Niombeeni ndugu zangu, nina ugonjwa wa ajabu

Niombeeni ndugu zangu, nina ugonjwa wa ajabu

Nipo South Africa siku ya tatu hii. Nlikuwa narudi toka China. Nikiwa kwenye ndege First Class nikaenda wash room ndo nikagundua nimetokwa na kipele(pimple) kwenye mkono.

Niliomba nishushwe South Africa wakanifanyie check up na surgery ikiwezekana. Maana naona kama kinaharibu mwonekano wangu.

Ni kikubwa. Kama punje ya ulezi hivi. Actually hakina maumivu wala muwasho. Dr. Has told me (huyu specialist wa magonjwa ya ngozi hapa South Africa) kuwa ni allergy tu.

Nikakumbuka kule China nilikuwa Hotel moja ilikuwa na chakula maalum cha baharini. Ile menu ilikuwa inauzwa kwa bei ya chini kabisa Usd 4,500.

Inawezekana moja ya wale samaki ndiye alinisababishia allergy. Sasa nilimjulisha Mzee. Alinikasirikia sana kuwa naendaje China bila Dr. Wangu. Actually nimekuwa nikijaribu kuishi maisha kama ya watu wengine ila mzee hataki kabisa.

Anataka nikiwa naenda sehemu niende na Dr. Mwanasheria, Secretary, Mpishi na Mhudumu binafsi.

Sometimes naona hii ni kama kujiweka hadharani kuwa nina vijicent jambo ambalo si sawa. Napenda kuishi tu maisha simple. Na amelalamika kuwa why nimeenda kutibiwa South Afrika wakati Madakatari wa familia yetu wapo USA?

Tatizo la Mzee hawaamini kabisa watu wa Africa. Toka siku ambayo aliensa Barber shop moja akawaambia wamnyoe nywele style flani wakakosea kidogo basi hana imani kabisa na professionals wa Afrika.

Sasa huu mgogoro umeanzia last week aliponiuliza Dereva wangu yupo wapi maana aliniona naendesha gari peke yangu kwenda Bagamoyo.nikamwambia anaumwa mafua amelazwa Aga Ghan wanamwangalia kwa ukaribu. Akaniuliza ya wapi nikamwambia ya hapa hapa Dar.

Alifoka sana kuwa inakuaje Dereva anaumwa analazwa Aga Khan Zahanati. Nikamwambia ni Hosp akawa mbogo na kuuliza namlipa tsh ngapi. Kwa kweli Dereva wangu nikiri kuwa namlipa tsh 15,000,000 kwa mwezi. Ila namsomeshea watoto wa ndugu zake wote shule ya International School ya Feza.

Na watoto wake wa 4 namsomeshea IST. Namlipia kodi ya nyumba hapa Oysterbay na kila mwisho wa mwezi namfanyia shopping. Mzee analaumu kuwa nimeanza kuwa mbahili. Kwanza namtibu Dereva Zahanati, pili namlipa kamshahara kadogo so anaweza akawa ananiendesha huku ana mawazo.

Sasa kumwambia natibiwa South Afrika yeye anaamini ni sababu nabana matumizi..kumbe siyo. Napenda niishi maisha simple tu kama watanzania wengine maskini. South Africa si mbaya kwa huduma ya Afya.

Sasa hili la hii chunusi limemtibua kabisa. Anataka nichague kuishi katika nyumba zetu za China, Canada, Sweden, Belgium, USA, Uk, Russia, Germany, Switzerland, Norway, Egypt au South Africa.

Namkatalia sababu hayo majumba ni makubwa sana mtu unaishi kwenye nyumba ambayo Rais wa hizo nchi husika akiwa na mawazo au amechoka anakuja kuomba kwetu akapumzike sehemu za nyumba zetu hizo. Wengi wanadai ni nyumba zaidi ya Ikulu za marais wa nchi hizo.

Maisha hayo ya upweke na kujikuta nimezungukwa tu na wafanyakazi mabint warembo bikra ambao wapo tayari kunipa huduma yoyote nitakayo. Maisha hayo yananishinda. Naona bora nije kujifunza maisha magumu na ya maskini wanaokaa huku Oysterbay.

Mniombee ndugu zangu mzee anielewe. Afahamu hata huku Afrika kuna maisha. Siyo walimvyokosea yeye huko kwa kinyozi basi ndo maisha yote wapo hivyo. Pia mniombee haka kakipele kapone maana naona kananipa mwonekano mbaya. Actually nikivaa shati la mikono mirefu hakaonekani but sijisikii tu comfortable kuwa na pimple.
Leo ndio nimejua Bill Lugano ni mtoto wa @kidukulilo
 
Leo ndio nimejua Bill Lugano ni mtoto wa @kidukulilo
Hapana ni mtu mmoja
Nimekuwa nikipokea malalamiko sana kutoka kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wakisema kuna watu wamekuwa wakiomba Funds kwa ajili ya Taasisi zao kwa kutumia jina langu la Kiduku Lilo.

Kwanza watu wangu walikuwa wanashangaa kuwa nini kimetokea mpaka naomba nichangiwe Usd 50,000 eti za kusaidia watu wenye uelewa hafifu na wenye mtindio wa kiuchumi. Maskini.

Jamaa zangu wengi na mashirika wamekuwa wakituma hizo pesa bila kuuliza. Lakini kuna jamaa yangu alinipigia simu leo akiwa Norway na kuuliza vipi hali yako kiuchumi mpaka unafikia kuomba utumiwe USD 25,000 Umekumbwa na nini? Ndo nikaona isiwe Shida. Kwa sasa Ntatambulika kama Bill Lugano. Hapo nimetumia jina moja la kibantu ambalo nilipewa kama kutunza asili ya Ubantu.

Huwa nawaambia mzazi wangu mmoja ana asili ya Tanzania. Mwingine ni Foreigner. So hapo walinipa majina moja la kizungu la Bill na lingine la Kibantu Lugano.

Karibuni sana wadau. Nipo hapa Hyatt Hotel napunga upepo tu weekend hii. Nikitafakari mambo mbalimbali. Nikichoka naenda zangu kulala, nilishachukua chumba. Waswahili hapo wakichukua chumba ni mpaka wawe na msichana. Si lazima.
 
Mimi ni ile thread yake tu kuhusu nyumba ya mengi yani nilipoisoma may 11 2019 nilicheka balaa .
 
Katika mambo ambayo hutakiwi kuyaletea masihara 1-MARADHI. Tena Kichwa cha Habari ulichokiweka.

Wapo wanaohitaji kuandika hiko kichwa cha Habari na wakiwa kweli ni wahitaji ila wengine wanashindwa kulingana na hali zao.

Kuwa Makini na Masihara na sio kila kifurahisha watu ni Haki yako kukifanya.
 
Back
Top Bottom