Nipashe: Mchakato wa Chato kuwa mkoa umekamilika

Kajifunze immigration ya makabila ya Tanzania yalivyokuwa yakimove. nimekwamvia hujui kitu. Kikerewe, kizinza, kisubi na kihaya ni kama lugha moja tu. Kawaulize babu zako watakuambia.
Hebu Soma hapa ujue wahaya ni wakina nani
Sio unakuwa mbishi na makabila ya watu

mkuu, Wahaya kama wahaya pia wamegawanyika kama kama walivyo wachaga na makabila mengine. Kwa wahaya Tofauti hiyo ya mafungu husababishwa na tofauti ya asili na mgawanyiko wa kiutawala wa ‘abakama' ambapo kila kundi lilikuwa na ‘mkama' wake. 'mkama' ni chifu na abakama ni wingi wa neno hilo, yaani machifu.

  • Waziba wanaotokea Kiziba
  • Wayoza wanatokea Kyamtwara,
  • Waendagabo wanatokea Bugabo
  • Wahamba wanatokea Kihanja
  • Wanyambo wanatokea Karagwe
  • Wanyahiyangiro wanaotokea Muleba

Kuna makundi mengine yanahusishwa na wahaya lakini wao wenyewe hawajihusishi nao kwenye asili yao kwa maana huchukuliwa kuwa ni wageni, hawa ni Wahangaza na Wasubi wanaotokea Ngara mpakani na Burundi na Biharamuro, wanajitofautisha na makundi haya, hasa kutokana hata na lugha za watu wanaosikilizana nao ambao ni Warundi, Wanyarwanda na Waha wa Kigoma ambao wanapatikana pia Kakonko karibu na Ngara.

Fungu la mwisho lenye kundi moja ni lile lenye Wakara wa kutoka Bukara Maruku na wale wa Bukara Kisiwani. Pana utata fulani kuhusu kundi hil. Katika hayo majina ya makundi, tofauti inasababishwa pia na asili licha ya ule mgawanyiko wa utawala wa kihimaya.

Kuhusu Waziba kudharauliwa na wahaya wengine sikubaliani nalo kwasababu wahaya sehemu zozote tunazoishi basi tunaishi kama ndugu wamoja.




Wahaya wote tunaelewana kwa lugha isipokuwa wahangaza na wasubi ambao ni wahamiaji kutoka Rwanda na Burundi. Wahaya tunatofautiana katika kuongea mfano Sisi watu wa Kiziba huwa tunavuta sana maneno na kuonekana kama tunadharau.

Mfano matangazo mengi wanayoiga/kuongea kwa lugha ya kihaya basi yale maneno wanavyotamka ndivyo waziba Tunavyoongea ( huyu naaaye hebu tuma SMS - Jay Millions)
 
Hapa umepuyanga tu. Kisubi hakifanani na Kihangaza wala kiha bali kinafanana na kihaya. Ni kama mnyamwezi na msukuma. Narudia tena kikerewe original na kizinza kinafanana sana tu na kihaya. Mzinza anaweza akaongea kizinza na mhaya akaongea kihaya na wakaelewana vizuri tu. Kihangaza na kiha hakifanani na kihaya ila kisubi, kizinza na kikerewe wanachoongea wasilanga(watawala) ni sawa tu na kihaya.
 
Source yako ni ipi.

Yaan unajifanya unajua wahaya kuliko wahaya wanavyojijua[emoji23]

Maana mie nimecopy kutoka dictionary ya kihaya
 
Ndugu yangu instanbul inawezekana uko sahihi ila mimi ninakuambia kwamba hao wazinza, wasubi na wakerewe original lugha yao inafanana sana na kihaya ila tofauti ni matamshi tu. Ni kama mnyamwezi na msukuma tu. Waulize wazee wa kihaya watakubaliana na hichi ninachokuambia. Vinginevyo uwe na usiku mwema.
Source yako ni ipi.

Yaan unajifanya unajua wahaya kuliko wahaya wanavyojijua[emoji23]

Maana mie nimecopy kutoka dictionary ya kihaya
 
Nakumbuka uchaguzi wa 2015 ulikua kada kindakindaki wa magufuli leo imekuaje tena?
Mi ni CCM kindakindaki haswa, hata huo mwaka nilimpigia mamvi na mwaka uliofuata nikampigia tundu.

Sometimes we need changes.

Hatufungwi,
 
We we ni jinga LA mwisho.soko LA dhahabu lipo geita tena kubwa sana nadhani kuliko yeyote tz
 
Kuijua vp.. ?! Yani huo mkoa wa geita tu. Haujatimiza hata miaka 10 leo ndani ya mkoa nao tupate mkoa mwingine..
Hakika mwendazke angekuwepo leo chattle ingekuwa nchi

Binafsi nimefurahi sana geita kuwa mkoa.....chato pia naitakia hivyo hivyo.
 
Niliambiwa kuwa kuna tofauti kati ya Wasubi (Biharamulo) na Washubi (Ngara). Nachelea kusema instanbul kama kawaida alishindwa kuandika h akajikuta anaongelea kabila jingine
 
Chato ni zao la Mkoa wa Kagera, kumbuka hii Wilaya ilimegwa kule na Wilaya zinazolengwa kuunda Mkoa wa chato ni pamoja na Ngara,Biharamulo na Chato yenyewe labda wataongeza Wilaya nyingine.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…