Ninunue lori ya kichina 0 KM au Scania used from Saab Scania

Mkuu una hakika P360 pale Saab Scania ni million 150 tu? Inakuwa ya mwaka gani? Ni hizi XT?
Xt , ni karibu dola 150000 if my memmory serves me right., unaongelea mil 300 na ushee , xt inakuja hapa kwetu ikiwa ni euro 3 compliant
Huyu anaongelea used euro 5 na 6 pusher za Uk ,ndo zina range ya 150 mil, na ndo hizo usipokuwa makini lazima ulale mlango wazi.
 
Hata mkeo akiamua ni stress tupu mkuu
 
Why buying from Scania? UK kuna Scania kibao Bei ya kutupa

?
Kwa mtu mwenye kazi ngumu kama hizo za migodini , likasi ,kolwezi na kadhalika , kununua scania ya Uk ni kujitafutia matatizo tu.
Uingereza ni visiwa , hawana safari ndefu na wala hawana kazi ngumu, wanapoagiza brand new kiwandani huwa hawaspecify truck to the best of both worlds. Ni gharama ku equip truck with extras , wao wanafanya basics kutokana na matumizi yao, ngumu sana kupata truck ina retarder ukinunua uk.
Kwa mtumba wa scania kwa ajilinya kazi ngumu nunua south afrika kama.pesa ipo , au nunua mtumba wa denmark , germany sweden nertheland au spain hizi zinakuwaga Lhd.
 
Scania, ni rahisi sana ku recover all your money au zaidi ukitaka kuuza... Na sababu nyingine nyingi, basi tu nina uvivu wa kuandika
Chukuwa scania mkuu utaleta mrejesho hapa parts zake zipo rundo na zina mafundi wazoefu sana, pia nakupa ujanja mara ununuapo gari za kichina badili sit ya dereva ndiyo inayoumiza kwa kweli.
 
Mkuu ushauri wangu kwa structure ya kazi zako na huko unakokwenda , nakushauri gari ya kichina,
Sipendi gari ya kichina na kupata madereva ni ngumu sana kwa sasa , kwa sababu as they become popular nowadays watu wanafahamu mengi kuhusu hizo gari , kiukweli sio rafiki wa afya kwa dereva , na zinachosha sana, yes zinatumia.mafuta vizuri lakini zikiwa mpya tu, zikichoka zipo vibaya ,
Kwa nini sikushauri scania japo naipenda sana , !!, sababu nimeona unafocus kwenye mtumba wa Uk, kama unaweza nenda botswana ,namibia au south africa huko utapata scania za kwenda nazo kolwezi.
R450 mtumba wa uk inakuja na diff yenye ration 2.92, hii ni diff ya mbio sio kupanda milima , R460 ya south ni euro 3 na inakuja na diff yenye ratio 3.08.hii ni diff ya milima sio.mbio, ndio maana ukiilazimisha r450 ya mtumbaipande milima kwa uwezo wa engine lazima utaoverhaul engine mapema
 
Wachina wajanja sana sit wamefanya isimpe furaha dereva hata kidogo ili awe makini infacts sit za howo hazikupi comfort!
Hata ubadilishe seat , bado hakuna comfort, structure nzima ya ile cabin pamoja na suspension ya pale mbele , hakuna namna inaweza kuwa comfortable.
Cabin insulation pia ni poor kwenye gari za kichina , hii inamuumiza sana dereva kama atalala.kwenye sehemu zenye baridi , ni kama unalala kwenye hema tu.
 
Mbona GSM ameyajaza mengi na yote yako mtaani au madereva wanaendeshea shida?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Nunua 0km mkuu, in 3 years liuze na hela yako itakuwa imerudi na faida.
 
Nilikua nautafuta uzi wa kula tunda kimasikhara nikajikuta nimetokea huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…