Ninja amewapa somo wanadharau vipaji vya watu

Ninja amewapa somo wanadharau vipaji vya watu

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Aliyekuwa beki wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' jana alifanyiwa vipimo vya afya kunako klabu ya LA Galaxy inayoshiriki ligi kuu ya Marekani

Ninja alifuzu vipimo hivyo na ameanza rasmi mazoezi katika klabu hiyo iliyosheheni nyota waliowahi kutamba barani Ulaya

Wakati yuko nchini, Ninja hakuwa akipewa heshima anayostahili kwa kuonekana ni mchezaji wa kawaida sana

Wako waliombeza kuwa hakuwa beki bora aliyepaswa kuwemo kwenye kikosi cha Yanga

Lakini usajili wake kwenda LA Galaxy ni somo kwa wale wanaodharau vipaji vya wachezaji wazawa

Ninja ametua Galaxy sio kwa muujiza, bali ameweza kuwashawishi mabosi wa timu hiyo yenye nyota kama kina Zlatan Ibrahimovic

Huyu Ninja ametoka Yanga na moja kwa moja kwenda LA Galaxy, kiwango chake alichoonyesha kwenye klabu ya Yanga ndicho kilichombeba

Kupitia video zake akiwa Yanga, wazungu wamemkubali na kuamua kumsajili tena bila hata ya kumfanyia majaribio! kitu ambacho ni nadra sana kwa wachezaji kutoka nchi zetu hizi za dunia ya tatu

Winga Mrisho Ngasa aliwahi kupata nafasi ya kwenda huko Marekani lakini licha ya ubora aliokuwa nao wakati huo, alifanyiwa majaribio ambayo hata hivyo hakufanikiwa

Wakati mwingine wadau wa soka hapa Tanzania huwa tunadhani tunaufahamu sana mpira, lakini kiuhalisia hatujui kitu

Imekuwa bahati mbaya hata maamuzi mengi yanayofanywa kuanzia ngazi ya vilabu mpaka timu ya Taifa, hutokana na msukumo wa mashabiki ambao wengi wetu tunadhani tunaujua sana mpira

Screenshot_2019-08-14-19-25-24.jpeg
 
Aisew hongera zaje Ninja shaibu ninja kwa kutusua aisee yaani akikomaa uyu ni billionaire wa kesho
 
Jamaa alikuwa beki mzuri sana, kuanzia umbo na uchezaji ila kutokana na njaa walizokuwa nao Yanga walishindwa kujua nyekundu na nyeupe.
 
Huu ndio UKWELI.... mtoa mada amezidisha chumvi... Na hapo Marekani amepelekwa LA GALAXY II.... ambayo ni sawa na kusema Timu ya vijana...
Mbona alikuwa Czech daraja la 3 katolewa mkopo LGalaxy B
 
😀
Huu ndio UKWELI.... mtoa mada amezidisha chumvi... Na hapo Marekani amepelekwa LA GALAXY II.... ambayo ni sawa na kusema Timu ya vijana...
Bado huoni kuwa haya ni mafanikio ! wonders will never end ! Ulitaka aende Qatar! Dogo ametoka,ashindwe yeye tu ! Ni aibu kwa Yanga kumwache kizembe ! Sawa na Simba Kwa Kotei na Zaina Koulbally😀
 
Back
Top Bottom