Ninunue lori ya kichina 0 KM au Scania used from Saab Scania

Mleta mada Leo umenifurahisha Sana kwa Uzi huu
Kwanza umenikumbusha mbali mno
Niliishi kwenye fleet na kuipenda hyo Kaz Sana

Ili fika mahali milio ya Malory ya kuchina na ya kizungu ubongo ukazoe hata nikiwa mbali nikisikia lorry linanguruma nitajuw. Tu Ni howo au scania r420 -480

Safi Sana ukinunua tafdhali tupe mrejesho

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Km mzunguko wa biashara ni mzuri chukua mchina kwanza for at least 2yrs then anza kuchanganya na scania ilimchina akianza choka scania anakubeba mzigo unakua na kitu kinaitwa business continuity
Bonge moja la comment.. shukrani sana mdau
 
Kwa hiyo kiongozi katika hili naomba ushauri wa best truck na best trailer..
 
Nimefurahi kusikia kuhusu mpango wako wa kuanzisha kampuni ya usafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani kama DRC, Zambia, Burundi, Rwanda, na kadhalika. Kwa upande wa gari, nashauri kuwa ununue Scania badala ya Howo au Faw, kwa sababu kwa mujibu wa utafiti wako wa awali, Scania inadumu kwa miaka saba hadi nane wakati Howo inadumu kwa miaka mitano tu. Ingawa gharama ya ununuzi wa Scania ni kubwa, inaweza kuokoa gharama ya mafuta, ambayo ni karibu Tsh 600,000 ($200), kutokana na ufanisi wake wa matumizi ya mafuta.

Kwa kuwa umeshaelezea kuwa una mpango wa kuanza na magari sita hadi kumi na mbili, ni vizuri kuchagua gari ambalo linaweza kudumu kwa muda mrefu na kuwa na dereva mzuri. Kwa upande wa yard yako, kuna mambo kadhaa ya kuzingatia, kama vile nafasi ya kutosha, upatikanaji wa huduma za ujenzi, na kadhalika. Kwa ujumla, nashauri uwe makini na uzingatie gharama na ufanisi wa gari, na uangalie pia upatikanaji wa huduma za matengenezo na vipuri kwa gari unalotaka kununua. Mafanikio mema katika biashara yako ya usafirishaji!
 
Chukuwa scania mkuu utaleta mrejesho hapa parts zake zipo rundo na zina mafundi wazoefu sana, pia nakupa ujanja mara ununuapo gari za kichina badili sit ya dereva ndiyo inayoumiza kwa kweli.
Wanasema hizi howo N7 siti zimeboreshwa ila ngoja nitafuatilia zaodi
 
Shukrani sana Mkuu kwa hiyo ni focus sana sana na euro 3 si ndio eeeh
 
Kwa sababu wewe ni mgeni wa biashara.

Kaa kwenye zero km.

Fuel Consumption itakubeba.

Spare parts nazo haitakugharimu sana

Mengine utajifunzia ukiwa field
Shukrani sana kamanda
 
Kwa hiyo kiongozi katika hili naomba ushauri wa best truck na best trailer..
Best trailer tafuta double tires on air suspension , preferably with bendix or wabco Abs system
Best truck kwa nature ya huko unakotaka kwenda tafuta gari ya kichina ambazo kwa kawaida ni 6x4, kama mfuko unaruhusu zama south kachukue R460 duoble diff mtumba wa south au namibia , hii unaweza kuja nishukuru baadaye , ni very best option kwa kazi na barabara zetu.
Kwa kazi zako kama ulivyoelezea mwanzo , kaa mbali sana na gari za mtumba wa uingereza , hasa euro 5 na 6.
 
Shukrani sana Mkuu kwa hiyo ni focus sana sana na euro 3 si ndio eeeh
Tafuta Euro 3 ! Kwa kuwa mafuta tunayotumia bado yana sulpbur content kubwa , Trucks za euro 5 na6 zinatumia ultra low sulphur diesel, huku hatuna hiyo , ndio sababu cha kwanza huwa zinazingua sensors ni nyingi na ukishawekandiesel yetu matatizo yanaanza , wich is the reason why hata ukiwa na pwaa yako scania Tanzania hawezi kukuagizia gari mpya yoyote ya euro 6, maana anajua hataweza kukupa warranty na litakusumbua .
kuna option kama mbili tatu,
1 ,brand new kutoka vingunguti
2 mtumba kutoka scandinavians, huko hawa kurush kwenye emmission control.kama Uk.
3 .mtumba kutoka south africa , namibia ,botswana au brazil .
 
Najaribu kuchambua comment.

Kuna maswala ya msingi sana technically kuna swala la diff ratio kwenye scania... nimeona zipo R450 ya UK ina diff ya 2.92 ambayo mdau kasema inaweza mbio na si heavy duty haipandi milima mikali HAIFAI. Ushauri wake kwa kuzingatia target ya route zako ni R460 ya S.A yenye diff ratio ya 3.08 inanguvu ya kupanda milima ila haina mbio na hii ndio itafaa uendako.

Kwa mchina Howo nimeona Imekuwa recommended kutokana na uhimilivu wake na configaration ya 6 by 4 yaani ni double diff pia fuel consumption iko vizuri [hapa navyo kumbuka huwa ku formula ya fuel consumption Hii inatofautiana gari na gari (Total Km (one way) x 0.3 empty plus Total Km (one way) x 0.5 loaded)x fuel price... kujua gharama za mafuta. HOWO inachangamoto za cabin suspension system na inner body design haitoi starehe kwa dereva wa long route. Pia life span yake ni 5years haina engine rebuild kit (overhaul) pia haiuziki kirahisi ikiwa used.

HOWO straingth ni 0 km, low maintanance cost, low fuel consumption, low buying price, cheap spare, easy spare availability and technicians (mafundi wapo)

Why Scania and not Scania...
Used Most is above 400,000km, high buying price, kodi kubwa, inategea hali ya hewa ya nchi ilikokusudiwa, inachagua barabara, spare ni aghali, fuel consumption is high ukilinganisha na HOWO, haina uhakika wa uzima wake baada ya kuinunua, ukiilazisha ni rahisi kuharibika, service ni aghali, wauzaji wake hawaaminiki kwenye taarifa za gari...kuna kupigwa!

Straingth ni imara ukibahatisha, inadumu muda mrefu, suspension system yake is superb very confortable , madereva wanaipenda, ukipata ya S.A R460 Euro3 yenye diff ratio ya 3.08 unauhakika wa kupasua milima

Matatizo ya kibiashara na uendeshaji, kuna utapeli kwa madalali, wizi wa mizigo hasa Congo, ubovu wa barabara Congo, kodi za gari, upandaji wa bei ya mafuta na vipuri, uaminifu kwa madereva na ujuzi wao wa kazi, ajali, changamoto za urejeshaji wa mkopo (ikiwa ulikopa) uharaka na uhakika wa upatikanaji wa mizigo.

Faida na hasara
Ni biashara yenye 50% risk
Ukipata mizigo kwa bei nzuri bila changamoto inalipa haraka sana. Na hasara ni haraka mfano kuungua kwa gari na mzigo, ajari kubwa, bima na nk

Hitimisho; chambua maoni fanya maamuzi.
 
KUlima ni Rukwa mzee, Ruvuma kanunue vitalu vya makaa ya mawe ndo habari ya mjini.
cheza bingo hiyo ukibutua ni mpunga wa kula hadi unaiaga dunia .ukifeli unalima mahindi.
Nipe ABC mzee..ni kule Kitai?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…