Nioe mke mwingine?

Pole sana Bw. Mulama!

Kwa hakika inauma sana hasa pale unapokumbuka mlikotoka mkiwa MME na MKE wa kweli lakini leo ndiyo hivyo tena. Kisa hiki kimenigusa sana kwani hata mie wife yuko nje kwa masomo na kwa bahati mbaya sana nimekwisha ona dalili za kukosa mwelekeo wa maisha tuliyokuwa tunategemea kuwa nayo siku za usoni - amebadilika sana kitabia hasa katika maisha ya NDOA takatifu, nipo home najipanga kuyakabili vilivyo haya yaliyokukuta ................................................ Pole sana mwombe Mungu akusaidie ili uisikate tamaa na nina hakika ya kuwa ataadhibiwa mkiwa hapa hapa duniani.
 

Nakushukuru kwa maoni yako. Kuhusu kuongea na kujadili na kushauriana vyote vilishafanyika bila mafanikio, hata mkielewana muda akishaenda kazini akirudi amebadilika kama sio yeye mliyekubaliana hapo kabla!

Hilo la id na avatar za uongo nakubaliana nawewe kwamba ndivyo ilivyo kwenye jf.
Ebu nipe maharifa eti wanawake wote wako hivyo siku hizi kwa sababu ya ulimbukeni wa kushika fedha na kumiliki mali eti wanasema masikini akipata m........ ulia mbwata eti!?

Inawezekana kuwa kweli kwamba mwanamke hakuumbwa kuwa tajiri ispokuwa utajiri wake ni mwanaume? na kwamba hili ndio tatizo wanakosa kujitawala kifikira kwa kujiona sasa nawao ni wanaume!
 
Mtaji unao huo mwili wako, we lialia ndani tu shauri yako, body hilo mali adimu.... ushaelewa vibaya hahahaha unaweza kuwa bauncer wa macelebrity au night club lol acha kulalama ingia mtaani mulama

Duh Shantel!
Mbona umennipa mtihani mzito?! kuwa baunsa si inabidi ubebe kwanza vyuma kwenye jim za kulipia?! na pia lishe iwepo ya uhakika!.
Huu mwili niliopewa na mola bila kuufanyia mazoezi kweli utaweza kumlinda huyo celebrity uliyemsema?. Kwanza anaishi wapi huyo celebrity niende kujaribu kumuomba kazi ya ulinzi nione kama atanikubalia?
 
anakupaga naniiiii...... au nayo kabana ? kama hakupi oa kesho mchango wangi milioni moja nipe acc, namber yako. pole lakini inauma....
 
Pole sana kaka, kiukweli kama jitihada zimeshindikana hakuna budi kujivua gamba maana utapoteza muda wako mwingi na magonjwa ni mengi siku hizi. Binafsi yalinikuta kwa kweli nilikuwa nimepoteza muda wangu mwingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…