Niokoleeni watoto wangu tafadhali wanaJF

Niokoleeni watoto wangu tafadhali wanaJF

mabwiku

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
447
Reaction score
390
Habari ndugu zangu,

Kama mada inavyoeleza apo juu,n ikwamba mwenyezi Mungu kanijalia kupata watoto mapacha wawili wa kiume na wa kike.Mpaka sasa wana miezi minne maana walizaliawa na miezi 7 tu,so mpaka sasa wanakaribia kufikisha miezi 5.

Tatizo lililonileta hapa kwenu ni hili. Walivokuwa na miez 2 tuliwanyoa nywele zao kwa mara ya kwanza, mtoto wa kike akaanza kutokewa vipele kichwani tukajua labda ni vipele vya kunyoa make tulinunua nyembe mpya kwa kazi hiyo.Lakini vipele hivyo vikaanza kusambaa mwili mzima na kutoa maji na vingine kama vinatunga usaa lakini vinapasuka vyenyewe.

Tukaenda hospitali tukaambiwa tununue gentosin tube,tulipompaka tu baada ya siku mbili akabadilika ngozi na kuwa mweupe wakati yeye ni maji ya kunde hivi, sasa ikabidi tuache hiyo dawa tukaanza kutumia za majani ya kienyeji.

Tumejaribu kila njia lakini hatujafanikiwa,sasa kwa sasa vimesaambaa kila mahali na ikifika muda akitaka kunyonya anajikuna mpaka anajichubua ngozi yake,nadhani vinamuwasha sana.

Nimekuja kwenu kupata msaada jamani,na kwa bahati mbaya hata huyu pacha wake nae naona vinamtokea vimeanzia mikononi na shingoni.
 
Attachments

  • 11414576_852296258194649_2001165336_n.jpg
    11414576_852296258194649_2001165336_n.jpg
    44 KB · Views: 1,517
  • 11262942_852296198194655_1627039437_n.jpg
    11262942_852296198194655_1627039437_n.jpg
    52 KB · Views: 1,357
  • 11541287_852296288194646_496471287_n.jpg
    11541287_852296288194646_496471287_n.jpg
    53 KB · Views: 1,294
  • f.jpg
    f.jpg
    60 KB · Views: 1,093
Mpeleke kanisani kwenye maombi na pia usichoke kuhangaika nae kutumia dawa mbali mbali
 
Pole sana mkuu, nadhani utapata majibu mazuri kwa matabibu. Usikate tamaa
 
Wiki 3 zilizopita mwanangu wa miezi 9 alianza kutoka vipele vikawa vinatunga usaha kuna jirani yangu akanishauri dawa baada ya siku 3 vikaanza kupotea waone matabibu na pia unaweza kujaribu
 
Attachments

  • 1434654785264.jpg
    1434654785264.jpg
    28.6 KB · Views: 1,093
Mpeleke pale mbagala mission wanaita kwa bruda......ile zahanati ya Roman Catholic wapo vizuri sana. .....jihimu mapema sana siku ya j tatu umpele, nakuhakikishia lazima apone na hawana bei kabisa
 
Pole sana mkuu, nadhani utapata majibu mazuri kwa matabibu. Usikate tamaa

Pole
Inaonekana kama uzio wa ngozi
Nakushauri daktari wa ngozi amwone,nenda muhimbili utapewa hudum
Kutibu ngozi yahitaji uangalifu mkubwa
 
Nenda TMJ kaombe kuonana na daktari wa ngozi,kila wiki huwa ana clinic,ilikuwa ni alhamisi,ila labda wanaweza kuwa wamebadili siku,please nenda hospital kwa uchunguzi zaidi.
 
Kaka pole sana
Nenda pale doctors plaza kuna daktari wa watoto nzuri sana
Anakuwapo jumamosi kuanzia saa 3 tafadhali kaka fanya hvyo
 
pole, Baby yaweza pia kuwa mlichotumia kunyoa nywele au ingewahiwa na dawa iliyokubali asingefika hapo. Pia ni ngozi yake ni mengi huwezi jua.

Yenye Hydrocortisone 1% w/w
kama hydrocortisyl skin cream najua ya 15g tube ni kadogo labda wana kubwa ila haijalishi. Pata ushauru wa DK kwanza.

Wengi utumia kwa sehemu ndogo ndogo kuondoa mkauko au madhara na yanaisha, ila kwa baby naona sasa imesambaa kwa hiyo ni kujaribu kwa ushauri mzuri, hiyo itaje tu ukienda kwa dk wa ngozi pia na ataamua mwenyewe ipi bora akimuona baby. Wapeleke wote.

Najua mtu mtoto wao ilichukua muda hadi alipofika miaka minne kupona na walijaribu kila kitu, iliyomfaa akapona now miaka 10 yupo free kabisa ila wazazi waliangaika kila cream/ dawa inabidi utumie kwa wiki 2/3 kabla ya kubadili ndio utajua inafanya kazi au la.

Ukienda kumuona dk wa ngozi hakikisha haujampaka chochote yaani mafuta. Pia acha kumpaka mafuta sasa ukiweza,

Watapona usiwe na wasi muhimu fata masharti na usichokeeee kabisa, waweza badili dk ykiona miezi inaenda no mabadiliko, kuwa mvumilivu sana.
 
Mpeleke pale mbagala mission wanaita kwa bruda......ile zahanati ya Roman Catholic wapo vizuri sana. .....jihimu mapema sana siku ya j tatu umpele, nakuhakikishia lazima apone na hawana bei kabisa
asante kwa shauri
 
pole, Baby yaweza pia kuwa mlichotumia kunyoa nywele au ingewahiwa na dawa iliyokubali asingefika hapo. Pia ni ngozi yake ni mengi huwezi jua.

Yenye Hydrocortisone 1% w/w
kama hydrocortisyl skin cream najua ya 15g tube ni kadogo labda wana kubwa ila haijalishi. Pata ushauru wa DK kwanza.

Wengi utumia kwa sehemu ndogo ndogo kuondoa mkauko au madhara na yanaisha, ila kwa baby naona sasa imesambaa kwa hiyo ni kujaribu kwa ushauri mzuri, hiyo itaje tu ukienda kwa dk wa ngozi pia na ataamua mwenyewe ipi bora akimuona baby. Wapeleke wote.

Najua mtu mtoto wao ilichukua muda hadi alipofika miaka minne kupona na walijaribu kila kitu, iliyomfaa akapona now miaka 10 yupo free kabisa ila wazazi waliangaika kila cream/ dawa inabidi utumie kwa wiki 2/3 kabla ya kubadili ndio utajua inafanya kazi au la.

Ukienda kumuona dk wa ngozi hakikisha haujampaka chochote yaani mafuta. Pia acha kumpaka mafuta sasa ukiweza,

Watapona usiwe na wasi muhimu fata masharti na usichokeeee kabisa, waweza badili dk ykiona miezi inaenda no mabadiliko, kuwa mvumilivu sana.
asante sana
 
Kaka pole sana
Nenda pale doctors plaza kuna daktari wa watoto nzuri sana
Anakuwapo jumamosi kuanzia saa 3 tafadhali kaka fanya hvyo
nashukuru sana mkuu tatizo nipo mkoani
 
nashukuru sana mkuu tatizo nipo mkoani

Upo mkoa gani? Kuna majani fulani hivi yana tambaa ila yana jani pana sijui jina lake ukipaka hayo ni ndani ya siku mbili tatu tatizo linakwisha. Nipo Dar nitayapiga picha kesho nikutumie kwenye PM. Lkn pia endelea kutafuta ushauri wa madaktari wa hospitali ya karibu.
 
malaika kama hao wasio na dhambi kwanini wanateseka? upo pahala gani labda naweza kukupa msaada ndugu.mimi nipo mombasa next week nakuja tz
 
Yaani watoto wanaugua Magonjwa ya Ngozi halafu awapeleke Kanisani!
We kweli Umetoa wazo la maana.

Teh teh teh teh.

katika mambo yahusuyo mateso ya malaika hao we unaleta mambo za kuchekacheka , shame on you
 
Back
Top Bottom