
12. Yuda Iskarioti. Baada ya kifo chake, nafasi yake ilishikwa na Mathiya
 
Unavyoelewa ww haijalishi upande
Nabii ni mjumbe aliyetumwa na Allaah Aliyetukuka bila kuteremshiwa sheria au kanuni mpya, yaani hutumia sheria za aliemtangulia. Mfano
Nabii Suleiman
Nabii Zakariyya
Nabii Saleh

Rasuul ni mjumbe aliyetumwa na Allaah Aliyetukuka ambapo hutumia sheria mpya alizoteremshiwa na Allah. Ambazo ndio huwa uongofu kwa umma wake. Mfano
Rasulullah Mussa
Rasulullah Issa
Rasulullah Muhammad

NB
Rasul waweza kumuita Nabii lakini sio kila Nabii ni Rasul.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…