Hivi unachosema kina ukweli? Miradi mingi ilianzishwa na Watanzania wenyewe kuliko na wakoloni! Nyerere aliposema tujitegemee alijua kuwa mojawapo ya mambo magumu ni kujifunza kuachana na kuwategemea wakoloni. Kwa kadiri tulivyopata wataalamu wetu wenyewe ndivyo vivyo hivyo wataalamu wa kigeni walivyozidi kupungua.
Tunaviangalia vitu kutoka katika pembe tofauti hapa. Mnaangalia vitu kwa sababu vilianzishwa. Mimi naangalia kuanzishwa na kuendelezwa.
Hapana, mimi kwa upande wangu wangu naangalia kuwa vitu vilianzishwa na vikaendelezwa ni hadi baadaye sana ndipo wengine wakavivunja. Si umesikia suala la shamba la mpunga la Mbarali? Kuna mifano mingi kweli. Sasa hawa wasipoendeleza leo tumlaumu Nyerere kwa kuanzisha na kuendeleza hadi alipofikia wakati anatoka?
Nyerere alifanya kiile ambacho aliweza kufanya, ni jukumu la waliompokea Nyerere kuendeleza "mema" na kuyaacha mabaya. Tatizo ni kuwa wao hata yale mema wameyatupa. Tatizo ni kuwa wewe unataka tumlaumu Nyerere kwa hawa kuivunja misingi ya taifa letu. Ni lini utaanza kuwawajibisha hawa waliochukua madaraka miaka 25 sasa tangu Nyerere aachie Urais? ama tusubiri miaka 50 baadaye ndiyo tuanze kufikiria labda tunawajibika na vitendo vyetu wenyewe?
Hivi wahisani wakikata misaada si tutarudi kwenye maisha ya pre-colonial 😕
Hii ndiyo point yangu, wakisitisha misaada labda tutaanza kutumia ubongo wetu!