niokoe ndugu yako!

Danstan Jr.

Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
7
Reaction score
0
habari za sasa wana jf wenzangu naomba nipate mawazo yenu ama msaada kwa haya majanga.Mimi ni kijana wa kiume,miaka 19 nina tatizo la kujamba sana tena kila wakati,shida zaid ni kwamba huwa si kwa hiari yangu ila nakuta tayari ishatoka bila mimi kufahamu wala kuruhusu.Tatilo hili lilinipata mwishoni mwa 2011 mara baada tu ya kurejea shuleni toka likizo ndefu,niligundua hasa baada ya kuona wenzangu wakikreka na kubana pua mara kwa mara,nikapata hisia kuwa ni mimi?nilipochunguza nilijua kuwa ni mimi na ndipo nilipoanza kujitenga na wenzangu kwa kutohudhuria vipind tena,kutoshiriki ibada na shugul yoyote yenye mkusanyiko wa watu kwa hofu ya kuchekwa na kuwa kituko mbele za wengine,hali ilyosababisha kutofanya vizur katika masomo yangu kwa kuwa muda mwingi nilgubikwa na huzun,mawazo na upweke. Nimejaribu kufanya tiba mbalimbali na kukutana na madaktar weng sana na hata maombi lakin vyote havjazaa matunda yoyote kwa afya yangu,tests kadhaa nimefanya ila bado!!naomba msaad wenu tafdhali!pamoja
 
Tiba ni rahisi sana kijana. Watu wenye matatizo kama yako inatakiwa mfanye kitu kimoja tu. Amka asubuhi alafu ufunge kama tunavyofunga sisi waislam mwezi wa ramadhan.

Ikifika jioni kula vyakula vyote. Ukiona hali haipo mchana anza kuruhusu vyakula vya aina moja tu mchana. Unaweza kuanza kwa kula ugali na mboga za majani tu mchana. Kama hali itakujia badilisha ugali labda kula ndizi. Ni aina ya chakula tu unachokula basi.

Pia ukienda haja kubwa jikamue hadi mwisho.

Alafu ukienda kwa wafamasia ukawaeleza tatizo lako watakupa dawa wao huwa wanafanya vitu simple na kwa mazoea kuliko madaktari na mala nyingi huwa inakuwa fine kwa matatizo madogomadogo.
 

athante ndugu,ntajaribu
 
je tumbo lina vimba yani unakuwa na gesi?
Je ushuzi unanuka sana?
Je ukila chakula ndo unaanza kujamba?
Kama ni baada ya kula je ni vyakula vya aina gani?
Je tumbo linauma?
Je unapata allergy kama macho kuwasha maskio kuwasha ngozi kuwasha?
 
je tumbo lina vimba yani unakuwa na gesi?
Je ushuzi unanuka sana?
Je ukila chakula ndo unaanza kujamba?
Kama ni baada ya kula je ni vyakula vya aina gani?
Je tumbo linauma?
Je unapata allergy kama macho kuwasha maskio kuwasha ngozi kuwasha?

tumbo mara zote huwa lina gesi nyingi sana,muda mwingne harufu ni mbaya sana,msaada
 
tumbo mara zote huwa lina gesi nyingi sana,muda mwingne harufu ni mbaya sana,msaada
Pole sana Tatizo lako la kujamba linatokana na tumbo lako kujaa gesi inawezekana wewe pia una matatizo ya ukosefu wakutopata choo kikubwa kwa njia ya urahisi fanya hivi.

Kila unapo amka Asubuhi kabla ya kula kitu chochote kunywa maji ya Uvuguvugu glasi 2 kisha nenda kapige mswaki

ukimaliza kupiga mswaki kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi 1 kisha kaa baada ya saa 1 kupita kunywa chai au chakula

cha asabuhi. kisha mchana kabla ya kula kitu kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi 2 kisha kaa baada ya saa moja kula

chakula cha mchana. Kisha usiku kabla ya kula kitu kunywa tena maji ya uvuguvugu glasi 1 kisha baada ya saa 1 kupita kula chakula

cha usiku. Na wakati wa kwenda kulala kunywa tena glasi 1 ya maji ya uvuguvugu kisha lala usingizi. Fanya hivyo kila siku

kwa muda wa siku 7 kisha uje hapa utupe feedback.
 
hapana sipat maumivu ya tumbo ila nakuwa na hali ya kutaka kutoa kila saa

mmh unashindwa kujielezea vizuri
but mara nyingi watu wenye tatizo kama lako huwa na overgrowth ya fungus wanaoitwa candida albicanas kwenye utumbo mkubwa (colon)

sabab ya hyo overgrowth ni pamoja na
kuishi maisha ya stress
kutumia dawa antibiotic (broad specrum) bila mpango na hivyo kuua bacteria wazuri (normal flora) wa tumboni ambao hu keep in chek na hao yeast/fangus (candinda albicanas)
nk

kwahyo basi maelezo ni marefu nakufupishia tu

kuna antifugal drugs mfano ketoconazole tablets 200g

ushauri ni miwili either ueende hospital kubwa mfano ya mkoa uwambie wakupime kimpimo cha damu kuchek yeast overgrowth au kipimo cha choo ndo kinatumika sana kuangalia yeast overgrowth

au uende phamarcy ukanunue hizo dawa nilizo kutajia hapo juu
 

nashindwa kuelezea vyote maana ni ving,asante mkuu
 

asante ndugu ntatumia ushauri wako then ntarud jamvini!
 
Duh....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…