Niokoeni jamani nimeanza kumpenda Mzigua90

Niokoeni jamani nimeanza kumpenda Mzigua90

Haya mambo ya thread thread sio ishu, nenda pm mwambie "bibie nna kisalio hapa nataka nikutumie upate lunch , sijui niitume vipi mama" Mzigua90 nae ana moyo lazma moyo utalegea atakupa namba ukifanya muamala itapendeza, hadi hapo mpira upo ndani ya box. Mnakompliketisha mambo
Sasa hii thread itaishia kukupa likes tu
Aisee kumbe sio kazi sana eeh?

Jiandae kunipokea
 
Me siwezi kua na yule kizee
Wanasema ng'ombe hazeki maini we unaelewaje huu usemi

Na msemo wa siku hizi wanasema
Wazee wanalea vijana wabahili sana

Na kuna huu mwingine vuna kwa wazee wekeza kwa vijana

We unaonaje hii misemo
 
Ndondondo si churururu ! Ndivyo ilikuwa nianza kwa kupenda michango yake iliyopevuka iliyosheheni mapenzi ya kweli na nia ya utulivu uso kifani,Taratibu dozi ikaanza kuniingia lahaula la kwata nikajaa nikawa bingwa wa kufuatilia post zake kuliko hata navyofuatilia za mshana jr ,deo msando na gudume .

Najileta kwenu waungwana mninusuru kwani nishaona dalili kuwa mzigua90 ataninyanyasa sana kwani mtizamo wake juu ya mahusiano ni hasi na ni dhahiri ni mtu mtemi asieshaurika, na ukiweka na kauzigua (Tanga ndo yalikozaliwa) mimi mnyalu wa watu najiona nikiuza kiwanja cha urithi.

Nafwaa wajameni.
Mm namkubali sn japo si peke yake nawakubali wengi humu JF ss tatizo alishasema yy wake Ngabu
 
Back
Top Bottom