Ninunue lori ya kichina 0 KM au Scania used from Saab Scania

Shukrani kiongozi
 
Chinese truck wazee wa dabo clutch, wazee wa rough road anapopita Mchina mswedeni apiti thus Dump truck nyingi ni Mchina contract ikiisha unauza gari.
Long safari, comfortability, long lasting, kuuzika Mswedeni yupo vizuri.
So unashauri nini kiongozi...
 
Nitakupa code mwamba..
 
haiwezi kuwa150Mil mzee ni zaid XT-P series ni gari mzee af c inajua P series ndo scania ndogo that's means kwa hio bei barabaran zingekuwa nyingi nishawah uliza kwa watu wanasema hip gari inaweza karibia 300mil
Hata mie najua hivo! Ila nataka nisikie kutoka kwake inawezekana anafahamu kitu. Maana R410 hadi R450 model za 2016 now zinasimamia million 120 hadi 135 kutokana na condition.

Pia pale Saab Scania ni wapigaji tu
1] Scania R440 iliua servo clutch master kupiga simu Saab Scania wanataka million 15 ila ikapatikana pale Tabata kwa million 2.5 tu na hadi leo ni miez 7 gari inapiga kazi bila kusumbua.

2] Nilinunua engine oil Saab Scania ila wakat wa kubadilisha Oil nyeusi na haina kiwango kufatilia dumu kwa chini limechomwa kuonyesha kuwa waliijaza kwa chini.
 
Inabidi upige hesabu vizuri sana ili.uweze kujustfy idea zako,
Biashara ya lori haiwezi.kuwa stress free hata siku moja , ndo maana inatakiwa ifanywe na watu ambao wanavumilia magumu.
Siamini sana gari ya kichina over mtumba , ila nafahamu zote hizo mbili zikiamua kukuchachafya lazima ulale na viatu.
 
Umefafanua vzr mno mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ila Mbona MO ana mitumba kibao ya Ulaya?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kachumbari ya magari haitakiwi hasa kwa mazingira yetu ya bongo ambapo kupata spare part original au best aftermarket ni mtihani,
Lakini tatizo kubwa kwa wasafirishaji wa Tanzania ni kuwa hawajui jinsi ya kuspecify gari kutokana na kazi walizo nazo mkononi, Naona mtoa mada pia anastruggle na tatizo hilo, kazi aliyonayo mkononi ni Congo migodini, kule kunahitaji gari heavy duty, yenye retarder , sio lazima iwe double diff , a tag unit with high range hub reduction diff ipo vizuri na ni nyepesi kuliko double diff .p 360 kama unaipeleka kolwezi basi angalau iwe ya south Africa , sio Uk.
Tatizo pia lipo kwa wanaouza hayo magari , hapa naongelea saab scania, wao gari mpya zao zipo well speced kwa mazingira yetu, ila mitumba wanaleta pusher trucks (mid lift), pusher trucks by default ni gari za kazi laini laini, ukishaanza kuipeleka kolwezi R450 pusher , unachezea pesa yako tu maana gharama lazima ziwe juu, kuanzia brake maintanace hadi drive train.
 
Just PM 0672273736
 
Mkuu nimsoma koment zote za wanna na hakika walio changia hapa Ni wazoefu mno

Namm niseme chukua hyo fao au howo kwa Kaz zako hzo ili kuepuka usumbufu fln kutoka kwa scania used

Howo na faw sinaweza shoruba Sana Mara chache sana kuikuta imezongua njiania Ni back to back tu baada ya miaka kadhaa uza faster agiza lingine

Nawaheshimu Sana scania kwa durability na uwezo ila kazi za shoruba atasubiri Sana

Nilikuwa manager wa jamaa mmoja mwenye scani 4 hz za 114 mende hzo katk Kaz za mchanga na kifusi ndipo nilipo gundua kuwa faw na howo Ni hbar nyingine kwa Kaz za shoruba
Mwisho
Naomba ajira kwenye kampuni yako hyo utakavyo fungua Nina uzoefu wa fleet usiotiliwa mashaka Ni najuwa Bei za spare na jinsi ya kupata kwa Bei ya mteremko

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…