Nioe mke mwingine?

Nioe mke mwingine?

Mmh! Pole sana jamani... Tafuta kibarua usonge mbele, maisha yenyewe mafupi haya kwanini mnyimane raha!
Kwa kipindi hiki inabidi uwe mvumilivu hata kama unanyanyaswa usiruhusu hali ya huzuni ikutawale.
Kuhusu mtoto kubaki st kayumba mwingne internetional lisikuumize. Hao watoto wote ni wenu, inawezekana mkeo hana uwezo wa kuwasomesha wote international ila na wewe ushaanza kuweka tabaka kwamba mmoja katengwa.
Mmmh! Hzi ndoa mbona zinatutisha!
 
Huyo mkeo limbukeni tuu, anaona kishafika. Pole sana mkuu, fadhila mfadhili mbuzi utakula nyama yake, siyo binadamu...
 
...Mimi naona ni bora kukazania kutafuta
kazi kwanza na kuimarisha maisha ya
Mwanao na yako pia ..
Kwa jinsi inavyo onekana jamaa akipata kazi yenye mshiko mzuri, mke atarejesha heshima kama zamani.

Pole sana mkuu. Kama umeongea na wazee wa ukoo na wameshindwa kutoa maamuzi ya kuboresha ndoa yako na mkeo, nakushauri waone tena wazazi wako na wazazi wa mkeo, pia washirikie viongozi wa dini yenu.

Waeleze kile kinacho kukera na nini maoni yako na wampe nafasi ya mkeo kujieleza, baada ya hapo nina uhakika muafaka utapatikana tu.
 
Ahasanteni sana kwa michango yenu mizuri, pia na wale ambao hawakunielewa nawashukuru sana kwakuwa nao wamewakilisha mawazo yao vizuri tu. Hakika nimeona umuhimu wa kujiunga na jf, naomba nitoea ufafanuzi wa ujumla kama ifuatavyo;
Wakati namsomesha ilikuwa ni kwa makubaliano kama mke na mume na kama ujuavyo maagizo yanasema mnakuwa mwili mmoja, hivyo sikuona taabu kwa yeye ambaye amenizidi darasa kidogo japokuwa division ilikuwa ni IV ya point 28 niliona badala ya mimi kwenda qt bora nimjengee uwezo yeye kwani ni kitu kimoja.
Sina pesa kwa sasa kwakuwa wakati nafanya kazi nilikuwa nawekeza kwenye masomo yake, nimekwishamshauri anipe mtaji wa biashara lakini ananiambia mimi sikusoma hesabu za kibiashara nitazijuaje!
Ubaguzi kwa mtoto wangu unakuwa dhairi sasa kiasi kwamba mtoto ameanza kuuliza kama huyu ni mamake mzazi au kuna mwingine ( mamake alishafariki) hii inanipa shida kwakuwa muda wote sikuzaa naye kwa kile alichokuwa anadai mimba hazishiki, japokuwa hivi karibuni katoa mimba akidai yuko busy hawezi kupata muda wa kulea mtoto kwa sasa!
Ninaposema nafikiria kuoa manake ni kuachana kabisa na huyu na kuanza upya, kama nimempa elimu anayoringia na kuninyanyasa nayo kwa sasa, kwani mimi siwezi kupata mwanamke mwenye upendo wa kweli nami akaniinua kimaisha au ni dhambi mwanamke kumuinua mwanaume?
Kiukweli ni visa vingi naweza kujaza kitabu
 
very interesting.. nimepata somo fulani hivi

btw; pole sana mkuu
 
Kwa jinsi inavyo onekana jamaa akipata kazi yenye mshiko mzuri, mke atarejesha heshima kama zamani.

Pole sana mkuu. Kama umeongea na wazee wa ukoo na wameshindwa kutoa maamuzi ya kuboresha ndoa yako na mkeo, nakushauri waone tena wazazi wako na wazazi wa mkeo, pia washirikie viongozi wa dini yenu.

Waeleze kile kinacho kukera na nini maoni yako na wampe nafasi ya mkeo kujieleza, baada ya hapo nina uhakika muafaka utapatikana tu.

Ahsante mkuu kwa ushauri huu, ila haya yote yalishafanyika bila kuleta jibu muafaka. Unajua suala la ndoa ni zito sana ukiona mtu analileta hapa barazani ujue kaelemewa kwa njia zingine zote.
 
tatizo ni moja tu: ukiwa msituni huoni msitu unaona miti tu! wanaume wazuri na wema wanapata wake vimeo,na wanawake wazuri na wema wanapata wanaume vimeo++. pole kaka,Mungu akutangulie ktk kusaka suluhisho.muhimu tafuta kazi pia, hata mwanamke akiwa tegemezi hujisikia unyonge pia,ni hali ya kibinadamu. usisahau kufanya mpango ujikwamue kiuchumi na kielimu pia kwa ajili ya baadae.
 
mie hata sijaelewa hapo, yaani wewe stdvii mke anaform iv, badala kusoma wewe umemsomesha yeye!!!ona sasa yanayokusibu, alishakukalia tangu mwanzo huyo, pole sana, na ukioa mwingi kama hautakuwa makini utaliwa tena.
 
hukukosea kumsomesha,ulifanya wajibu wako kama mume,kitu kinachokufanya kuwa mume na baba bora.endelea kuwatia moyo watoto wenu wote kuwa ktkk maisha kuna mapito mbalimbali ambayo Mungu anaturuhusu kupitia ili tujengeke kihekima na kiimani pia. hata kama unaamua kumuacha usifanye hivyo kwa kukimbilia mahuiano mengine. chukua muda kupumzisha nafsi yako na kujiimarisha kiuchumi.usikubali kumuachia akufanye ujiskie w ni duni,la hasha. uanaume wako haupimwi kwa fedha wala elimu,ni kwa jinsi unavyoweza kuhimili na kukabili vikwazo vya kimaisha.
Sina pesa kwa sasa kwakuwa wakati nafanya kazi nilikuwa nawekeza kwenye masomo yake, nimekwishamshauri anipe mtaji wa biashara lakini ananiambia mimi sikusoma hesabu za kibiashara nitazijuaje! Ubaguzi kwa mtoto wangu unakuwa dhairi sasa kiasi kwamba mtoto ameanza kuuliza kama huyu ni mamake mzazi au kuna mwingine ( mamake alishafariki) hii inanipa shida kwakuwa muda wote sikuzaa naye kwa kile alichokuwa anadai mimba hazishiki, japokuwa hivi karibuni katoa mimba akidai yuko busy hawezi kupata muda wa kulea mtoto kwa sasa! Ninaposema nafikiria kuoa manake ni kuachana kabisa na huyu na kuanza upya, kama nimempa elimu anayoringia na kuninyanyasa nayo kwa sasa, kwani mimi siwezi kupata mwanamke mwenye upendo wa kweli nami akaniinua kimaisha au ni dhambi mwanamke kumuinua mwanaume? Kiukweli ni visa vingi naweza kujaza kitabu
 
mie hata sijaelewa hapo, yaani wewe stdvii mke anaform iv, badala kusoma wewe umemsomesha yeye!!!ona sasa yanayokusibu, alishakukalia tangu mwanzo huyo, pole sana, na ukioa mwingi kama hautakuwa makini utaliwa tena.

Katika kupenda kuna kupenda kwa dhati na kuna kupenda kwa kupitisha siku, sema hapa tatizo ni kwamba nilipenda kwa dhati na kuubwaga moyo wangu kabisa kwake nikijua nayeye yuko hivyohivyo kwangu!
Hapa ukisema alinikalia tangu mwanzo au ni kwa ajili ya mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwake sijui kwakweli!
 
Kwa jinsi inavyo onekana jamaa akipata kazi yenye mshiko mzuri, mke atarejesha heshima kama zamani.

Pole sana mkuu. Kama umeongea na wazee wa ukoo na wameshindwa kutoa maamuzi ya kuboresha ndoa yako na mkeo, nakushauri waone tena wazazi wako na wazazi wa mkeo, pia washirikie viongozi wa dini yenu.

Waeleze kile kinacho kukera na nini maoni yako na wampe nafasi ya mkeo kujieleza, baada ya hapo nina uhakika muafaka utapatikana tu.

kweli kabisa XP
lakini ni bora apate kazi kwanza
halafu baada ya hapo mie naona acheze mbele.
haina haja ya mtu mzima kuka na kuendelea
kuumizwa kiasi hicho..... kwa maelezo yaelekea
huyo dada hampendi yeye anampenda akiwa na
kitu tu basi...

Kilichoniuma zaidi ni cha mtoto..
kweli kabisa kuna ambao hawana huruma
miaka 11 bado ubaguzi wa kipuuzi hivyo..
XP mie naona bora jamaa apate kazi, amchukue
mwanae na maisha yaendelee..
 
Pole sana Mulama, mi nakusisitiza usikimbilie kumuacha mkeo,naomba utafute kazi au namna ya kujiendeleza. Ni rahisi sana watu kumuona huyo mwanamke mbaya lakini nikuhakikishie wanawake wengi hawatakuwa tofauti na huyo mama. Kama baba wa familia jitahidi nawe uingize kipato hata kama ni kidogo na pia kwenda kazini itakupunguzia stress unazopata sasa,atleast kule uta interact na watu,utakuwa na marafiki ambao kwa namna moja au nyingine watakuwa msaada kwako hata kama ni wa kisaikolojia. Nakutakia kila la kheri.
 
hukukosea kumsomesha,ulifanya wajibu wako kama mume,kitu kinachokufanya kuwa mume na baba bora.endelea kuwatia moyo watoto wenu wote kuwa ktkk maisha kuna mapito mbalimbali ambayo Mungu anaturuhusu kupitia ili tujengeke kihekima na kiimani pia. hata kama unaamua kumuacha usifanye hivyo kwa kukimbilia mahuiano mengine. chukua muda kupumzisha nafsi yako na kujiimarisha kiuchumi.usikubali kumuachia akufanye ujiskie w ni duni,la hasha. uanaume wako haupimwi kwa fedha wala elimu,ni kwa jinsi unavyoweza kuhimili na kukabili vikwazo vya kimaisha.

Ahsante sana kwa mchango wako na ushauri wako mzuri, lakini suala la kukimbilia uhusiano mwingine huoni kama ni muhimu kwa kipindi hiki kwakuwa niko desperate na wakati huo yeye ana good time, think of mimi ndio nafanya kila kitu nyumbani (house boy) yeye anarudi muda anaotaka. Kwa sasa mtotot wake yuko boarding mimi wa kwangu yupo tunaishi naye nisipohangaika hali ni kweli niendelee kuvumilia? ya chumbani naogopa kusema nisijemvunjia heshima hapa mbele za watu.
 
sijaelewa uhusiano kati ya ww kutafuta mwanamke mwingine na kujitahidi. ina maana utatafuta mwanamke a kukutunza ama wa kukupenda na kukuheshimu kama mume? ukiwa desperate unaweza kujikuta unaingia kwenye matatizo makubwa kuliko uliyonanyo sasa. muhimu ni kuweka nguvu katika kutafuta kibarua uweze kujikimu wakati unachukua muda kutafuta suluhisho la matatizo yenu. ni ngumu hasa ka mwanamke, lakini unaweza kuja kugundua baadae kuwa ulikuwa unajisikia mnyonge zaidi kwa sababu ya hali inayokukabili kwa sasa. tatua kwanza la kifedha,manake inaonekana bibie anaponzeka na mapito. wakati huu ongea nae,jaribu kumkumbusha kwa upole juu ya mlipotoka na mnapoelekea sasa. pole ndugu,naamini utavuka tu,Mungu sio king'asti
Ahsante sana kwa mchango wako na ushauri wako mzuri, lakini suala la kukimbilia uhusiano mwingine huoni kama ni muhimu kwa kipindi hiki kwakuwa niko desperate na wakati huo yeye ana good time, think of mimi ndio nafanya kila kitu nyumbani (house boy) yeye anarudi muda anaotaka. Kwa sasa mtotot wake yuko boarding mimi wa kwangu yupo tunaishi naye nisipohangaika hali ni kweli niendelee kuvumilia? ya chumbani naogopa kusema nisijemvunjia heshima hapa mbele za watu.
 
Pole sana mpendwa.
Nakuomba usikimbilie kuoa mke mwingine kwa sasa tulia utafute kazi ujipange upya ndo uanze kumtafute mke mwingine wa kuoa taratibutaratibu na kuwa makini sana wakati wakuchagua mke wa kuoa usije ukaoa matatizo mengine tena
 
Kwanza kabisa pole sana Mkuu;
Pili Akufukuzae akwambii Toka....;
Tatu Tafuta kazi na ikifika hii hatua usichague kazi, kazi ni kazi bora mkono uende kinywani, tafuta kazi hama hapo tengeneza maisha yako na ya mtoto wako sababu mateso sasa si yako pekee bali na mwanao
 
Back
Top Bottom