Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Wakati mpaka leo hii nikiwa sipati logic ya mgombea kupata udhamini wa chama cha siasa,kinachonishangaza zaidi ni hili swala la mgombea urais kutakiwa kutafuta wadhamini wa kumdhamini kugombea uraisi wa nchi hiii.
Utaratibu huu bila shaka tumeuiga kutoka katika mataifa mengine duniani maana sisi ni watu wa kuiga tu na kubuni vyetu huwa ni mthani.
Sasa najiuliza ni nini umuhimu wa wadhamini hawa?
Kwa maneno mengine,wadhamini hawa wana wajibu gani kwa mgombea au ni nini kitaharibika iwapo mgombea atakuwa hana wadhamini?
Hili zoezi la kutafuta wadhamini sio tu linaingiza wagombea na vyama vyao katika gharama kubwa,bali pia linachosha wagombea ambao bado wanajukumu la kuzunguka nchi nzima kufanya kampeni.
Hivi ukishakuwa Raisi,wadhamini wana lipi tena kwa mtu ambae ameshakuwa ni Raisi wa nchi?
Na hata wanaojitokeza kumdhamini mgombea uraisi,wanajua wajibu wao kwa mgombea?
Na je,si wajibu wa Tume ya Uchaguzi kuelimisha wananchi ili waelewa wanapomdhani mgombea wa uraisi maana yake huwa ni nini hasa?
Na kama swala la wadhamini ni la muhimu,ni kwanini mgombea asipitishwe na Tume kwanza alafu ndio atakiwe kutafuta wadhamini kama shariti la kukamilisha sifa za kuwa mgombea ili kutowaingiza wagombea na vyama vyao gharama alafu baadae unakuja kuenguliwa.
Na hizi gharama wanazoingia sio chanzo kimojawapo cha baadhi ya watu kutumia vibaya madaraka yao ili warudishe gharama wanazoingia katika kusaka uraisi?
Yaani waliotunga hii sheria/utaratibu huu hawakuona kuna tatizo kwa mgombea na chama chake kuingia gharama huku akiwa na uwezekano wa kuja kuenguliwa na Tume ya Uchaguzi?
Alafu ni lazima mgombea azunguke physically nchi nzima kutafuta wadhami katika dunia hii ya leo yenye teknolojia inayoweza kurahisha jambo hili kama ni la lazima sana?
Duniani kote huu ndio utaratibu?
Na kama dunia nzima hali ndio iko hivyo,sisi hatuwezi kuwa wa kwanza kufanya kitu cha tofauti mpaka mambo yote yaanzie Ulaya na Marekani?
Mwenye hoja na si vihoja tunamuomba atusaidie/atuelimishe.