Danstan Jr.
Member
- Aug 29, 2013
- 7
- 0
habari za sasa wana jf wenzangu naomba nipate mawazo yenu ama msaada kwa haya majanga.Mimi ni kijana wa kiume,miaka 19 nina tatizo la kujamba sana tena kila wakati,shida zaid ni kwamba huwa si kwa hiari yangu ila nakuta tayari ishatoka bila mimi kufahamu wala kuruhusu.Tatilo hili lilinipata mwishoni mwa 2011 mara baada tu ya kurejea shuleni toka likizo ndefu,niligundua hasa baada ya kuona wenzangu wakikreka na kubana pua mara kwa mara,nikapata hisia kuwa ni mimi?nilipochunguza nilijua kuwa ni mimi na ndipo nilipoanza kujitenga na wenzangu kwa kutohudhuria vipind tena,kutoshiriki ibada na shugul yoyote yenye mkusanyiko wa watu kwa hofu ya kuchekwa na kuwa kituko mbele za wengine,hali ilyosababisha kutofanya vizur katika masomo yangu kwa kuwa muda mwingi nilgubikwa na huzun,mawazo na upweke. Nimejaribu kufanya tiba mbalimbali na kukutana na madaktar weng sana na hata maombi lakin vyote havjazaa matunda yoyote kwa afya yangu,tests kadhaa nimefanya ila bado!!naomba msaad wenu tafdhali!pamoja