Nipambanaje na wawangaji bila maombi na bila kutumia nguvu za giza??

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2017
Posts
6,097
Reaction score
7,199
Jana sijalala, leo nakesha:

Pazia linapepea kama bendera wakati hali iko tulivu wala hakuna upepo kabisa. Naskia purukushani za popo na mbio za mapanya kwenye 'silingibodi", sio kawaida. Mapaka yanalia nje kwa sauti kama ya watoto na yanaparuzana kwa makucha na kufokeana kwa sauti za ukali. Mlango naskia unagongwa kama mtu anaomba kuingia, nikifungua hamna kitu. Minyato ya mtu kutembea na milio kama ya 'matiti-ndala' (paaapaaa, paaapaaa) yanasikika kama mwanamke mzee ambye hajavaa sindilia anarukaruka ndani kwangu. Jana nlishusha chandarua baada ya muda nikashtuka naumwa na mbu, kumbe chandarua imeshakunjwa. Nikashusha tena, ikapandishwa, kama mara4 hivi. Nikajua lazma wachawi wameingia, nawangiwa. Na leo sipaelewielewi hapa.

Bila kutumia nguvu za giza na maombi, kuna njia zipi (za kiasili labda) zitakazofanya wachawi wasiweze kabisa kuniwangia mimi binafsi wala kusogelea mji wangu. Niweke nini, nivae nini au nifukize vitu gani ili kuwakomoa hawa majamaa. Mimi siamini ktk kujikinga kwa nguvu za giza lkn pia bado sijaiva, sina nguvu ya maombi.

Ushauri wenu wajuzi wa haya mambo

Cc. Mshana jr, Mti Mkavu, Yericko, walozi, wachawi na waaguaji wote JF
 
Kama wewe ni mkristo, sali sala ya baba yetu, tu. Hapo umemaliza kila kitu. Jaribu kusali kwa utulivu hatakama hujaiva hii sala kiboko yao.

Nakushauri pia kama vepee hama mtaa. Inaonekana majirani zako hawakupendi.

Damu ya Yesu ikufunike.
 
Watakuua hao, maana ni wazi kua "hujielewi" unasema huamini katika kujikinga na nguvu za giza then unaomba ushauriwe nini?? Kama uko neutral utapata shida sana ni bora uwe upande mmoja, mtegemee Mungu (my first advice) au mtegemee shetani but remember "if you can't fight them, join them "
 
Ngoja nijaribu tuone.
Je, ww sio mmoja wao? ID hyo
 
Watakuua hao, maana ni wazi kua "hujielewi" unasema huamini katika kujikinga na nguvu za giza then unaomba ushauriwe nini?? Kama uko neutral utapata shida sana ni bora uwe upande mmoja, mtegemee Mungu (my first advice) au mtegemee shetani but remember "if you can't fight them, join them "
Ninaimani ya dini, lakini sijaiva coz matokeo nimeyaona jana pamoja na kupga maombi lkn nlifua dafu, ndo maana naomba msaada wenu walozi wa JF nimegeeni mbinu rahisi
 
Ahaa Kumbe umeamua kuomba msaada kwa walozi Subiri waje
Kama hata unambinu ya kimafia lete mkuu, me nateseka. Hapa kuna mtu kaniambia nichome mavi ya punda kwenye kifuu, ndo natest apa, ila nimetumia ya ng'ombe coz punda adim sana mjin hapa
 
Mkuu maombi ni silaha katika kila jambo, Muombe Mungu na mkabidhi yesu maisha yako hakika hautapata tabu tena , wachawi watakuja Kwa njia moja Ila watasambaratika Kwa njia sana. Mtegemee Mungu, Kwa akili zetu au sijui njia za asili ni bure mkuu. Hata hizo nguvu za giza ni kujidanganya tu hazina kitu. Mungu ndie muweza wa yote. Omba mkuu Mungu hachelewi.
Ahsante, naamini utamuomba sana Mwenyezi Mungu.
 
washa taa wafungulie mziki wa alikiba huu mpya au huyu wa rickross wa haleluja...watatulia utalala salama salimin
 
Enjoy the show kama hutaki maombi au tunguri!
Nadhani anaona raha huyu kupapaswa na hao wajomba zake popobawa
 
Back
Top Bottom