Mulama,
Kama ndoa yako ya miaka 11 ni halali na kama hii hoja umeileta ikiwa ni wewe mwenyewe muathirika basi nakushauri usikurupuke kuoa mwanamke mwingine...
Kuoa TENA hakujawahi kuwa ni suluhisho la matatizo ya ndoa duniani kote - Mke wa pili huwa ni MBAYA zaidi kuliko Mke wa kwanza, na watatu ni mbaya zaidi kuliko wa pili, e.t.c.
Kutokana na post yako inaonekana mkeo wa kwanza mlishaachana (kwa uzuri au kwa ubaya), equally na mkeo wako huyu "msumbufu" alikwisha achika (kwa uzuri au kwa ubaya) and that tells me that nyote ni "broken-heart" kwa kuwa mahusiano yenu ya kwanza YALISHINDWA KUSIMAMA.. Kwa mantiki hiyo basi, inawezekana sana hata hiyo miaka 11 imekuwa ni ya "kubahatisha" zaidi na ndiyo maana wewe binafsi umeshindwa kuongeza hata elimu kiasi cha kutosha na mkeo pia haujamsomesha kiasi cha kutosha..
Administrative Secretary (post form IV) siyo "investment" ki-elimu bado angaweza kuwa kwenye nafasi kubwa zaidi kama kumsomesha kwako na mahusiano yenu ya ndoa yangekuwa IMARA toka mwanzo.. Na wewe pia kama ungekuwa hauna "element" ya "Utegezemezi aka Mario" kwa miaka kumi na moja ungekuwa una japo Diploma na au umejiajiri mwenyewe e.t.c
Kwahiyo I would boldly say, Ndoa yenu haijajengwa kwenye msingi imara, na, kwa maana hiyo basi inabidi NYOTE wawili mrudi kwenye "drawing board" na muanze upya kutengeneza ndoa yenu, of which naamini kwa msaada wa Wazazi, Ndugu, na Viongozi wa Imani za kiroho mnaweza kuanza upya maisha mema ya ndoa yenye heri na baraka... Ikishindikana, basi, ni vyema, kila mmoja akachukua mkondo wake mpya wa maisha na ku-MOVE ON kwa maana kuwa you two were not meant for each other...
Jioni Njema - Nawahi Bia za Baridi pale Baracuda kabla Tanesco hawajakata umeme!