Ninunue lori ya kichina 0 KM au Scania used from Saab Scania

Ninunue lori ya kichina 0 KM au Scania used from Saab Scania

Kwa ushauri wangu napendekeza chukua gari za China (HOWO or FAW) . Hii ni kwa sababu ya matumizi ya mafuta yapo chini na pia kwa kuwa ni mapya ulaji wa mafuta utakuwa chini zaidi kwa miaka miwili ya mwanzo. Mafuta ndiyo prime component kwenye fleet industry .

Pili spare parts zinapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu. Tatu pamoja na kuwa life span ya gari za kichina ni fupi ila ukizingatia service vizuri unaweza fika nalo hata miaka saba. Na kwa kuwa ni gari unanua jipya hatugemei upaate breakdown za mara kwa mara. Tofauti na ukinunua hizo scania used.Kwa hili pia itakupunguzia gharama za uendeshaji.

Tatu kwa kuwa una uhakika wa mizigo basi jitahidi uwe unapata na mizigo ya kurudi , hasa huko Congo(Kolwezi, Likasi, Lubumbashi ) mara nyingi mzigo wa kurudi ni copper . Hapo utatengeza faida vizuri. Na umesema umepata agent basi hakikisha ni mwaminifu kazi nyingi zenye madalali zinakuwa na ubabaishaji sana. Ninaposema ubabaishaji namaanisha malipo na pia inakuwa ni kazi yenye chain kubwa. Kwa gari zako sita kwa upande wangu naona kama umeanza vizuri na ni vyema ukatengeneza network na kampuni kubwa zinaingiza mizigo ambazo reliable , achana na madali.
Shukrani kiongozi
 
Chinese truck wazee wa dabo clutch, wazee wa rough road anapopita Mchina mswedeni apiti thus Dump truck nyingi ni Mchina contract ikiisha unauza gari.
Long safari, comfortability, long lasting, kuuzika Mswedeni yupo vizuri.
So unashauri nini kiongozi...
 
Kwakuwa biashara ni ya uhakika (nadhani ni contract) ni vema ukaanza na magari mapya yenye uhakika kwa safari hizo ndefu.
Pamoja na kwamba ni mpya, naamini spea haziko bei juu kwakuwa wazalishaji wameshajua tumenunua sana magari yao hivyo spea ziatakuwepo nyingi tu na za bei nafuu.
Ninasistiza gari mpya kwakuwa routes zako ni za masafa marefu, routes hizo hazitaki gari za kubahatisha. Hata hivo vyuma vya pale subscania siyo vya mchezo likini siyo reliable kwakuwa ni used. P360 nimeona ASAS anazitumia sana kwa matenki ya mafuta, unaweza kupata uzoefu live.

Mwisho wa siku kwakuwa unaanza biashara na umeshapata a b c za kila upande wa vyuma, chukua Howo/Faw 4, kisha Scania 2 ili upate fufsa nzuri ya kuyasoma yote kwakuwa umesema biashara ni ya muendelezo (kuitanua zaid)

NB kuna Benzi Actress to SA nimeona baadhi ya makampuni kama TBL na Coca-Cola wanazitumia japo sina uzoefu nazo.

Kila la kheri!! Huwa nipo mitaa fulan nitaziona zikianza kazi, nipe alama!
Nitakupa code mwamba..
 
haiwezi kuwa150Mil mzee ni zaid XT-P series ni gari mzee af c inajua P series ndo scania ndogo that's means kwa hio bei barabaran zingekuwa nyingi nishawah uliza kwa watu wanasema hip gari inaweza karibia 300mil
Hata mie najua hivo! Ila nataka nisikie kutoka kwake inawezekana anafahamu kitu. Maana R410 hadi R450 model za 2016 now zinasimamia million 120 hadi 135 kutokana na condition.

Pia pale Saab Scania ni wapigaji tu
1] Scania R440 iliua servo clutch master kupiga simu Saab Scania wanataka million 15 ila ikapatikana pale Tabata kwa million 2.5 tu na hadi leo ni miez 7 gari inapiga kazi bila kusumbua.

2] Nilinunua engine oil Saab Scania ila wakat wa kubadilisha Oil nyeusi na haina kiwango kufatilia dumu kwa chini limechomwa kuonyesha kuwa waliijaza kwa chini.
 
Chukua kitu 0 km ya Mchina, miaka 4 stress free,
Gari used ni used tu, haina uhakika wakati wowote unapigiwa simu na dereva , halafu spea za Scania bei ziko juu .
Pesa utayookoa ya utofauti wa bei ya kununua kwa idadi hiyo ya magari uliosema unapata gari nyingine mpya hapo..
Inabidi upige hesabu vizuri sana ili.uweze kujustfy idea zako,
Biashara ya lori haiwezi.kuwa stress free hata siku moja , ndo maana inatakiwa ifanywe na watu ambao wanavumilia magumu.
Siamini sana gari ya kichina over mtumba , ila nafahamu zote hizo mbili zikiamua kukuchachafya lazima ulale na viatu.
 
kutokana na experience chukua mchina fanyia kazi
Scania na euro truck zipo comfortable na zinaishi miaka mingi Ila inatkiwa uwe unaliudumia vizuri vinginevyo 4 month utalipaki
Mchina utaenda nae sawa Ila maisha yake c marefu na hazipo comfortable

ukilinganisha scania 124l yenye horse power 420 na howo yenye HP 371 utagindua scania ina fuel consumption kubwa kuliko howo

Miguu ya gari hizi moja euro truck ni standard sana kama ni mtumba basi uwe wa south Africa Ila ukichukua wa ulaya itakuzingua niamini mm upande wa pili Chinese truck miguu yake haiwezi kuabsorb shock zinazotokana na roughness ya barabara so madeva wanalalamika usalama wa afya zao lakn miguu ya howo chaka lolote inatoboa

life span ya engine na power magari ya kizungu yapo fresh ukilinganisha na mchina na ikumbuke in case engine ya shackman,howo,faw au dong feng zikizingua unanua mpya maana ukiifanyia overall inazingua tena

spare parts za howo ni cheap sana kuliko scania na euro truck na zipo nyingi
ushauri kama unanunua scania iwe ya south Africa isiwe single yaan iwe double differential (diff) lakin
kwangu mm Chinese kwa Africa wapo fresh kibiashara Ila muonekano na comfort ni zero
Umefafanua vzr mno mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
mtumba wa ulaya kiafrica unafel broo trust me Ila hao wanaojiita sub-scania nao ni wapigaji sana kk scania ukiinunua ya ulaya basi uipe trailer ambayo kazi zake c ngumu mfano trailer iwe petroleum tank af iwe inakanyaga rami tu mzee ili ikupe unafuu katka gharama za matengenezo
Ila Mbona MO ana mitumba kibao ya Ulaya?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
watu wengi ni kama tunachanganya mambo ukiona logistic company inaagiza scania ujue they have already reach economic prosperity hata ukichunguza hizo kampuni utagundua wana gari pia za kichina sijawaona world oil tu na prime fuel Ila kampuni zingine wamechanganya wana mzungu na mchina huwez fika Kongo bila break down na scania ya mtumba
Kachumbari ya magari haitakiwi hasa kwa mazingira yetu ya bongo ambapo kupata spare part original au best aftermarket ni mtihani,
Lakini tatizo kubwa kwa wasafirishaji wa Tanzania ni kuwa hawajui jinsi ya kuspecify gari kutokana na kazi walizo nazo mkononi, Naona mtoa mada pia anastruggle na tatizo hilo, kazi aliyonayo mkononi ni Congo migodini, kule kunahitaji gari heavy duty, yenye retarder , sio lazima iwe double diff , a tag unit with high range hub reduction diff ipo vizuri na ni nyepesi kuliko double diff .p 360 kama unaipeleka kolwezi basi angalau iwe ya south Africa , sio Uk.
Tatizo pia lipo kwa wanaouza hayo magari , hapa naongelea saab scania, wao gari mpya zao zipo well speced kwa mazingira yetu, ila mitumba wanaleta pusher trucks (mid lift), pusher trucks by default ni gari za kazi laini laini, ukishaanza kuipeleka kolwezi R450 pusher , unachezea pesa yako tu maana gharama lazima ziwe juu, kuanzia brake maintanace hadi drive train.
 
Habari natumaini wakongwe mko vizuri


Nina mpango wa kuanzisha kampuni ya usafirishaji nikiwa na mpango wa kusafirisha mizigo kutoka nchini kwenda nchi jirani kwa maana DRC, Zambia, Burundi, Rwanda n.k
(Transit)

Katika kuuliza uliza nimekutana na mawazo makuu mawili ambayo yamekuwa yakinipa mawazo nikaona ni vyema niilete kwenu kwa majadiliano wakongwe

WAZO LA KWANZA

Wazo la kwanza ni kuchukua lori 0 Km kutoka kwa wachina aidha Howo au Faw

WAZO LA PILI

Wazo la pili ni kichukua scania used kutoka saab scania ambapo pale naweza kupata P360 iliyosimama

Trip ni kusafirisha makontena kuelekea maeneo kama vile Congo Kolwezi, Likasi, Lubumbash, Kasumbalesa, Lusaka, Rwanda, Burudi na Malawi

Hivyo basi nataka kujua gari sahihi ambalo wakongwe mtanishauri ninunue kutokana na aina ya safari zangu hizo

Tayari Agent yupo ambaye uhakika wa kutupa tenda za kusafirisha ni uhakika

Kwa kuanza tuna mpango wa kuanza na magari sita (06) lakini upo uwezekano wa kununua mpaka kumi na mbili (12)

UTAFITI WANGU WA AWALI

Gharama za mchina na Scania hazitofautiani sana mathalan kwa mfano ukienda kwa Dr Howo pale kurasini gari N7 na tella lake ambazo ni 0 Km ni $81,000 wakati saab scania used p 360 ni Tsh 150M , ukichukua na tella la superdol na bima na kila kitu ni kama 250M ambayo ni $106,000

MANUNUZI

Mchina:Truck and trailer (both brand new) $81,000
Scania : Used and trailer (brand new) $106,000

MAFUTA

Kwa upande wa mafuta wachina kwenye mafuta wako vizuri kwa maana trip ambayo scania atatumia lita 1900 mchina anaweza kutumia lita 1700 hiyo lita 200 unakuwa umeokoa ambayo ni takribani laki sita (600,000)

Kwa maana mchina gharama za ununuzi ziko chini, uendeshaji ziko chini ila hazidumu sana kwa maana baada ya miaka yako mitano gari kwisha kazi

Ila scania gharama za ununuzi ziko juu, uendeshaji, iko juu ila zinadumu hadi miaka saba hadi nane..

Naileta hii mada kwenu kwamba je niingie kwa mchina au niingie kwa msweeden?

WHY SAAB SCANIA NA SIO KUAGIZA SCANIA KUTOKA UINGEREZA


Watu wamenishauri kuagiza scania gharama haitofautiani iwapo ukaenda kununua saab scania lakini haina guarantee unaweza agiza gari kutoka UK used limetembea km 400,000 ukaanza safari kufika chalinze tu ngoma imesizi, hapo uneshapokea mzigo wa mtu ni lazima ufanye engine overhaul na mambo mengine mengi

Hapo unakuta unapoteza mpaka 9 M kwa engine na fundi etc

Lakini pia kwa upande wa kichina ni kwamba madereva wazuri wanazikimbia sababu ya aina ya magari kiafya sio rafiki kwao hivyo ukiwa na scania kama p360 ni rahisi kupata madereva wazuri kwani talent pool ya madereva wanaotaka kuendesha hizo p360 ni kubwa pia

Hivyo basi naomba kuuliza kwa gari 6 mpaka 12, agent tayari kashakuwa spotted anaweza kutupa kazi trip ni za kwenda Congo Kolwezi, Likasi, Lubumbash, Kasumbalesa, Lusaka, Rwanda, Burudi na Malawi je nishukue mchina au niingie kwa m sweeden naomba kujua sana sana technical know hows za hizi chuma mbili

Maana kuna watu wanashauri kuwa ni bora mchina na wengine wanashauri ni bora m sweeden used

Tayari eneo ambalo nitalifanya kama yard nimesha li spot ambapo ni Kibaha kwa mathias itakapokuwa makao makuu na main yard ya chuma kwa maana agent akikamilisha kila kitu chuma zinaamsha toka kibaha kwenda bandarini kupakia kisha kuamsha...

Natanguliza shukrani

C.T.UView attachment 2566531View attachment 2566532
Just PM 0672273736
 
Mkuu nimsoma koment zote za wanna na hakika walio changia hapa Ni wazoefu mno

Namm niseme chukua hyo fao au howo kwa Kaz zako hzo ili kuepuka usumbufu fln kutoka kwa scania used

Howo na faw sinaweza shoruba Sana Mara chache sana kuikuta imezongua njiania Ni back to back tu baada ya miaka kadhaa uza faster agiza lingine

Nawaheshimu Sana scania kwa durability na uwezo ila kazi za shoruba atasubiri Sana

Nilikuwa manager wa jamaa mmoja mwenye scani 4 hz za 114 mende hzo katk Kaz za mchanga na kifusi ndipo nilipo gundua kuwa faw na howo Ni hbar nyingine kwa Kaz za shoruba
Mwisho
Naomba ajira kwenye kampuni yako hyo utakavyo fungua Nina uzoefu wa fleet usiotiliwa mashaka Ni najuwa Bei za spare na jinsi ya kupata kwa Bei ya mteremko

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom