Kama habari inavyojieleza mimi ni muhanga wa mmba wa kichwani ingawa napunguza nywele kila wiki,napenda kufahamu chanzo cha mmba kichwani na nini tiba yake kwani nimeshajaribu shampoo,sabuni za asili na hata dawa za hospitalini za kumeza na kupaka ila bado tatizo liko palepale,naombeni kwa anayefahamu zaidi anijuze na iwe pia faida kwa wengine.
Natanguliza shukrani