Monoko Mushi,
Hizi EPA zimeibiwa lini? je Richmond, IPTL, Rada na Ndege koko na upupu mwingine umeanza lini? Kama tutasema ulianza baada ya Azimio la Zanzibar mwaka 1992, hiyo ni miaka 30 tangu tuwe huru na bado tulikuwa na umasikini.
Ufisadi nna kilichohujumiwa katika Ufisadi ni kiwango kidogo sana na si tiba kwa Umasikini wa Tanzania.
Ukisoma ripoti ya CAG, utaona ni jinsi gani pesa zinatumika vibaya na zinaidhinishwa kibajeti, lakini ni mali bila daftari.
Nimekujibu hapo juu, suala ni Uongozi. Kule kwenye mada ya Azimio na Vijiji vya Ujamaa, conclusion yetu wote ni Uongozi.
Ukiwahoji hawa Viongozi kuhusu utendaji na ufanisi, wakashindwa kujibu na kuonyesha matokeo, ndipo utaanza kujenga mtaji imara wa kisiasa ambao utawezesha kupata kura Bungeni ambazo zitalazimisha kutungwa Sheria na hata kubasilisha Katiba.
Focus yetu ya kuleta maendeleo tumeiwekeza kwenye kulilia tulihujumiwa na Richmond. tumeunda kmati, tumechunguza, lakini hakuna hatua za kisheria au kinidhamu zimechukuliwa. Sawa na suala la EPA, Mzee Balali katutoka, hakuna ambye yuko tayari kumkaba koo aliyekuwa Waziri wa Fedha hata Rais kujua iweje kulikuwa na uzembe na kukosekana kwa ufuatiliaji makini ambao usingetuletea EPA?
Leo hii tunajiuliza, pamoja na kelele zote kuhusu Ufisadi, sijui EPA na upuuzi mwingine, Watu wamejichoeta Bilioni 300 kutoka mabenki ya Tanzania, je hatukujifunza kujenga mfumo bora wa kifedha baada ya EPA?
Jibu lake ni moja, hatuna Uongozi Imara, hatuna Uongozi Makini na hivyo kushinda Umasikini wa Tanzania si vita vya UFISDI pekee, bali ni kuwa na Uongozi Fanisi na Imara unaojua kuchapa kazi na unaowajibika na kuwepo na chombo chenye uwezo wa kuwajibisha!
Mzee wangu Reverand Kishoka nimekuapata,hata hivyo nina kijiswali;
Je utawaambia wananchi tatizo la hao viongozi tusiowataka warudi madarakani ni yapi?
Yes ni kweli utawaambia kuwa hatuna uongozi imara na makini,sasa ni kipi haswa kinachopelekea viongozi hao kutokuwa imara na makini kama si ufisadi?
Hakuna wanachokifanya ambacho hakihusishi maslahi binafsi,that by itself constitutes ufisadi!
Ni lazima tu identify matatizo yaliyoko mbele yetu and what led to them....Najua umezungumzia hapo nyuma na kutolea mifano ya chaguzi mbali mbali walizoshindwa chadema licha ya kuwaeleza wananchi kuhusiana na ufisadi wa Richomd nk,hata hivyo sidhani kama hilo ndilo tatizo ama sababu kwamba hawakuchaguliwa,yani kuwajulisha kuhusu ufisadi,tuendelee kuwaelimisha wananchi kuhusiana na ubovu wa viongozi "Ufisadi" Halafu kama wameeelewa,then tuangalie sasa ni kwanini bado wanaendelea kuwachagua mafisadi hao....Kama ilivyoonekana huko Busanda nk!
Kama ulipitia ile thread yangu yenye kuuliza ni wapi tumekwama,utaona nilitolea mfano wa kauli ya Dr Slaa kuhusiana na mapokeo ya rushwa kwa wananchi kutoka kwa mafisadi hao nyakati za uchaguzi,there binafsi i believe is one of the critical problems
pengine wananchi hawajui kuwa rushwa pia ni ufisadi?
Je na sisi hapa JF kama tusipo udefine ufisadi ipasavyo mwananchi wa kawaida itakuwaje?Ufisadi certainly si EPA na Richomnd pekee,hiyo ni mifano tu,
Ufisadi ndiyo sytle yetu ya uongozi hilo wana JF tulielewe,muda ni mfupi uliobaki,tulitakiwa kwa sasa tuwe tumesha identify sababu na wapi tumekwama na kwa wakati huu, ilitakiwa tuwe tuna angalia ni kwa
namna gani wananchi nao wataelimishwa kuwa hata rushwa ni ufisadi na wala si ishara ya upendo,Unaweza kuona tatizo hata la ku identify kuwa ni wapi tumekwama linatukabili hata sisi wana JF!
Cha muhimu hapa kwa wananchi ni uelewa kuwa hata ubaya una dalili za wema,nilishatoa mfano huko nyuma kwamba tunaweza kuwa in a wrong direction lakini dalili za njiani zitakawa kama ni right directions, hata shetani alimcorrupt mwanadamu kwa kujifanya anampenda na kupelekea mwana wa Adam kulimung'unyua tunda la mti wa kati wa bustani ya Eden!
Ni lazima tuwe na pahala pa kushikilia wakati wa madai yetu ya uhuru mpya!In times of crisis kama tuliyoko,ni lazima tuwe na yale tunayoyashikilia na kuamini kuwa ndio nguzo ya kutunasua! Ukikwama baharini na kama hutaki uzame,ni lazima uwe na mambo kadhaa ya kutilia maanani,kwa mfano ni lazima ufloat,na kama hujui kuogelea,ni lazima uhold on on something that floats....Pia huwezi kutapa tapa na kutaka kushikilia kila kitu! Utazama!
Nilishasema hapo awali kuwa kuna dalili ambazo tunapewa na Mungu lakini tuna zi ignore kwasababu tuna zi missidentify!
Kimsingi ili kuondoka tulipokwama ni lazima tuhold on something that we know it will help us achieving our goal,that is to get out of the current mess!
This time kuwaelimisha wananchi nini haswa maana ya ufisadi na consequences zake,na kabla ya kuwaelimisha wananchi,sisi wenyewe kwanza tuelimishane,halafu kama tukikubaliana kuwa ni wapi tumekwama na and therefore what we should do,then ni lazima tuwe na one voice for sure kwamba this is what we think it will get us through!
Tukipotezana hapo haitajalisha busara na hekima walizonazo wengi wetu humu,tutabaki pale pale and the time tunarealise,its a whole new ball game!