Mbalamwezi, Crown ziko za versions 14 kuanzia zilipoanza kutengenezwa mwaka 1955. Crown nyingi tunazotumia hivi sasa ni version/kizazi cha 12 (12th Generation) ambazo zimetengenezwa kuanzia mwaka 2003-2008. Ukubwa/uwezo wa Engine unaanzia 2490 (4GR), 2990 (3GR), 3490 (2GR) na 4290 (V8).
Mark X ni mwendelezo wa Mark II na ilikuja kuibadili Verossa ambayo haikufanya vizuri kwenye soko. Mark X ina Engine zenye ukubwa/uwezo kuanzia 2490 (GRX120), 2990 (GRX125) na 3490 (GRX130).
Average consumption ya mafuta ni 8.6 -10km kwa lita moja kutegemea na mazingira (mjini kwenye mijifoleni au nje ya mji/kusiko na mafoleni makubwa), uendeshaji na uzima wa gari kwa ujumla (engine, aina ya tairi, kiasi cha upepo kwenye tairi, wheel balance na alignment).
Ukitaka kuendesha kama Michael Schumacher ndipo utajua kama inabwia au inamwaga mafuta.
Gari zote mbili zina comfortability ya hali ya juu.
Kwa kigezo cha nafasi crown ni spacious zaidi. Chukua crown kutegemea na injini utakayoipenda. The Higher the CC the better the performance.