kilambimkwidu
JF-Expert Member
- Jul 21, 2017
- 6,097
- 7,199
Jana sijalala, leo nakesha:
Pazia linapepea kama bendera wakati hali iko tulivu wala hakuna upepo kabisa. Naskia purukushani za popo na mbio za mapanya kwenye 'silingibodi", sio kawaida. Mapaka yanalia nje kwa sauti kama ya watoto na yanaparuzana kwa makucha na kufokeana kwa sauti za ukali. Mlango naskia unagongwa kama mtu anaomba kuingia, nikifungua hamna kitu. Minyato ya mtu kutembea na milio kama ya 'matiti-ndala' (paaapaaa, paaapaaa) yanasikika kama mwanamke mzee ambye hajavaa sindilia anarukaruka ndani kwangu. Jana nlishusha chandarua baada ya muda nikashtuka naumwa na mbu, kumbe chandarua imeshakunjwa. Nikashusha tena, ikapandishwa, kama mara4 hivi. Nikajua lazma wachawi wameingia, nawangiwa. Na leo sipaelewielewi hapa.
Bila kutumia nguvu za giza na maombi, kuna njia zipi (za kiasili labda) zitakazofanya wachawi wasiweze kabisa kuniwangia mimi binafsi wala kusogelea mji wangu. Niweke nini, nivae nini au nifukize vitu gani ili kuwakomoa hawa majamaa. Mimi siamini ktk kujikinga kwa nguvu za giza lkn pia bado sijaiva, sina nguvu ya maombi.
Ushauri wenu wajuzi wa haya mambo
Cc. Mshana jr, Mti Mkavu, Yericko, walozi, wachawi na waaguaji wote JF